Ifikapo 2030 hizi nyimbo za kipuuzi za bongo flava zitaiharibu jamii nzima

Halafu hawa watu wa mabasi sijui wanatuonaje......wanapenda sana kutuchezea video za bongo flava zenye maudhui ya ngono na ukahaba. Yaani mtu huwezi hata kusafiri na mtoto wako kwenye basi moja kisa nyimbo na video za ngono, bangi, ushoga, usagaji na mambo mwengine ya ovyo. Inauma sana.
 
Cha ajabu utasikia wengine wanazipenda hizo nyimbo, ukiwawekea muziki wa maadili mema unaonekaka umri umekutupa mkono🙂
Hasa hawa akina mama ndio balaa kabisa aisee! Unamkuta mama mtu mzima anashobokea nyimbo hizi za kipuuzi na kipumbavu na anajua kuimba mashairi yake hadi unashangaa kwamba huyu mama kama yupo hivi watoto wake wana hali gani na watalelewa na nani ikiwa mama yao tu anahitaji kulelewa kimaadili.🤯🤯🤯
 
Hizo nyimbo hazina uwezo wa kuharibu jamii.

Jamii iliyoharibika ndiyo inaachia nyimbo hizo zitamalaki.

Unaliangalia hili jambo kinyumenyume.
 
Tatizo SIO wasanii tatizo ni Wanasiasa wanaojali maslahi Yao na kupuuza Kila kitu kinachoweza kikawakosesha umaarufu.

CCM ni kichaka cha Uovu wote Tanzania na Dunia Nzima.
Ili Hii nchi iwe na Jamii Bora ni Lazima CCM IFE kifo cha asili. Yaani taifa ni Lazima lizaliwe upya Kwa kuweka misingi ya maadili Kwa Taifa . Kwa Sasa Taifa halina misingi Wala dirá ya Taifa Kwa sababu ya CCM kuweka maslahi ya chama kushika hatamu bila kujali iwe ni Kwa halali au haramu.
Wasanii wengi wanaoimba nyimbo za matusi na kuashiria ngono na maneno yasiyo na staha wanatumika sana Wakati Wa kampeni za uchaguzi. Na huko wanatumika kuharibu sana maadili ya vijana na Watoto na wanawake .
Pia wasanii Hao Hao wanatumika kwenye shughuli za Mwenge n.k.

Nchi Haina maadili ya uongozi Wa umma na kuheshimu ofisi za umma . Pia Haina maadili ya kijamii kama waafrika Kwa sababu hatujakaa kama Taifa na kuweka misingi ya maadili ya Kitanzania na kuyaweka kwenye Sheria na Katiba Kama tunu ya taifa.

Watanzania tukiendelea kuwaendekeza Wanasiasa Wachache wanaonufaika na Hali iliyopo kimaadili kuanzia kwenye utumishi ,biashara na Mitaani SIO muda Mrefu taifa litaingia kwenye mmomonyoko mkubwa sana Wa maadili na kuwa na Kizazi cha hovyo.
 
Njemba kujiita Vanilla ni 2nd derivative ya ungapu.
 
Huko mbona mbali Sana mkuu... Jamii ishaisha.
 
Matope kwa bata ni starehe, kwa wengine matope ni uchafu. Haitakiwi wote tubambikiwe kwenye matope kisa kuna bata kadhaa wanaona matope ni starehe. Kama kuna ambao wanapenda huo uchafu basi iwe private, sio kenye public transport.
Mkuu umemaliza kila kitu. Hizi nyimbo za ngono kwa kweli zinatia kichefuchefu na bahati mbaya hata BASATA wanazikubali na kuzipitisha ili zije mtaani kumomonyoa maadili ya kijamii. Hii ni nchi ya kipuuzi sana.
 
Hizo nyimbo hazina uwezo wa kuharibu jamii.

Jamii iliyoharibika ndiyo inaachia nyimbo hizo zitamalaki.

Unaliangalia hili jambo kinyumenyume.
Kivipi mkuu. Hebu fafanua vizuri. Sasa unashauri nini kifanyike?
 
Umeongea vizuri sana mkuu. Ni kweli ukiangalia kwa jicho pevu utaona maadili yameanza kuporomoka kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi ya shina. Hapa ndipo tunapofeli kama taifa kwa sababu tumekosa msingi wa maadili ya kitaifa. Taifa lisilokuwa na maadili ni kama chai bila sukari.
 
Hata hizo movie ni balaa.
Nilipanda basi la BARAKA toka shamba kuja Dar iliwekwa movie moja ni aibu!
Watu wanajamiiana na watoto wamo kwenye basi wana angalia.
Hizi basi ndogo ndogo za Coaster ni shida zaidi movie haziko rated na parental guide, muziki ya singeli na bongo flava za uchiuchi tupu wanabambiana na vijora na Madera yao au na bikini.
Dkt. Gwajima D aione hii akamfikishie waziri wa uchukuzi. Sumatra wamelala fofofo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…