Nimejibu swali lako na mimi naomva ni kuulize hili swali hapa, je?
Maana ya muweza wa yote kwa mapenzi yake ni nini?
Hujajibu swali langu. Unarukaruka tu.
Unaelewa kwamba, kwa maelezo yako, Mungu wako huyo unayemsema, akijua kwamba utaiba kesho, huwezi kuepuka kuiba?
Unakubali hilo au unakataa?
"Muweza yote kwa mapenzi yake" si muweza yote. Kwa sababu uwezo wake umefungwa ndani ya mapenzi yake. Maana yake kuna mambo hawezi kufanya. Mungu wa Biblia na Quran anasemwa kuwa muweza yote, uwezo wake hauna mipaka. Huyo "muweza yote kwa mapenzi yake" ni mwenye mipaka ya uwezo wake.Si Mungu, ni dubwana tu.
Kwa sababu uwezo wake una mipaka.
Zaidi, hata nikikuruhusu useme Mungu huyo "muweza yote kwa mapenzi yake" yupo, na ndiye aliyeumba ulimwengu huu, na kauumba kwa mapenzi yake, nikikuuliza, kwa nini mapenzi yake yamekuwa kuumba ulimwengu ambao unaweza kuwa na mabaya, wakati ana upendo mkubwa kwa viumbe vyake, na aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kuwepo, unarudi pale pale uliposhindwa kujibu.
Muweza wa yote ni hoja ya kufikirika ambayo kiuhalisia haipo.
Kwa sababu kuweza yote maana yake ni kuweza kufanya mambo yanayojicontradict, kama Mungu kuumba jiwe ambalo hawezi kulibeba.
Mungu anaweza kuumba jiwe ambalo hawezi kulibeba?
Akiweza kuumba jiwe hilo, kutakuwa na kitu hawezi kufanya, kwa sababu atakuwa hawezi kubeba jiwe hilo.
Akiwa hawezi kuumba jiwe hilo, kutakuwa na kitu hawezi, atakuwa hawezi kuumba jiwe hilo.
Vyovyote vile hapo, Mungu hawezi yote.
N aukiruhusu contradiction, maana yake umeruhusu unaposema Mungu yupo, umaanishe Mungu hayupo!