Ifikapo 2030 hizi nyimbo za kipuuzi za bongo flava zitaiharibu jamii nzima

Kizazi kishafeli

Kizaz kishakata kamba hiki

Ova
 
Hii ni mbaya sana. Maadili ya kitaifa yakishaanguka, tutakuwa na taifa la watu wasiokuwa na mwelekeo wala kujitambua. Hapo labda ndipo serikali itaamka kutoka usingizini na kuchukua hatua ya kudhibiti upumbavu huu. Inauma sana.
 
Nyimbo za matusi nyingi wnaimba wasanii wa kiume
 
Mh Dkt. Gwajima D tafadhali tazama hili jambo kwa jicho la tatu. Mmomonyoko wa maadili unaporomoka kwa kasi ya kutisha kwa sababu ya nyimbo zinazomomonyoa maadili ya jamii. Hili suala la mabasi kucheza nyimbo za matusi bila kujali kuwa watu tunasafiri na watoto na wakwe zetu, halivumiliki hata kidogo. Tunapata kero sana kwenye mabasi ya abiria; tunaomba uzuie upigwaji wa nyimbo na video kwenye mabasi.

Kwanza, sio lazima mabasi yaoneshe video au kutazamisha/kusikilizisha abiria video/nyimbo. Elekeza mabasi yote (dalala na mabasi ya mikoani) kusitisha kero hii mara moja. Bora tusafiri kimya kimya kuliko kukerwa tangu mwanzo hadi mwisho wa safari.

Asante kwa kunielewa daktari. Nina imani hili utalifanyia kazi.
 
Hizi nyimbo na video za ngono limeishakuwa tatizo la kitaifa. Zinapigwa kila mahali na kila kona ya nchi. Hivi BASATA wanaruhusuje upumbavu huu uingie kwenye jamii?
 
mie namaindi lile goma la manungayembe la ngoni tribe kufungiwa halafu siku hizi zinaachiwa nyimbo za kishenzi tu

View: https://www.youtube.com/watch?v=0UXiqw6JaJQ
Kati ya taasisi za ovyo ambazo hazijitambui ni hawa BASATA. Sijui hata wanafanya kazi gani wakati kila mwezi wanalipwa mamilioni ya mishahara. Ni bora tu wasingekuwepo kwa kuwa hatuoni wanachokifanya hapa nchini.
mie namaindi lile goma la manungayembe la ngoni tribe kufungiwa halafu siku hizi zinaachiwa nyimbo za kishenzi tu

View: https://www.youtube.com/watch?v=0UXiqw6JaJQ
 
Mi naona ipite sheria zipigwe nyimbo za King Kiba tu mabasi yote 😎😎😎
 
Umesahau haniiii
 
Tz haina Mdhibiti wa Sanaa ya Muziki na Maigizo (Performing Art).

BASATA ya Mwl. Nyerere ilikuwa makini na weledi kusimamia utamaduni wa jamii ya Kitanzania.

BASATA ya marais Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na Samia inajuwa mlungula tu ili sanaa ya mtu ipate ithibati kuingia sokoni.

Miziki na maigizo inazuka tu na Media na COSOTA nazo pia zimenasa kwy mtego wa Wasanii.

Mzungu akiweka kizuizi cha rika kwy kazi za sanaa basi kinaheshimiwa na kila mtu na kila taasisi japokuwa wana mambo yao mengine ya hovyo sana.

Nadhani warasimu hawahangaiki kwa sababu wao vizazi vyao haviburudishwi na sanaa hizi za ki-local (siyo walaji wa kazi za sanaa hizi za ki-local).

Kule Msasani Peninsula, Njiro, Pasiansi, Mji wa serikali, Shanty Town kwenye ma-Bangalore hakuna Mondi wala Konde Boy, TMK wala Zuchu, badala yao kuna akina Katy Perry, Michael Jackson, Miley Cyrus, Britney Spears, Elton John, George Michael, Ed Sheeran, David Austin, Cliff Richard nk.

Bila kutafuna maneno BASATA, COSOTA, MEDIA zote kasoro TBC ni saratani ya utamaduni wa taifa.

Zimetumwa kulinda siasa na wanasiasa, ndiyo maana ukitungwa muziki unaokosoa wanasiasa utasikia tayari Msanii yuko kwenye mikono ya dola au katekwa na watu wasiojulikana.

Mtoto wa mwanasiasa mmoja kiongozi (ambaye mtoto wake huyu alikuwa kambi ya upinzani) aliwahi kumuhoji babake kwanini mkiimbwa kwa kukosolewa mnamkamata Msanii lakini wakikosolewa kwa sanaa wapinzani na raia wa kawaida mnakaa kimya?

Alimjibu kitanda usichokilalia huwezijuwa Kunguni wake, ukitaka kujuwa sababu hama upinzani uje CCM.
 
Mkuu nimekuelewa vema. Kumbe kwa hali hii sasa serikali ya CCM ndio waharibifu wa maadili ya jamii simply because their dynasty is not affected. Hii nchi ngumu sana.
 
Hizi nyimbo na video za ngono limeishakuwa tatizo la kitaifa. Zinapigwa kila mahali na kila kona ya nchi. Hivi BASATA wanaruhusuje upumbavu huu uingie kwenye jamii?
"MWAGIA NDANI CHAKULA CHA WATOTO," "HANIIIIIIIII,"
 
Enzi za Mwalimu ukipiga nyimbo za chakakacha polisi wanakuja kukukamata na zilikuwa na mafumbo mtoto ngumu kuelewa, ila sasa matusi wazi wazi hadi ktk redio zinapigwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…