Ifikapo 2030 hizi nyimbo za kipuuzi za bongo flava zitaiharibu jamii nzima

Kuna siku waliweka wimbo wa Mr Mwanya, aisee ilibidi wautoe. Ulikuwa Kama pono vile. Nikajiuliza BASATA wameruhusuje kitu Kama hiki.
Hii kitu waiangalie. Kwa wastani sio afya kuwa na nyimbo kama hizo kwenye mazingira yanayokutanisha watu wa aina mbalimbali.
 

Kweli kabisa. Halafu abira ni kama wamelikubali au wanaoneana haya. Maana kwenye basi unaweza kupigiwa wimbo mpaka ukafumba macho. Bora waweke movie angalau.
 
50/50 ni usawa wa binadamu yaani kila anachofanya mwanamke na mwanaume afanye na anachofanya mwanaume na mwanamke afanye kuanzia majukumu ya nyumbani,kazi,starehe na thamani ya maisha.
Nyimbo za matusi hazihusiani na hiyo
 
Japo hatujawa na msimamo wa nini hasa ni maadili ya Kitanzania, ila tusipokuwa makini tutakuwa na kizazi cha wakaa uchi. Tutakuwa tumechelewa sana.
 
Hivi karibuni nilikuwa ndani ya basi safarini, nilijisikia vibaya sana unakuta miziki inayooneshwa ni ya hovyo kabisa, watu wanacheza kwa mrengo wa kungonoka tu na maneno yasiyo na staha yani ni kama watunzi wa hizi nyimbo wanashindana nani anajua kufanya matusi zaidi.

Kuna mama mmoja alikaa nyuma yangu alilalamika wee mpaka kachoka na humo ndani kuna watoto wadogo ambao hakuna namna utawazuia wasiangalie. Kama kuna eneo ambalo watanzania tunaharibiwa maadili basi ni kwenye miziki na programu za TV zinazorusha hii miziki.

Marekani ilianza kuporomoka kimaadili like 60 yrs ago sasa hivi wamefika pabaya sana. Na inasemwa kuwa maadili yakiporomoka, Taifa linaanguka. Hiyo ni kanuni ya kihistoria japo sijui uhusiano wake ukoje. Ziko empires zimeanguka kwa sababu ya vitu ambavyo usingedhania kama vingekuwa na impact kwenye kuangusha hizo empires.
 
Uko ni mbali sana juzi kati nimerudi hm kutoka safarini Sumbawanga namkuta mwanangu wa miaka mitatu na nusu ananiimbia hanii hanii dah iliniuma sana na nikammaindi sana mama yake
 
Hii Ina uhusiano gani n nyimbo za kipuuzi kuharibu maadili Kwa mujibu wa mleta Uzi!?
Haina uhusiano sawa lakini ukubali usikubali 50/50 imechangia 96% mmomonyoko wa maadili,gender moja inatembea uchi makusudi kwa sababu kuna mahakama,inaimba nyimbo za chumbani bila aibu kwa sababu ina pesa na elimu,hakuna tena ubinadamu ni umbuzi kwa kwenda mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…