IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

Hayo maneno si kitu kabisa unapolinganisha na kosa kubwa alofanya Msomali la kuua watu wasio na hatia!

Uhai wa binadamu unathamani kubwa sana isiyo mithiri.

Uhai wa mwanadamu ukishapotea hauwezi kupatikana popote Duniani hata kwa kuuzwa !

Acheni chuki jamani !
Natamani nione comment yako iliyowahi kutetea uhai wa maelfu ya watu waliouwawa na polisi wetu, watu wasio na hatia. Mfano tu wale wa zanzibar mwaka jana.

Au hao polisi waliouwawa na Hamza wana damu ya juice ya zabibu? Uache double standards!
 
Hahaha ni kweli wewe unawafahamu ila umechanganya madesa kidogo.

Mimi wengi wao nimekua nao toka watoto wa Mahita nawajua vizuri sana

Ndomaana nimesikitika sana kauli ya huyu mkuu wakati kwake nako kuna shida na tunajua
😄😄 Sawa mkuu, msalimie saitoti.
 
Natamani nione comment yako iliyowahi kutetea uhai wa maelfu ya watu waliouwawa na polisi wetu, watu wasio na hatia. Mfano tu wale wa zanzibar mwaka jana.

Au hao polisi waliouwawa na Hamza wana damu ya juice ya zabibu? Uache double standards!
Kwamba yao Ni zabibu?😁😁😁😁😁
 
Katika kikundi cha wazazi sita, wanne wameshaijadili hii kauli ya Sirro, na ni ukweli kuwa wengi hawajaipenda na imewasikitisha.

Isipokuwa kwa akina Mr and mrs privilege's kama Akilinjema na mama D ndio waliomuunga mkono afande Sirro.
Hii kauli hadi maofisa wa polisi wameshtushwa kuisikia
 
IGP Sirro jana umetoa kauli nzito na ngumu mno kutolewa na kiongozi wa aina yako na mtu mwenye umri mkubwa kama wewe na mtu anayeheshimika kwa cheo chake kama wewe.

Angalia sana ulimi wako jinsi unenavyo, muombe sana Mungu akupe hekima ili kabla ya kutamka neno lolote hekima ikutangulie.

Jana ulitamka maneno haya nami nakunukuu.

"Watanzania kuweni makini msije mkazaa mtoto wa hovyo hovyo kama Hamza aliyetuletea majanga Watanzania, wazazi wa Hamza mnajisikiaje kuzaa mtoto kama huyo? Na nyie ndugu zake mnajisikiaje kuwa na ndugu kama Hamza?". Mwisho wa kunukuu.

IGP Sirro, hakuna mzazi anayepanga azae mtoto wa aina gani, Binadamu tunazaa mwili hatuzai Roho.

Kuna kijana anasumbua sana mitaani, anajitapa kwamba hakuna wa kumfanya lolote kwa sababu Baba yake ana cheo kikubwa mno serikarini, kijana huyo huvuta unga na kwenda hadi kwenye Hotel ya Baba yake iliyoko Chanika ambako hufanya vituko vya ajabu, ukiwemo kupiga watu.

Je, unajua huyo mtoto ni wa nani? Tafadhali sana, wazazi wa Hamza hawakujua kama wanazaa mtoto wa aina gani, hata wazazi wako wewe Sirro hawakujua kama ipo siku utakuja kuwa IGP.

JITOKEZE UIOMBE MSAMAHA FAMILIA YA HAMZA ILI ULINDE HESHIMA YAKO.
 
Iliyoko Pasiansi? Kumbe ni hotel ya Sirro? Basi kuna ufisadi mahali, huwezi kujenga kwa mshahara wa u IGP!
Nan anaishia kwa mshahara cku hizi, upo nyuma sana mzee. Mtu mwenye ng'ombe Mia tu anaweza kufanya maajabu ndan ya muda mfupi na usiamini macho yako
 
Natamani nione comment yako iliyowahi kutetea uhai wa maelfu ya watu waliouwawa na polisi wetu, watu wasio na hatia. Mfano tu wale wa zanzibar mwaka jana.

Au hao polisi waliouwawa na Hamza wana damu ya juice ya zabibu? Uache double standards!


Mimi Imani yangu inakataza kulipa kisasi !

Tunatakiwa kumuachia Mwenyezi Mungu yeye ndiye anayejua jinsi ya kuwalipa uovu wao.

Allah Wakil.
 
Back
Top Bottom