Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Adam aliumbwa bila kifo ila kifo kilikuja baada ya kula mti wa katikati,rejea kauli ya Mungu alipowaambia kuwa mkila tunda la mti huo mtakufa,kama walikuwa wanakufa tangu mwanzo asingewaambia hilo
Kilichotokea ni Mungu kuweka ulinzi kwenye bustani ya eden ili Adam asijekula mti wa uzima wakaishi milele,kumbuka mti huu waliruhusiwa kula matunda yake kabla ya wao kula huo mti wa ujuzi wa mema na mabaya,aliweka ulinzi ili wasije wakala na wakaishi milele
Hiyo inamaana kuwa tunda la ujuzi wa mema na mabaya liliwasababishia kifo lakini kama wangekula tunda la uzima wangeishi milele kitu ambacho hakikuwa chema kwa Mungu
Mungu alitaka tuishi milele lakini bila kuwa na ujuzi wa mema na mabaya kwakuwa hatukustahili hilo,lakini tulipokula ndipo kifo kilipozaliwa ndani mwetu
How?
Ishmael aliposema kuwa Mugu yuko juu ya logic hakusema kuwa Mungu ni kinyume cha logic bali Mungu ni zaidi ya logic
Logic tulionayo haiwezi na imeshindwa kuthibitisha uwepo wa Mungu kwa namna ya kushikika kama vile unavyoweza kuona kuwa 2+2=4 na unaiona nne,kama kuna logic inayoweza kufanya hivyo basi sio hii tuliyonayo ni nyingine ambayo ni kubwa kuliko hii
Mtu anapohoji kifo na jinsi mungu alivyoachia kifo, hahoji tu jinsi Adam alivyokufa.
Mimi nahoji ule uwezekano mzima wa kifo kuwezekana, ambao lazima uliumbwa na mungu katika original configurations za ulimwengu kwa mujibu wa worldview yenu. Kwa nini mungu aliachia uwezekano wa kifo kuwepo hata kabla Adam hajaumbwa?
Au unataka kusema mungu hakuumba uwezekano wa kifo, ulimshinda tu na kutokea wenyewe?
Unawezaje kuthibitisha kwamba mungu yupo, let alone yuko zaidi ya logic?
Huwezi kuanza kuzungumzia kwamba mungu yupo juu ya logic kabla hata hujathibitisha kwamba mungu yupo.
Hilo litakuwa ni sawa na kurahisisha argument yako by fiat.
Mtu mwingine anaweza kutumia non argument yako na kusema "Santa Claus exists and he lives at the North Pole, you can't really see him because he is beyond logic".
What is the difference between that and you saying mungu yupo juu ya logic?
Tutajuaje kwamba hili ni jambo la kweli na si hadithi tu?
Unaweza kuthibitisha?
Nishaongelea sana habari za "Deus ex machina" hapa. Inaonekana hii habari ya mungu kuwa juu ya logic ni classic "Deus ex machina".
http://en.wikipedia.org/wiki/Deus_ex_machina