IGP alieleza wazi tangu mwanzo kuwa Mbowe si malaika na kwamba ushahidi upo wa kutosha juu ya ushiriki wake kwenye ugaidi.
Tunayoyaona na kusikia mahakamani yanathibitisha ukweli kuwa kila binadamu ana siri kubwa moyoni mwake. Kamwe usisema fulani siyo au fulani hawezi kufanya hili wala lile. Yaliyo moyoni mwake ni giza tororo na ni siri yake.
Ushahidi unaotolewa kila kukicha kuthibitisha jinsi Mbowe alivyoshiriki kwenye njama za kufanya ugaidi zinatuacha midomo wazi. Ni aibu kwa waliofikiri Mbowe ni malaika. Muhimu ni kuiacha mchakato wa mahakama uendelee hadi mwisho na mbivu zitajulikana. Kwa ushahidi tunaoona, hatutashangaa tukisikia mtu anakula miaka 30 jela.