If it is government funds, why call it Samia scholarships?

If it is government funds, why call it Samia scholarships?

Daraja la Kijazi ama Mfugale ni fedha za Umma why yanaitwa hivyo?

Airport je?
Hostel ya JPM je?
Mkicomment narudi
Hebu tofautisha Fedha na kitu? Kitu lazima kipewe Jina ndio maana madaraja, airport yanapewa majina...ila fedha kama fedha iliyo katika mfumo wa karatasi huwezi ipa Jina lako labda uwe wewe ndio ume izalisha.
 
Rais Samia pesa anatoa wapi za kuwapa watu ufadhili? Au sijaelewa? If it is government funds, why call it Samia scholarships?
Unahangaika bure,umewahi sikia kitu inaitwa Obamacare? Pesa zilikuwa za Obama? Muachage ujinga basi..

Sasa kwa taarifa yako sio tuu Kuna hiyo Samia Scholarship Bali Kuna Samia Housing Scheme pia.
 
Kuna mambo mengi sana ya kurekebisha kwenye nchi yetu tatizo ni kila ukiangalia huoni mtu sahihi wa kuyafanya.

Hizi pesa zingewekwa kwenye mfuko wa bodi ya mikopo, watoto wengi sana wa masikini wangenufaika nazo.

Tunaendelea kubuni vitu nje ya mfumo wa kisheria wakati vile vilivyo kwenye mfumo wa kisheria tumeshindwa kuvitekeleza kwa japo 70%.

Kwa vigezo vya hiyo inayoitwa scholarship, wenye sifa karibu 98% ni watoto ambao wazazi wao wanaweza kuwasomesha bila mikopo. Hapa naomba isitafsiriwe kuwa watoto wa wenye nacho hawapaswi kutazamwa lakini tuangalie hali ya wanaopitia watoto wanaosoma shule ambazo haya sehemu ya kukaa ni ya kugombania. Je wanaweza kushindana na wale wanaofika shuleni na kukuta kila kitu huko?

Kila siku ukikaa na kujiuliza hii nchi ina matatizo gani, sidhani kama utaweza kupata afya.
Wengine tuliishaliona kitambo kuwa sasa wanaanza kuwagawa watoto wa maskini na wa matajiri halafu mmoja kaandika humu jf kuwa hela hizo zinaenda kuwanufaisha watoto wa maskini.nchi hii ngumu sana na kizazi kilichopo sasa ni cha ajabu sana.
 
hii nchi bora tusingepewa uhuru tu kuliko kuangukia kwenye mikono ya CCM.
 
Rais Samia pesa anatoa wapi za kuwapa watu ufadhili? Au sijaelewa? If it is government funds, why call it Samia scholarships?
Ni kweli government funds, lakini aliye elekeza hizo funds ziende kwa ajili ya scholarship ni Madamme Samia , angetaka kuzielekeza kwenye matumizi mengine kusingekuwa na hiyo scholarship.
Ndio maana ukipewa mkopo na benki husemi nimepewa mkopo na depositors wa benki , kwa sababu benki kama benki hawana pesa zao bali unasema nimepewa mkopo na benki.
 
Kama ni Government funds sio sahihi kutumia jina lake while ni wananchi wanachangia 100% kwa pesa zao.

The good things would have been kuanzisha foundation yake baada ya kutoka madarakani na kuchangisha pesa kwa.wadau then anatoa hizo.scholarhip.

Ila utaratibu huu sio sawa.
 
Rais Samia pesa anatoa wapi za kuwapa watu ufadhili? Au sijaelewa? If it is government funds, why call it Samia scholarships?
Ili aweze kugawa anaowataka yeye kwa upendeleo.

Haya ndiyo mambo ya kipuuzi kabisa yanayoonyesha ni kiasi gani nchi imekuwa ya kijinga kabisa.
 
Amepotezaje mwelekeo wakati anatoa scholarship? Au mwenzetu hufahamu maana ya scholarship?
Hakuna taasisi inayoshughulikia mambo hayo, bali inabidi yeye ndiye awe mhusika?

Kuna maana gani ya kuwepo na watumishi kama yeye ndiye anayeweza kusimamia kila kitu.
 
Back
Top Bottom