new user2025
JF-Expert Member
- Jun 18, 2025
- 236
- 358
sijajua andiko lako niliiteje, ila lina sifa zifuatazoMuslim Brotherhood, ilianzishwa mwaka 1928 nchini Misri, ni shirika la kimataifa la Kiislamu la Sunni linalolenga kutekeleza sharia na kuanzisha caliphate ya kimataifa.
Itikadi zao zimezijenga vikundi vya kigaidi vingi duniania ikiwemo hamas na al-qaeda.
Mataifa kama Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Misri, Jordan, na Bahrain yanaiteua kuwa shirika la kigaidi kwa ushirika wao katika kufadhili vikundi vya kigaidi.
Qatar na Turkey ndio wamebaki kuwa support. Kama mnavyoelewa Qatar iliwapa hospitality viongozi wa hamas na kuenjoy mabilioni yao pale pia Uturuki ni nchi ambayo inayo support uwepo wa hamas na ugaidi wake.
BAADHI YA MATUKIO YALIYOFANYWA NA MUSLIM BROTHERHOOD:
Mwaka 2013,Wafuasi wa Brotherhood walipora na kuchoma vituo vya polisi na makumi ya makanisa ya Kikristo huko Misri.
Mwaka 1982, Kundi hilo nchini Syria liliongoza uasi wa kutumia silaha dhidi ya Serikali. Mapigano haya yalisababisha mauaji ya takriban watu 10,000–40,000, wengi wao wakiwa raia, katika mzingiro wa kikatili.
Mnamo Aprili 2025, Jordan iliwakamata wanachama 16 wa Muslim Brotherhood wanaotuhumiwa kupanga mashambulizi kwa kutumia roketi na ndege zisizo na rubani.
@hujataja vyanzo vya haya maelezo yako(mtu hawezi kuaminii maneno yaliyoandikwa bila ushahidi)
@unaonekana maelezo yako yameegemea uapnde mmoja(hakuna namna yeyote inaonyesha kauli au ushahidi wa mojakwa moja kkutoka kwenye kundi)
@haujatoa suluhisho,yaani baada ya yote hayo kufanyika kwenye habari yako hamna suluhisho labda bado wapo,wamesambaratishwa au kuna jitihada gani za kuondolowa au kuendelzwa hilo kundi
@nakupa 100% kwenye title, moja ya title bora zizovutia(umenishawishi hadi kufungua nisome)
@kwakua andiko lako limehusisha dini(entity kubwa) ulitakiwa uandike vitu wazi, ushahidi wa kutosha na maandiko ya kweli(uwe na ushahidi unachoandika ni kweli)
MWISHO! Nina imani muda uliotumia kuandaa title, ndio muda bora zaidi kuliko andiko lenyewe