Ifike mahali Watanzania tuache kukubali hadaa na uzushi unaotolewa na akina Evarist Chahali na Kigogo

Mkuu ulitaka Generali wa Jeshi la JMT..Aende kinyume na Rais wa JMT ili kitokee nini?

Ulitaka atamka Tarehe tofauti na iliyokubalika na Serkali ili watanzania Wakose imani na Serkali? Halafu kitokee kitu gani?

Kuna Vitu huwa viko Ndani ya Kiapo mpaka unakufa na kama ni Dhambi bhasi utakufanya nayo Ilu kulinda Maslahi ya Serkali iliyopo madarakani
Halafu bado mleta mada anataka tumuone ana akili Sana. Huko serikarini si ndo kuna mkubwa aliyesema Magufuli ni Mzima wa Afya yuko ofisini?
 
Kinachofanya watu wazushe ni serikali kuficha taarifa... Mfano wakati rais anaumwa unasema rais anaumwa tunaomba privacy...

Sasa kusema rais anapiga kazi na haonekani sio sawa.

Equally saga ya VP Mpango eti kapotea mwezi haonekani ni mwendelezo wa kuficha taarifa
 
namuamini Mabeyo ni mtumishi na hana makando kando.
Kwahiyo na sisi sote tumuamini! Huyo ni sehemu ya utawala ni lazima aende sambamba na utawala.
Mimi sjaelewa na sitaelewa kwanini hali ya rais ilipokuwa tete viongozi wakuu hawakuwepo hospitalini! Rais alikuwa Tanga huku waziri mkuu alikuwa Tunduma msikitini akitoa taarifa kuwa yuko ofisini anachapa kazi!
 
Tumemsikia Mkuu wa Majeshi Mstaafu Generali Mabeyo akisimulia hivi karibuni jinsi Magufuli alivyouguzwa hadi kufariki.

Katika maelezo yake, Generali anadhihirisha kuwa Magufuli alifariki tarehe na muda uliotajwa na Mhe. Samia alipokuwa akitangaza kifo hicho.

Lakini akina Evaristi Chahali na Kigogo wakajifanya wana taarifa za ndani na nyeti na kutangaza kuwa kifo hicho kilitokea kabla.

Mbaya zaidi Chahali akadai kuwa Zitto Kabwe alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha Mhe. Samia kuapishwa kuwa Rais akidai kuwa kuna baadhi ya viongozi walitaka asiapishwe.

Lakini Generali anaonesha kuwa hakukuwa na changamoto ya namna hiyo. Hata kama ingekuwepo wasingemtafuta Zitto atoe ushauri.
Una umri Gani?
 
mkuu endelea kuwaamini kina Chaali na Kigogo.
 
Mkuu unaufahamu Gani kuhusu Clafsied Information na declassfief imformation na Time classfied information?

Unafahamu kila Intel ya Kiserkali ina Expire date?
Unafahamu leo hii Usingejua kuhusu baadhi ya Siri endapo zingekuwa hazina expire date?
Shida Inakuja Japo zina Expire date ila Kuna mipaka zipi ziende Public zipi zibaki private..
Nadhani classified information hudumu kuanzia miaka 10 na baadhi miaka 30 ndipo zinaweza kuwa- disclassfied.
 
hata hivyo
uposhwaji, uzushi, habari, stori na simulizi kama hizo za hawo wazushi ulowataja,
zinaaminika, zinapendwa na kukubalika sana chadema, kwasababu hawana wanachoweza kufanya ispokua kubabaika na uzishi....
na huwa wanajadili uzushi kama huo hadi kamati kuu...
Zamani niko mtoto kama wewe nilidhani viongozi wa dini hawawezi kusema uongo, kumbe dah!! uongo inabidi usemwe ili waishi.
 
Tumemsikia Mkuu wa Majeshi Mstaafu Generali Mabeyo akisimulia hivi karibuni jinsi Magufuli alivyouguzwa hadi kufariki.

Katika maelezo yake, Generali anadhihirisha kuwa Magufuli alifariki tarehe na muda uliotajwa na Mhe. Samia alipokuwa akitangaza kifo hicho.

Lakini akina Evaristi Chahali na Kigogo wakajifanya wana taarifa za ndani na nyeti na kutangaza kuwa kifo hicho kilitokea kabla.

Mbaya zaidi Chahali akadai kuwa Zitto Kabwe alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha Mhe. Samia kuapishwa kuwa Rais akidai kuwa kuna baadhi ya viongozi walitaka asiapishwe.

Lakini Generali anaonesha kuwa hakukuwa na changamoto ya namna hiyo. Hata kama ingekuwepo wasingemtafuta Zitto atoe ushauri.
Kwa kuwa kasema unaamini kuwa kila alichosema ni kweli. Kuna mengine hajayasema.

