Unabakije kuwa kiongozi au mzazi/mlezi kama unakuja na mipango ya kibaguzi ya aina hii? Kwa hiyo watoto wasiofanya vizuri kwenye masomo lakini Mola amewajalia vipaji kwenye mambo mengine wao hawastahili ufadhili wake? Ni sawa na mzazi ana watoto watatu wanasoma darasa moja, wawili hawafanyi vizuri kwenye masomo, mmoja ndiye anafanya vizuri..kwa hiyo ni sahihi mzazi kumsomesha huyo mmoja anayefanya vizuri na kumgharimia vyote atakavyo na hawa wawili wao hata waache shule wakachunge ni sawa, nadhani mzazi mwenye kujua wajibu wake atatumia rasilimali kadiri awezavyo kusaidia hawa wawili zaidi kuliko huyo mmoja!
Lakini pia, utaanzishaje scholarship bila kutaja vyanzo vya resources za huo ufadhili? Kiongozi mwema ni yule anayelenga kusaidia zaidi wenye uwezo mdogo kuliko wanaojiweza..WENYE AFYA HAWAHITAJI DAKTARI BALI WALIO WAGONJWA..na kutaja vyanzo vya funding ili wengine wenye nafasi washiriki kuchanga ili wanufaika wawe wengi kwa kuangalia uhitaji zaidi na sio ufaulu tu!