"IGA ya DPW imetusaidia sana kujitambua. Tuna wanasheria wa Aina Gani!, Bunge na Serikali yetu, Ilipitishaje IGA Hii?

Kuna viashiria vingi hili jambo la DP WORLD haliko sawa. Serikali inatumia nguvu kubwa sana ktk kulifanikisha hili jambo kwanini? Kama ni jambo jema na lipo sawa sidhani kama kungeitajika nguvu kubwa sana ktk kulifanikisha.

Fikilia pale Mbowe aliposema atahutubia taifa kuhusu msimamo wa chama ktk hili saata mambo yaliyoibuka gafla. Eti mkutano wa wahariri wa habari eti mara rais anahutubia sijui nini na nasikia hata ile tarehe iliyopangwa na wakina Dk. Slaa kufanya mkutano mkubwa wa kuhusu hili suala, eti yanga Fc nayo ndio wametangaza kufanya siku ya wananchi
 

Well said, ndy uhalisia.
Mwanabodi kaweka record yk safi ktk Uzalendo.
 
Kwa bandiko hili ndugu Pascal Mayalla umeona mwenyewe kwamba jamii inakupenda ukiungana na matarajio yao. Ndio hivyohivyo siku ukikatika kidole ukaomba msaada jamii itahamasika kukuunga mkono lakini yawezekana serikali unayoitetea isikuunge mkono kurudishia kidole chako. Hata unapotembea mtaani ukiwa mtu wa jamii unalindwa na jamii yenyewe kuliko unapokuwa upande unaoinyanyasa jamii. Bandiko limeshiba na ningekuwa wewe ningeendelea kukuza mtaji wa kuungwa mkono na jamii.
 
Tumehakikishiwa kuwa watazaliwa watoto wazuri sana watatu mapacha! Majina ya watoto hao yatakuwa Ms Hga, Ms Concession na Ms Leasing. Watoto hawa watakuwa wa siri (hatutawaona) ili kulinda heshima ya utu wao. Ila wajukuu tutawaona na watakuwa na majina yanayoishia na Ms Performance, Ms Efficiency na Ms Win-Win! Tusiwe na wasi wasi na neema hiyo iliyotokana na tukio hilo la IGA.
 
Mtu aliyesoma anielekeze jamaa anapinga au ana support, maana vichwa vya habari vya Paschal havijawahi eleweka.
Hapo mwamba kapinga fln hivi kimafumbo. Lkn kwa kuwa wengi wanasema kasema ukweli maana yake yupo timamu Leo kasema ukweli ulio sahihi. Mimi ni shabiki mkubwa na makala za mkubwa wangu Paskal tangu nijiunge humu miaka ya nyuma Sana.

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Binafsi kanichanganya Tundu Lissu kwamba
1. Ukiunga mkono maamuzi ya Bunge maana yake wewe umelamba asali, au
2. Huna akili kabisa.

Kwake yeye wasiolamba asali na wenye akili lazima waupinge ule mkataba. Hapo ndipo natingwa.
Ila naungana na wale wanaotaka maboresho ya Mkataba. Mama kasema wakusanywe wapingaji wenye Nia njema ili wasaidie kuboresha mkataba endapo kama tuna hiyo nafasi. Binafsi nitafaidika na dipiwedi pale nitakapoagiza gari kwani Hadi sasa nimewahi agizia flash Tu kupitia kikuu na sijui kama ilipitia bandarini au Mwl nyerere Int airport

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 


Sawa, ngoja nikasome, na kama anastahili kupongezwa, nimpongeze.
 
Profesa Shivji kukosolewa sio tatizo kaka Paschal, watu wamewakosoa kina Kwame Nkrumah na Julius Nyerere enzi zile wakiwa hai itakuwa Profesa mwalimu wa chuo kikuu hapo Mlimani.

Shivji alitoa maoni akidhani kuwa tunakwenda kuingia mkataba na DPW kwa kutegemea IGA iliyopelekwa bungeni akasahau kuwa huu mfumo wa IGA ni wa kisasa zaidi, wa miaka ya karibuni.

Aliongelea BIT badala ya kuongelea IGA. Alichukua hoja zile zile za BIT katika kuikosoa IGA iliyokwenda bungeni, hilo ni kosa lake na ni la kibinadamu lenye kuweza kufanywa na mwanazuoni yoyote yule.

