Uchaguzi 2020 IGP Simon Sirro akutana na Wadau wa Uchaguzi 2020, aitaja JamiiForums na Mitandao mingine kama changamoto ya Uhalifu wa Kimtandao sababu ya Teknolojia

Uchaguzi 2020 IGP Simon Sirro akutana na Wadau wa Uchaguzi 2020, aitaja JamiiForums na Mitandao mingine kama changamoto ya Uhalifu wa Kimtandao sababu ya Teknolojia

Ni kazi bure kuhubiri utulivu na amani, kabla ya kuhubiri haki na usawa.

Kama democracy zimetushinda na hatupo tayari kusikiliza wasiokubaliana na sisi, tubadili katiba twende kikorea Korea.

Maana kelele zinapigwa kwa kuwa wapiga kelele wanasema ni haki yao kikatiba kupiga kelele, na hata wakienda mahakamani, wanashinda kesi,

Sasa tubadili katiba ili wasiwe na cha kusingizia bali kukaa kimya na kukubaliana na fikra za bwana mkubwa.
..Kwa kweli kama IGP anataka kutenda HAKI basi aitishe kikao na viongozi wa UPINZANI.

..Pia ninamshauri awe HONEST, and FAIR, awaeleze wapinzani makosa yao, na akubali kusikiliza madukuduku yao.

..Huenda wanaotoa kauli kali wana machungu yao ambayo wanaona hayajashughulikiwa.

..Huu utaratibu wa kukusanya viongozi wa dini ambao ni Pro-CCM na Pro-serikali halafu kuwaelekeza wajibu hoja za wapinzani siyo suluhisho la tatizo lililopo.

..Pia namshauri kuanzia sasa aongeze msisitizo ktk suala la HAKI.
 
..huyu Afande kuna HILA anazifanya dhidi ya CDM.

..matamshi yake yanaonyesha ana CHUKI / KISASI dhidi ya CDM.

..CDM wanapaswa kuwa makini sana na michezo michafu inayopangwa dhidi yao.

NB:

..IGP siyo mtoto wa sekondari asiyejua nini cha kipi kinafaa, na kipi hakifai, kuwa ktk presentation sensitive kama ile.

Hapo hasa ni kuwa makini na ulinzi wataopewa
 
Jamiiforums ni shule tosha kwa kutoa elimu endelevu kwa majadiliano ya kina na mabandiko ya kuelimisha kuliko chombo chochote cha media nchini Tanzania.

Hivyo nyote mnakaribishwa msitishwe kuja kujiunga au kusoma mradi tu kuhakikisha vigezo, masharti , kanuni na sheria za Jamiiforums zizingatiwe ili tuendelee kuwa chanzo cha kuaminika kwa majadiliano mazito na kujifunza.
 
Kitakuwaje chanzo cha kuaminika wakati kimeegemea upande moja wa wale ambao mirija yao imekatwa. JF ile unayoikumbuka wewe ilikufa sasa unaongea kwa sababu ya mirija ambayo wewe unaifahamu imekatwa? Nyinyi mna-chuki binafsi tu ndio inawasumbua. Tanzania ni ya kila mtu tatizo lenu mpo minority mnataka msikilizwe nyie tu, hiyo haiwezekani.
 
Back
Top Bottom