If it is government funds, why call it Samia scholarships?

If it is government funds, why call it Samia scholarships?

Kuna mambo mengi sana ya kurekebisha kwenye nchi yetu tatizo ni kila ukiangalia huoni mtu sahihi wa kuyafanya.

Hizi pesa zingewekwa kwenye mfuko wa bodi ya mikopo, watoto wengi sana wa masikini wangenufaika nazo.

Tunaendelea kubuni vitu nje ya mfumo wa kisheria wakati vile vilivyo kwenye mfumo wa kisheria tumeshindwa kuvitekeleza kwa japo 70%.

Kwa vigezo vya hiyo inayoitwa scholarship, wenye sifa karibu 98% ni watoto ambao wazazi wao wanaweza kuwasomesha bila mikopo. Hapa naomba isitafsiriwe kuwa watoto wa wenye nacho hawapaswi kutazamwa lakini tuangalie hali ya wanaopitia watoto wanaosoma shule ambazo haya sehemu ya kukaa ni ya kugombania. Je wanaweza kushindana na wale wanaofika shuleni na kukuta kila kitu huko?

Kila siku ukikaa na kujiuliza hii nchi ina matatizo gani, sidhani kama utaweza kupata afya.
Tunataka katiba mpya. Rais ana mamlaka makubwa sana mpaka sasa amefikia hatua ya kutumia fedha za serikali kujitangazia scholarship ambayo awali haikuwepo kwenye mipango na bajeti ya nchi. Sasa italazimika kuingizwa kwa manufaa binafsi ya kisiasa ya Rais.
 
It's how we operate. How we treat our leaders. Godlike. It's as if every cent they approve it's coming from the pockets!
Try watching TBC just for 1 hr. I dare you!
If not wanting to smash your TV you will be depressed the whole day![emoji24][emoji855][emoji35][emoji34]
In such institutions, is where the most bogus people, you will find.
 
Kuna maslahi zaidi ya kusomesha bure wanaofaulu vizuri?

Hilo la dini umelitoa wapi? Unaota?

Punguani wahed.
Lugha unayotumia inadhihirisha wewe huenda ndiye punguani. Kama una akili, japo kidogo, ujibu au ujadili hoja yake, na ndivyo wenye akili wote wanavyofanya.
 
Rais Samia pesa anatoa wapi za kuwapa watu ufadhili? Au sijaelewa? If it is government funds, why call it Samia scholarships?
Inasikitisha Sana kila jambo kufanyika Kisiasa Kwa nini pesa ya serikali itumike kwa Jina la mtu binafsi.

Huyu Katoa wapi hizo billions za scholarship. Kwa nini hizo pesa zisiende HESLB.

Hata huko ulaya nchi ndo hutoa scholarship au tasisi Fulani Sasa yeye anatoa scholarship kama Nani wakati ni raisi wa watu wote.


Jingine Best students mara zote ni watoto wa wenye nazo na wenye uelewa kuhusu elimu. Inshort hakuna motivation yoyote anayofanya. Bali kaamua kusomesha watoto wa vibosile huku kayumba hali itabaki palepale kulia na bodi ya mkopo.

Mwisho tunataka kujua hizo hela anazipata wapi?
 
Wazo la Samia? Acheni utani jamani!
Ni idea yake ya kuweka hamasa everyone comes with their own motivations on multiple aspects along the line during their monstership .
Being positive is the best regardless of the situation, the government is a collective wheel, it's functionality is preditermined by bosses- The worse is for the subordinates and the good ones are for the bosses.

She deserves more credits for this, may be the criteria on who gets and on what bases should be placed under general public scrutiny.

We have had historical proof on how severally good things have badly failed. The bottom line has party been poor operationalization of plans.

Some of things with public and inclusivity faces requires a closer monitoring process on implementation phase.

I wish her to be the supreme observer for a better and desirable implementation of the amazing scholarships that triggers science destined horizon for our daughters and sons.

I have exercised my right to commend her Excellency SSH.
 
Haya unayoeleza ndo yananifanya nisione kama tuna waziri anayefaa. Wizara hii haijawahi pata waziri mzuri kwa kipindi kirefu. Huyu ni Profesa lakini pia yaonekana hana ubunifu wa kuinua elimu.

Haya uliyoyasema ni mazuri sana. Ongezea ukweli kwamba huwezi kuinua elimu vyuo vikuu wakati sekondari ziko hoi kiasi tunachokiona nchini. Hakuna maabara ikimaanisha hakuna practices za chemistry, biology na physics, na hakuna waalimu wa hesabu/hisabati. Yeye akiwa Waziri alistahili kuliona hilo, lakini naona shortsightedness haiondoki kwa kusoma PhD.
Viongozi wetu wameishiwa ubunifu, wamechoka na hawawezi tena kitu.

Kuna watu wachache wanadai huu ni mpango wa kuchochea watoto wapende masomo ya sayansi, sasa najiuliza mbona Bodi ya mikopo miaka yote imekuwa ikitoa kipaumbele kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi?

Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuwashindanisha watoto waliosoma shule za kata na wale wa shule za Private kama Feza. Hawa watoto wana kila kitu kinachoweza kuwafanya wafanye vizuri kwenye masomo hayo ya sayansi.

Kinachonisikitisha mimi ni watoto wa kimaskini waliosoma kwa shida wanakosa mikopo au wanapewa pesa kidogo(tena watakuja kuzilipa) ila pesa nyingi za umma zinakwenda kusomesha watoto ambao wazazi wao wana uwezo wa kuwasomesha hata vyuo vya Ulaya huko. Hii ni dhambi tu kama dhambi nyingine.
 
Rais Samia pesa anatoa wapi za kuwapa watu ufadhili? Au sijaelewa? If it is government funds, why call it Samia scholarships?
Mkuu, naona sasa umeanza kuelewa jinsi kampeni na propaganda zinavyofanyika. Hongera sana!
 
Katika kuanzisha foundations kama hizo za kutoa financial , kuitwa jina la mtu linaonesha ownership/possession of that foundation being serviced with own money. sasa Samia anatumia fedha za serikali. Haipashwi kuitwa jina lake!
 
Back
Top Bottom