Aliongea kama vile kinachokwenda kufanyika ni Bilateral Trade yaani biashara ya ubia wa nchi mbili wakati ni uwekezaji wa DP hapa Tanzania uliopita bungeni ili kuwapa wawekezaji wazalendo nguvu ya kisheria kwenye masuala mbalimbali yatakayoibuka mbeleni.

Afadhali hata ya Shivji aliyejikita kwenye mkataba licha ya makosa ya kiufundi aliyofanya, huyo Nshala hakuna la maana aliloliongea zaidi ya kutaka kuwatisha wanasheria wasomi wa serikali na akamtukana Rais na kumdharau Spika.

Huyo Msomi Nshala, kaongea pumba tupu na anayo bahati amekutana awamu hii ya sita ni ya kiungwana vinginevyo angekutana na awamu ya tano muda huu angeshapotezwa siku nyingi.
 
Hao wote uliowataja wametumiwa na wapigaji wa bandarini kuongea mbele ya watu ili watakaowapinga waonekane ni maadui za watu hata kama baadhi yao waliongea pumba mbele ya kamera za waandishi wa habari.

Ni vita ya kiuchumi na nzito ndio maana wazee wa nchi wakatumiwa maana yake wamelipwa pesa nyingi sana ambazo ni sehemu ndogo sana ya hicho wanachoingiza kila siku pale bandarini.

Wanasheria wa serikali wamejibu hoja zao zote kisheria bila ya kutukana mtu.
 
Kaka umekuwa very objective kwenye suala hili.Kuna kitu kiko ndani yako kama utathubutu kidogo tu kuwa kwakusudi la Mungu kuna namna alikuumba wa aina fulani utakuwa mtu wa heri na heshima sana kwa miaka atakayokupa Mungu zaidi hapa duniani.
Kumbuka tunakuja duniani kwa kusudi,kama tulivyozaliwa mara moja na kufa ni mara moja.
Heri kuishi maisha mafupi ya faida kuliko maisha marefu ya hasara.
Jipe muda sikiliza sauti ya upole ndani yako then jiulize muitikio wangu kwenye maisha haya na ninavyotenda ni kwa faida?
Siku zote be you,be yourself dhamiri yako isipokushitaki una ujasiri mwingi hata mbele za Muumba.
Mahali pa kusaidia,saidia ndugu Watanzania wenzako kwa kipawa Mungu alichoweka ndani yako pasi na hofu na unafiki.
Usimuogope awezae kuua mwili asiweze kuua roho kwani wote tutawajibika kwa Mungu.
Mungu akutunze na kukusemesha ujue njia ya kuiendea siku zote sio kwa faida yako wala watu fulani lakini kwaajili ya kusudi la kuwepo kwako hapa Duniani specific hapa Tanzania.
 
Karibu tunavuka mto pamoja Mkuu
Cannan si mbali tutauona mji ule!
 
We ndio kilaza wa ajabu, halafu mnaona sheria sijui ni rocket science. Sheria inasomwa na watu wenye uwezo mdogo ndio maana ndio fani iliyojaa warembo. Angalieni wenzenu wenye akili, Human doctors, Engineers, Pharmacists, Accountants, Economists, Computer Scientists and Engineers na wengineo wako kimya wanapiga kazi ya kuendesha nchi, ninyi wambea mnaojiita wanasheria kozi ya warembo kazi yenu ni kupotosha wananchi, kuzushi mauwongo huku mkijaa arogance za kipuuzi, ni kawaida ya watu wenye IQ ndogo kwanza kuwa na pomposity, arrogance na mambo ya kijinga km hayo. Hakuna la maana mnasaidia nchi hii ktkt uzalishaji. Kazi yenu ni kuhakikisha migogoro na kesi inazalishwa ili mdhulumu binadamu wenzenu. Baba wa Taifa hakukosea kusema nyie ni watu wabaya na hatari ktkt ustawi wa nchi. Ni fani naidharau sana haina msaada ktkt ustawi wa binadamu zaidi ya kuzalisha migogoro na kuzusha taharuki na uwongo kwa maslahi yenu mnaojiita wanasheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…