Mpaka sasa haiingii akilini kwa mkewe kutokuwepo hospital siku nzima.
 
Kwani alikuwa hawezi kuzungumza? mbona alikuwa akizungumza mpaka siku ya mwisho? ka anazungumza alishindwa nini kuongea na simu na waziri mkuu na kumpa maelekezo? kumbuka afya ya Rais ni swala la ulinzi na usalama na hakuna viongozi waloruhusiwa kumuona isipokuwa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Kwa hiyo hata mkewe hakuwa wanaruhusiwa kumuona!?
 
Kigogo na Chahali waliona mapema hicho kifo na kutoa taarifa

Mabeyo hata body language yake inamshtaki kana kweli Mwendazake alikufa siku hiyo
 
Tumemsikia Mkuu wa Majeshi Mstaafu Generali Mabeyo akisimulia hivi karibuni jinsi Magufuli alivyouguzwa hadi kufariki.

Katika maelezo yake, Generali anadhihirisha kuwa Magufuli alifariki tarehe na muda uliotajwa na Mhe. Samia alipokuwa akitangaza kifo hicho.

Lakini akina Evaristi Chahali na Kigogo wakajifanya wana taarifa za ndani na nyeti na kutangaza kuwa kifo hicho kilitokea kabla.

Mbaya zaidi Chahali akadai kuwa Zitto Kabwe alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha Mhe. Samia kuapishwa kuwa Rais akidai kuwa kuna baadhi ya viongozi walitaka asiapishwe.

Lakini Generali anaonesha kuwa hakukuwa na changamoto ya namna hiyo. Hata kama ingekuwepo wasingemtafuta Zitto atoe ushauri.
Wakati mwingine ni heri kukaa kimya kuficha ujinga. Kama una akili timamu na kama umemuelewa mabeyo ni dhahiri kuwa kuna kundi la watu walikuwa hawataki mama achukue kijiti na anasema ndio maana walichelewa kwa siku mbili kumuapisha. Hata kina kigogo walisema hivyo hivyo kama mabeyo alivyosema. Tatizo lako unaendeshwa kwa mihemko
 
U mean kuna baadhi zinaweza Expire ila kwa kikomo fulani so kila mtu ataona hizo taarifa ama kuzisikia
Yeah..
Ulisikia mwaka 2035 mpaka 2050 walisoma Baadhi ya Siri za Tanganyika kipindi cha nyerere zitakuwa eXpired na zitakuwa Disclassfied?
Ipo.siku Siri zitavuja mkuu
 
Dunia ipo ili izunguke na watu tuishi. Jamii haijawahi kuishiwa watu wa kaliba hio hatuwezi fanana wote si lazima wote tufanane na pia hawadhuru.
 
Tumemsikia Mkuu wa Majeshi Mstaafu Generali Mabeyo akisimulia hivi karibuni jinsi Magufuli alivyouguzwa hadi kufariki.

Katika maelezo yake, Generali anadhihirisha kuwa Magufuli alifariki tarehe na muda uliotajwa na Mhe. Samia alipokuwa akitangaza kifo hicho.

Lakini akina Evaristi Chahali na Kigogo wakajifanya wana taarifa za ndani na nyeti na kutangaza kuwa kifo hicho kilitokea kabla.

Mbaya zaidi Chahali akadai kuwa Zitto Kabwe alihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha Mhe. Samia kuapishwa kuwa Rais akidai kuwa kuna baadhi ya viongozi walitaka asiapishwe.

Lakini Generali anaonesha kuwa hakukuwa na changamoto ya namna hiyo. Hata kama ingekuwepo wasingemtafuta Zitto atoe ushauri.
WaTanzania tuamke.
Haya mambo ya kuwaongelea waliotangulia na wenye makelele! Yanasaidiaje kupatikana kwa ubora wa maisha ya waTanzania Hali ngumu maji, umeme, barabara, Huduma afya, shule nk.

Hizo stories za Mkuu Nani Sasa asiyeelewa alienda? Tusirejeshane kweusi, hata Mkapa alienda jameni.
Nasi tutaenda siku ikija.

Mfungo mwema.
 
Amesema kifo kilitokea saa 12 jioni wakaanza kujadili namna ya kumtaarifu Samia,Mke na Mama wa JPM.Wakawaita Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi kwa kuwa walikuwa Dar.Wakahakikisha Mama wa JPM aliyekuwa Chato amepelekewa taarifa na mtu aliyetumwa kwa ndege.Na amesema ndiyo maana tangazo lilitolewa saa Tano usiku kwa sababu ya taarifa hizo zilitakiwa kuwafikia hao watu muhimu.
Maana ya maelezo hayo ni kwamba hiyo tarehe ni Machi 17.
Mama yake magufuli alipata stroke kumbukumbu zikapotea zote hata magufuli anafariki alikua hajapona bado
 
Back
Top Bottom