Ifikapo 2030 hizi nyimbo za kipuuzi za bongo flava zitaiharibu jamii nzima

Ifikapo 2030 hizi nyimbo za kipuuzi za bongo flava zitaiharibu jamii nzima

Ila kwa kweli, wenye mabasi wangepewa muongozo wa aina ya vitu vya kuonyesha..tuna vivutio vya utalii kibao..tungeonyesha hivyo vitu kuliko kuonyeshana matusi. Ukisafiri na wakwe, wazazi au watoto inabidi mjifanye mmelala msisikie na kutazama yanayoendelea.
Halafu hawa watu wa mabasi sijui wanatuonaje......wanapenda sana kutuchezea video za bongo flava zenye maudhui ya ngono na ukahaba. Yaani mtu huwezi hata kusafiri na mtoto wako kwenye basi moja kisa nyimbo na video za ngono, bangi, ushoga, usagaji na mambo mwengine ya ovyo. Inauma sana.
 
Cha ajabu utasikia wengine wanazipenda hizo nyimbo, ukiwawekea muziki wa maadili mema unaonekaka umri umekutupa mkono🙂
Hasa hawa akina mama ndio balaa kabisa aisee! Unamkuta mama mtu mzima anashobokea nyimbo hizi za kipuuzi na kipumbavu na anajua kuimba mashairi yake hadi unashangaa kwamba huyu mama kama yupo hivi watoto wake wana hali gani na watalelewa na nani ikiwa mama yao tu anahitaji kulelewa kimaadili.🤯🤯🤯
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, ndivyo unavyoweza kusema. Nipo kwenye basi natokea Songea naenda Mwanza, safari nzima tunasikilizishwa nyimbo na video za kihuni za bongo flava mwanzo mwisho. Baadhi ya nyimbo zinazopigwa humu ni hizi:

1. Kila demu ana matako.
2. Nataka kunya
3. Nitongoze
4. Nipe tamu yangu

Wewe fikiria nyimbo za kipumbavu na kipuuzi kama hizi zinapigwa na kuchezwa hadharani kwenye video. Maadili ya jamii yatabaki salama? Ukija kwenye video ndiko kwenye balaa zaidi. Mabinti wanacheza uchi huku wskishikwashikwa matiti na makalio hadi kero. Hii nchi ina mambo ys kipumbavu ssna.

Watu tunaogopa kusafiri na watoto pamoja na wakwe zetu kwa sababu ya kuogopa kuabika kutazamishwa video za kingono zinazochezwa kwenye mabasi haya. Chanzo kimojawapo cha kusambaza uharibifu wa maadili potovu yaliyomo kwenye nyimbo za bongo ni kupitia mabasi ya daladala na haya ya mikoani

Ifike wakati serikali ipige marufuku nyimbo na video hizi za kihuni kupigwa kwenye mabasi ili kuepuka kusambaza sumu ya uharibu wa maadili katika jamii. Mwisho wa siku serikali itakuja kuanza kuwalaumu wazazi wakati yenyewe ndio imeshindwa kusimamia utaratibu wa kistaarabu na kimaadili ktk jamii.

Tujifunze kutiokana na makosa ya wengine. Wazungu waliruhusu mfumo wa maisha huria kwa raia wa nchi zao lakini sasa wanalia baada ya maadili ya jamii kumomonyoka kwa kiwango kisichorekebika. Hata kama vyama vya siasa vimekuwa vikiwatumia wasanii kuimba nyimbo hizi za ovyo kwenye kampeni za kisiasa, wakati umefika sasa serikali iache kuharibu maadili ya jamii kwa kisingizio chochote cha kisiasa. Tusipiziba ufa ipo siku tutajenga ukuta mzima.
Hizo nyimbo hazina uwezo wa kuharibu jamii.

Jamii iliyoharibika ndiyo inaachia nyimbo hizo zitamalaki.

Unaliangalia hili jambo kinyumenyume.
 
Tatizo SIO wasanii tatizo ni Wanasiasa wanaojali maslahi Yao na kupuuza Kila kitu kinachoweza kikawakosesha umaarufu.

