Ifahamu nchi kubwa kuliko zote duniani

Ifahamu nchi kubwa kuliko zote duniani

IJUE NCHI KUBWA KULIKO ZOTE.

Je, unafahamu kuwa Urusi (Russia)/ USSR Ndio nchi inayo shika rekodi ya kua nchi kubwa kuliko nchi yeyote duniani?

Basi fahamu Kuhusu ukubwa wake, eneo lake kwa ukubwa ni 17,075,400km² za mraba (million17.1km²), ambayo sawa na 12,577mile kwa urefu.

Pia Urusi inachukua 11% ya eneo lote la nchi kavu duniani.

Na imepakana na nchi 14 ambazo ni North Korea, China, Norway, Finland, Ukraine, Georgia, Mongolia, Latvia, Estonia, Azerbaijan, Belarus, Lithuania, Abkhazia na South Ossetia.

Lakini pia nchi hii imepakana na Taifa la Marekani ikiwa imetenganishwa na Bahari. Iko karibu vilevile na maeneo ya Marekani (jimbo la Alaska liko ng'ambo ya mlango wa Bering) na Japani (kisiwa cha Hokkaido kiko ng'ambo ya mlango wa La Pérouse.

Urusi Pia inajumla ya wakazi 145,934,000 yaani Wanaume wakiwa 67,640,000 ambao sawa na 47% ya wakazi Wake na wanawake wakiwa 78,294,000 sawa na 53% ya wakazi wake wote.

Lakini pia Russia ni nchi ambayo imeingia (inapatikana) katika mabara mawili tofauti yaani Asia na Ulaya licha ya kuwa Russia rasmi hupatikana Bara la Asia
Pia maajabu yaliyopo ndani ya Russia ni kwamba kuna baadhi ya maeneo yanatofautiana hadi masaa 11. Yaani eneo moja la Russia linaweza kua saa 12 asubuhi wakati huo huo eneo jingine ni saa 10 jioni.

Hiyo ndo Russia na hayo ni machache kuhusu Urusi
TANZANIA inaingia mara ngapi hapo?
 
Ila wanaliwa kichwa na Ukraine kinchi kama Rwanda tu [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]
USA, EU, NATO + UKRAINE, wote hao wameungana kuipiga Urusi lakini bado wanachezea kichapo. Amka ndugu!
 
Yani pamoja na ukubwa wote huo bado ana tamaa na kaeneo kadogo ka ukraine?
Siyo tamaa bali ni sababu za kiusalama zaidi lakini kwa sisi Watanzania kwetu suala la usalama sio tatizo kwasababu WAZUNGU wanaweza kuja na kuchukua chochote na kuondoka muda wowote kwenye nchi yetu
 
Ila inakalishwa na ukraine kanchi kadogo 🤣🤣🤣🤣🤣😀😂😂 big up ukraine nyie ni shupavuu sanaaa hata kama mkielemewa but mmeonesha umwamba wenu bila chenga
 
Ila inakalishwa na ukraine kanchi kadogo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji3][emoji23][emoji23] big up ukraine nyie ni shupavuu sanaaa hata kama mkielemewa but mmeonesha umwamba wenu bila chenga
We mwenyewe unajicheka Kwa Sababu unajua unachoongea hakiko sahihi.
 
Japani ukubwa wake ni sawa na mkoa wa Singida lakini wametuzidi kwa kila kitu watanzania

Ukubwa wa nchi sio kitu kikubwa
 
Siyo tamaa bali ni sababu za kiusalama zaidi lakini kwa sisi Watanzania kwetu suala la usalama sio tatizo kwasababu WAZUNGU wanaweza kuja na kuchukua chochote na kuondoka muda wowote kwenye nchi yetu
Sababu kama zipi?

Mbona nilisikia ni mpango wake kuiteka keilviv
 
Bando langu leo limenifanya nijifunze mambo kadhaa katika huu uzi.

1.russia ndiyo nchi kubwa duniani.

2.mashariki na magharibi ya russia inatofautiana kwa masaa 11.

3.russia ukubwa wake imepakana ana marekani huku boundary yao ikiwa ni maji ya bahari ambayo wakati wa baridi kali maji hayo huganda na kugeuka barafu kiasi kwwmba unaweza kutembea juu kutoka russia mpaka marekani.

Kumbe mrusi jirani yake ni marekani tena wametenganishwa na bahari tu.

Nashkuru Mungu kwa kunifanya nijiunge JF
Ongezea hii, hapo zamani za kale Marekani hapakuwa na watu wanaoishi hapo, wahindi wekundu wakati wanawinda dubu kutokea Mongolia wakajikuta wametokea Marekani na bahari imeshayeyuka barafu hawakuweza kurudi tena nyuma ili kurudi Urusi mpaka kwao. (Mfano kutoka Dar kwenda Zanzibar winter ikubali mnatembea kwa miguu kwenda Zanzibar, baada ya winter ndio mnashtuka barafu imeyeyuka kumbe kuna bahari mnashindwa kurudi Dar mnaanzisha maisha huko mpaka vizazi na vizazi, ndio sababu kihistoria unaambiwa Marekani ni nchi ya wahindi wekundu ndio wa kwanza kufika hapo

Algeria ndio nchi kubwa Africa lakini sehemu kubwa haikaliwi na watu, sawa na Urusi wana eneo kubwa ambalo ni useless ni barafu tupu na wala halitumiki.
 
Aises hatari.

Sasa hawa wahindi wekundu wako wapi?

Na ilikuwaje wakapotea race yao wakaja hawa akina trampu ?
 
ongeza na Hii,
Waliuza Jimbo la Alaska wakiwa wamewaka yaani wamepiga mavitu Yao Ugimbi aina ya Vodka
Wakauza Kwa vijisent
(in Chenge voices )
Pesa ikatumika kumcheza ngoma mwali aliyekwisha tolewa bikra na wahuni

Wakaja shtuka pombe ilivyoisha wapo na Hangover Ndio wanaona
Bendera Yenye manyota nyota Inapepea
Walipiga yowe lakini haikusaidia

Tsar:Hawa American wamevamia nchi yetu na kuweka bendera Yao!

Yktak kolochev:Mweshimiwa mfalme mbona umeuza Alaska Jana usiku!

Tsar:Nimeuza Alaska Jana hii inawezekanaje?

Yktak kolochev:Ulikua umelewa sana Mweshimiwa mfalme na Bolishev alipotaka kukuzuia ulimpiga risasi ya kichwa binamu Yako Ndio kafa hivyo!
Tsar:Ati niniiiiii,uwiiiiiii uwiiiii inawezekanaje?

Yktak kolochev:Mkataba wa kuuza Alaska huu hapa Kuanzia Leo kule ni Marekani yaani Tena Jana ulivyolewa Ulikua na furaha sana kiasi Kwamba ulimtoa mke wako Kwa Mr Washington Jr kama zawadi amtumie apendavyo na Kwa taarifa za chini chini alimpa 076...yaani

Tsar:mamaaaa weeeee uwiiiiiii Vodka vodka vodka
Imenitendea Nini Mimi Leo ni msiba mkubwaaaaa,najutaaaaa!

[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji91][emoji91][emoji91]
***** sisi ambao hatujasoma kazi tunayo
 
Back
Top Bottom