Ifikapo 2030 hizi nyimbo za kipuuzi za bongo flava zitaiharibu jamii nzima

tpaul

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
24,225
Reaction score
22,632
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, ndivyo unavyoweza kusema. Nipo kwenye basi natokea Songea kwenda Mwanza, safari nzima tunasikilizishwa nyimbo na video za kihuni za bongo flava mwanzo mwisho. Baadhi ya nyimbo zinazopigwa humu ni hizi:

1. Kila demu ana matako.
2. Nataka kunya
3. Nitongoze
4. Nipe tamu yangu
5. Finyia ndani
6. Hapo kati

Wewe fikiria nyimbo za kipumbavu na kipuuzi kama hizi zinapigwa na kuchezwa hadharani kwenye video. Maadili ya jamii yatabaki salama? Ukija kwenye video ndiko kwenye balaa zaidi. Mabinti wanacheza uchi huku wakishikwashikwa matiti na makalio hadi kero. Tukienda na mwendo huu hadi 2030, jamii itakuwa imeharibiwa sana na nyimbo hizi za ajabu ajabu.

Watu hadi tunashindwa kusafiri na watoto pamoja na wakwe zetu kwa sababu ya kuogopa kuaibika kutazamishwa video za kingono zinazochezwa kwenye mabasi haya. Chanzo kimojawapo cha kusambaza uharibifu wa maadili potovu yaliyomo kwenye nyimbo za bongo flava ni kupitia mabasi ya daladala na haya ya mikoani

Ifike wakati serikali ipige marufuku nyimbo na video hizi za kihuni kupigwa kwenye mabasi ili kuepuka kusambaza sumu ya uharibifu wa maadili katika jamii. Mwisho wa siku serikali itakuja kuwalaumu wazazi wakati yenyewe ndiyo imeshindwa kusimamia utaratibu wa kistaarabu na kimaadili ktk jamii.

Tujifunze kutokana na makosa ya wengine. Wazungu waliruhusu mfumo wa maisha huria kwa raia wa nchi zao lakini sasa wanalia baada ya maadili ya jamii kumomonyoka kwa kiwango kisichorekebika.

Hata kama vyama vya siasa vimekuwa vikiwatumia wasanii kuimba nyimbo hizi za ovyo kwenye kampeni za kisiasa, wakati umefika sasa serikali iache kuharibu maadili ya jamii kwa kisingizio chochote kile. Tusipiziba ufa ipo siku tutajenga ukuta.​
 
Ila kwa kweli, wenye mabasi wangepewa muongozo wa aina ya vitu vya kuonyesha..tuna vivutio vya utalii kibao..tungeonyesha hivyo vitu kuliko kuonyeshana matusi. Ukisafiri na wakwe, wazazi au watoto inabidi mjifanye mmelala msisikie na kutazama yanayoendelea.
 
Cha ajabu utasikia wengine wanazipenda hizo nyimbo, ukiwawekea muziki wa maadili mema unaonekaka umri umekutupa mkono🙂
 
Kiwango cha kushuka kwa maadili kimepanda sana nchi hii. Kiwango cha ujinga nacho kiko juu kweli. Mitaani kote si akina baba wala akina mama, wote wanapenda nyimbo za kipuuzi kwa kiwango cha kutisha.

Jambo kubwa linahitaji kukomesha ujinga japo umeshika kasi mithiri ya moto wa nyikani. TCnini wale wamefeli balaa wawekwe kando wote.
 
Uje uangalie hata hadhi ya wahudumu wa mabasi hayo,utagundua na wenyewe yale yale tu.
Ila jambo la kujiuliza: zipigwe zipi? Za kilokole, si kwamba watu wote watapenda. Za kihuni hizo,si kwamba wote wanapenda. Mawaiza,si kwamba wote watapenda. Miaka ya nyuma walikua wakiweka muvi mwanzo mwisho,niliona kulikua na ahueni tofauti na sasa. Bila namkatia vibuno hawajafurahia. Hawaangalii wamebeba watoto na watu wazima. Ini shoti, wanaonaga abilia kama wahuni wenzao. Teh teh teh teh teh
 
50 50 imeleta mambo haya na inachangia 95% ya mmomonyoko wa maadili katika nchi yetu.
 
Matope kwa bata ni starehe, kwa wengine matope ni uchafu. Haitakiwi wote tubambikiwe kwenye matope kisa kuna bata kadhaa wanaona matope ni starehe. Kama kuna ambao wanapenda huo uchafu basi iwe private, sio kenye public transport.
Cha ajabu utasikia wengine wanazipenda hizo nyimbo, ukiwawekea muziki wa maadili mema unaonekaka umri umekutupa mkono🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…