CCM ni kichaka cha Uovu wote Tanzania na Dunia Nzima.
Ili Hii nchi iwe na Jamii Bora ni Lazima CCM IFE kifo cha asili. Yaani taifa ni Lazima lizaliwe upya Kwa kuweka misingi ya maadili Kwa Taifa . Kwa Sasa Taifa halina misingi Wala dirá ya Taifa Kwa sababu ya CCM kuweka maslahi ya chama kushika hatamu bila kujali iwe ni Kwa halali au haramu.
Wasanii wengi wanaoimba nyimbo za matusi na kuashiria ngono na maneno yasiyo na staha wanatumika sana Wakati Wa kampeni za uchaguzi. Na huko wanatumika kuharibu sana maadili ya vijana na Watoto na wanawake .
Pia wasanii Hao Hao wanatumika kwenye shughuli za Mwenge n.k.

Nchi Haina maadili ya uongozi Wa umma na kuheshimu ofisi za umma . Pia Haina maadili ya kijamii kama waafrika Kwa sababu hatujakaa kama Taifa na kuweka misingi ya maadili ya Kitanzania na kuyaweka kwenye Sheria na Katiba Kama tunu ya taifa.

Watanzania tukiendelea kuwaendekeza Wanasiasa Wachache wanaonufaika na Hali iliyopo kimaadili kuanzia kwenye utumishi ,biashara na Mitaani SIO muda Mrefu taifa litaingia kwenye mmomonyoko mkubwa sana Wa maadili na kuwa na Kizazi cha hovyo.
 
Njemba kujiita Vanilla ni 2nd derivative ya ungapu.
FB_IMG_16989997791646004.jpg
 
Hata mbuyu ulianza kama mchicha, ndivyo unavyoweza kusema. Nipo kwenye basi natokea Songea kwenda Mwanza, safari nzima tunasikilizishwa nyimbo na video za kihuni za bongo flava mwanzo mwisho. Baadhi ya nyimbo zinazopigwa humu ni hizi:

1. Kila demu ana matako.
2. Nataka kunya
3. Nitongoze
4. Nipe tamu yangu

Wewe fikiria nyimbo za kipumbavu na kipuuzi kama hizi zinapigwa na kuchezwa hadharani kwenye video. Maadili ya jamii yatabaki salama? Ukija kwenye video ndiko kwenye balaa zaidi. Mabinti wanacheza uchi huku wakishikwashikwa matiti na makalio hadi kero. Hii nchi ina mambo ya ovyo sana.

Watu hadi tunashindwa kusafiri na watoto pamoja na wakwe zetu kwa sababu ya kuogopa kuaibika kutazamishwa video za kingono zinazochezwa kwenye mabasi haya. Chanzo kimojawapo cha kusambaza uharibifu wa maadili potovu yaliyomo kwenye nyimbo za bongo flava ni kupitia mabasi ya daladala na haya ya mikoani

Ifike wakati serikali ipige marufuku nyimbo na video hizi za kihuni kupigwa kwenye mabasi ili kuepuka kusambaza sumu ya uharibifu wa maadili katika jamii. Mwisho wa siku serikali itakuja kuwalaumu wazazi wakati yenyewe ndiyo imeshindwa kusimamia utaratibu wa kistaarabu na kimaadili ktk jamii.

Tujifunze kutokana na makosa ya wengine. Wazungu waliruhusu mfumo wa maisha huria kwa raia wa nchi zao lakini sasa wanalia baada ya maadili ya jamii kumomonyoka kwa kiwango kisichorekebika.

Hata kama vyama vya siasa vimekuwa vikiwatumia wasanii kuimba nyimbo hizi za ovyo kwenye kampeni za kisiasa, wakati umefika sasa serikali iache kuharibu maadili ya jamii kwa kisingizio chochote kile. Tusipiziba ufa ipo siku tutajenga ukuta.​
Huko mbona mbali Sana mkuu... Jamii ishaisha.
 
