RC na DC wanamamlaka ta kuliamuru Jeshi la Polisi kamata fulani weka ndani na sio Waziri. Waziri pekee mwenye mamlaka hiyo ni Waziri wa mambo ya Ndani.
Polisi ni chombo cha dola kilichopo chini ya kundi la majeshi, kinaendeshwa kwa amri kutoka juu. Kitaifa amri ni inatoka kwa rais, ambaye ni CinC na kumuagiza IGP. Mwanasiasa pekee anayeweza kutoa amri ya kitaifa kwa IGP, Jeshi la Polisi likamate yoyote ni Waziri wa Mambo ya Ndani. Wakuu wa mikoa ni wawakilishi wa rais kwenye mikoa husika, na ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi za mikoa hivyo nao wana deraitive powers za kutoa amri kwa Polisi wa mkoa husika kumkamata yoyote. Ma DC nao ni kama ma RC, kwa wilaya zao. Viongozi wengine wote wa serikali, hawana mamlaka ya kidola kuamrisha Jeshi la Polisi kumkamata yoyote, bali wana uwezo wa kuripoti jinai yoyote na Jeshi la Polisi linawajibika kufanya uchunguzi wa kijinai, kutegemeana na jinai husika, uamuzi wa kukamata na kuseka ndani ni uamuzi wa kipolisi na sio amri ya Waziri. Alichofanya Waziri Gwajima ni kuripoti tuu kisiasa in public kuliagiza Jeshi la Polisi kumchunguza Askofu Gwajima. Tangazo lile linatakiwa kufuatiwa na barua rasmi kutoka Wizara ya Afya kwenda kwa IGP yenye tuhuma specific na Jeshi la Polisi ndio litaamua kama tuhuma hizo zinamstahili mtuhumiwa kukamatwa au la. Kinga ya mbunge kusema chochote bila kukamatwa ni kauli za wabunge ndani ya Bunge. Mbunge akifanya jinai yoyote nje ya Bunge anakamatwa tuu kama mhalifu mwingine yoyote!. Ila kama uhalifu huo umefanyika kipindi cha vikao vya Bunge vinaendelea na mbunge huyo yuko Bungeni kuhudhuria vikao na anatakiwa kukamatiwa Bungeni, then Spika lazima aarifiwe ndio atoe idhini kwa Jeshi la Polisi kumkamata mbunge akiwa viwanja vya Bunge . Kwa vile mbunge ni mtumishi wa Bunge, akifanya jinai yoyote popote, mwajiri wake pia anaarifiwa. Hivyo kwa vile sasa Bunge liko kwenye vikao vya kamati, kama ni kweli serikali imedhamiria kumshughulia Askofu Gwajima na sio utani wa mtu na shemeji yake, then kauli ile ya kisiasa ya Waziri wa Afya itafuatiwa na barua rasmi ya Wizara ya Afya kwa Jeshi la Polisi yenye tuhuma rasmi itatua mezani kwa IGP cc. Spika wa Bunge, na ndipo Polisi waifanyie kazi. Waziri wa Afya au Waziri mwingine yoyote nje ya Waziri wa mambo ya Ndani, hawezi kutoa amri kwa Jeshi la Polisi kumkamata yoyote.
P