Kuna mambo mengi sana ya kurekebisha kwenye nchi yetu tatizo ni kila ukiangalia huoni mtu sahihi wa kuyafanya.
Hizi pesa zingewekwa kwenye mfuko wa bodi ya mikopo, watoto wengi sana wa masikini wangenufaika nazo.
Tunaendelea kubuni vitu nje ya mfumo wa kisheria wakati vile vilivyo kwenye mfumo wa kisheria tumeshindwa kuvitekeleza kwa japo 70%.
Kwa vigezo vya hiyo inayoitwa scholarship, wenye sifa karibu 98% ni watoto ambao wazazi wao wanaweza kuwasomesha bila mikopo. Hapa naomba isitafsiriwe kuwa watoto wa wenye nacho hawapaswi kutazamwa lakini tuangalie hali ya wanaopitia watoto wanaosoma shule ambazo haya sehemu ya kukaa ni ya kugombania. Je wanaweza kushindana na wale wanaofika shuleni na kukuta kila kitu huko?
Kila siku ukikaa na kujiuliza hii nchi ina matatizo gani, sidhani kama utaweza kupata afya.