Matope kwa bata ni starehe, kwa wengine matope ni uchafu. Haitakiwi wote tubambikiwe kwenye matope kisa kuna bata kadhaa wanaona matope ni starehe. Kama kuna ambao wanapenda huo uchafu basi iwe private, sio kenye public transport.
Mkuu umemaliza kila kitu. Hizi nyimbo za ngono kwa kweli zinatia kichefuchefu na bahati mbaya hata BASATA wanazikubali na kuzipitisha ili zije mtaani kumomonyoa maadili ya kijamii. Hii ni nchi ya kipuuzi sana.
 
Hizo nyimbo hazina uwezo wa kuharibu jamii.

Jamii iliyoharibika ndiyo inaachia nyimbo hizo zitamalaki.

Unaliangalia hili jambo kinyumenyume.
Kivipi mkuu. Hebu fafanua vizuri. Sasa unashauri nini kifanyike?
 
Tatizo SIO wasanii tatizo ni Wanasiasa wanaojali maslahi Yao na kupuuza Kila kitu kinachoweza kikawakosesha umaarufu.

CCM ni kichaka cha Uovu wote Tanzania na Dunia Nzima.
Ili Hii nchi iwe na Jamii Bora ni Lazima CCM IFE kifo cha asili. Yaani taifa ni Lazima lizaliwe upya Kwa kuweka misingi ya maadili Kwa Taifa . Kwa Sasa Taifa halina misingi Wala dirá ya Taifa Kwa sababu ya CCM kuweka maslahi ya chama kushika hatamu bila kujali iwe ni Kwa halali au haramu.
Wasanii wengi wanaoimba nyimbo za matusi na kuashiria ngono na maneno yasiyo na staha wanatumika sana Wakati Wa kampeni za uchaguzi. Na huko wanatumika kuharibu sana maadili ya vijana na Watoto na wanawake .
Pia wasanii Hao Hao wanatumika kwenye shughuli za Mwenge n.k.

Nchi Haina maadili ya uongozi Wa umma na kuheshimu ofisi za umma . Pia Haina maadili ya kijamii kama waafrika Kwa sababu hatujakaa kama Taifa na kuweka misingi ya maadili ya Kitanzania na kuyaweka kwenye Sheria na Katiba Kama tunu ya taifa.

Watanzania tukiendelea kuwaendekeza Wanasiasa Wachache wanaonufaika na Hali iliyopo kimaadili kuanzia kwenye utumishi ,biashara na Mitaani SIO muda Mrefu taifa litaingia kwenye mmomonyoko mkubwa sana Wa maadili na kuwa na Kizazi cha hovyo.
Umeongea vizuri sana mkuu. Ni kweli ukiangalia kwa jicho pevu utaona maadili yameanza kuporomoka kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi ya shina. Hapa ndipo tunapofeli kama taifa kwa sababu tumekosa msingi wa maadili ya kitaifa. Taifa lisilokuwa na maadili ni kama chai bila sukari.
 
Uje uangalie hata hadhi ya wahudumu wa mabasi hayo,utagundua na wenyewe yale yale tu.
Ila jambo la kujiuliza: zipigwe zipi? Za kilokole, si kwamba watu wote watapenda. Za kihuni hizo,si kwamba wote wanapenda. Mawaiza,si kwamba wote watapenda. Miaka ya nyuma walikua wakiweka muvi mwanzo mwisho,niliona kulikua na ahueni tofauti na sasa. Bila namkatia vibuno hawajafurahia. Hawaangalii wamebeba watoto na watu wazima. Ini shoti, wanaonaga abilia kama wahuni wenzao. Teh teh teh teh teh
Hata hizo movie ni balaa.
Nilipanda basi la BARAKA toka shamba kuja Dar iliwekwa movie moja ni aibu!
Watu wanajamiiana na watoto wamo kwenye basi wana angalia.
Hizi basi ndogo ndogo za Coaster ni shida zaidi movie haziko rated na parental guide, muziki ya singeli na bongo flava za uchiuchi tupu wanabambiana na vijora na Madera yao au na bikini.
Dkt. Gwajima D aione hii akamfikishie waziri wa uchukuzi. Sumatra wamelala fofofo.
 
Back
Top Bottom