IGP mtimue au mfute kazi RPC wa Dodoma ikikupendeza

Kabla hamja mchukulia kahaba hatua jiulizeni kwanini anajiuza na mmefanya jitihada gani kumsaidia ili aweze kuacha
 
Kabla hamja mchukulia kahaba hatua jiulizeni kwanini anajiuza mmefanya jitihada gani kumsaidia ili aweze kuacha
 
Rais ni Mwanamke na RPC ni Mwanamke na aliyefanyiwa ukatili ni Mwanamke!!!
Kumbe ni kweli wanawake hawapendani
 
Kumbuka Rais wa nchi pia ni mwanamke na Toka hili tukio litokee hajawahi kutoa neno unapata picha Gani?
 
 
Uelewa wako mdogo pole kijana, issue ya ukahaba inaingiaje hapo? Huoni kwamba wanatengeneza mazingira ya kumnusuru afande aliyeagiza hicho kitendo kifanyike? Na kwa kusema kwamba alikuwa kahaba kitu ambacho hakihusiani na dhana nzima ya tukio huoni kwamba ni kumdhalilisha binti? Mm ningekuwa mwanafamilia wa huyo binti huyu Rpc ningempeleka mahakamani athibitishhe huo ukahaba.
 
Aisee.....si mchezo
Kwa hiyo mvuta bangi akibaka na kufira mtu ni sawa?..
Kwa maana hiyo mtu akiwa kahaba kama kweli ni kahaba kufanywa vile ni haki yake au sio..?..
Hivi huyu jamaa anajua impact ya kauli hizi kwa huyu dada na familia yake na Taifa kwa ujumla?...
Level ya RPC.....
 
Wasifu wa hao vijana wameutaja wamesema sio maaskari bali ni wavuta bangi
 
Kati ya hao walifanya huo uchunguzi na yeye ni mmoja wa viongozi ktk hiyo timu bado huoni kosa lake?

Kwa suala kama ilo lilivyotrand na kuchafua taasisi nzima ya jeshi la polisi unazan uyo mama atakua na maamuzi ya kupinga mbele ya boss zake?
 
Daah!😔 kuna yule jamaa huwa akiandika kuwa "KUZALIWA AFRICA NI LAANA", kama pepo ipo kweli basi sisi inabidi tuzame bila pingamizi.

Kwanza unawezaje kuthibitisha kwamba mtu ni kahaba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…