IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

Binafsi niliona hakuna mtu aliyekuaga anaongea kwa kibri au majivuno kama yule aliyesema aitewe General leeee
 
Sio hajaja mjini akiwa mlinzi kulinda bank n wakubwa zake,lenana imejengwa miaka ya tisini...siro akiwa hana cheo
Kamanda Sirro huyu huyu aliyesoma Tosamaganga. Sina hakika sana kama lenana ni ya kwake ila mzee kajitahidi kuwekeza sana katika lodges na bar na aliona mbali kufungua kiwanda cha kuzalisha unga kinachoitwa musoma food ambacho kipo shinyanga.

ila kwa watoto tu, mzee kazaa watoto wake ni watukutu walevi na wanapenda sifa mno kwa cheo cha baba yao.
 
Katika kikundi cha wazazi sita, wanne wameshaijadili hii kauli ya Sirro, na ni ukweli kuwa wengi hawajaipenda na imewasikitisha.

Isipokuwa kwa akina Mr and mrs privilege's kama Akilinjema na mama D ndio waliomuunga mkono afande Sirro.
Huyo mama uliemtaja nahisi dish limeyumba,huku lumumba wamemkopa sana utamu...yani ni kusifu tu hata kama jambo la hovyo
 
Huyo mama uliemtaja nahisi dish limeyumba,huku lumumba wamemkopa sana utamu...yani ni kusifu tu hata kama jambo la hovyo
Anaonekana ni mama asiye na majukumu, kazi yake kubwa itakuwa ni kuwahudumia wakubwa wa CCM chai na karanga asubuhi…
 
Siro ukimwangalia mwonekano wake kimwili utadhani ni mtu wa kuheshimika sana!

Hapana, kuna wakati hata matamshi yake yalionekana kuwa ya mtu mwenye busara.

Haieleweki ni kitu gani hasa kimembadilisha akili kiasi hiki alivyokuwa sasa?

Unajua, inasemekana damu za binaadam zikimwagwa kwa uonevu tu, hazimwachi mtu anayesababisha zimwagike, ni lazima atadhurika tu kwa njia moja au nyingine.

Siro ni mhanga wa umwagaji wa damu za waTanzania ambao hawakustahili kuuliwa au kuumizwa.

Maisha yake ya uhai wake uliosalia yatakuwa ya matatizo tupu.
Mimi nafikiri kateleza tu kibinadamu baada ya kuwapoteza vijana wake wawili,tumsamehe Sirro hajakamilika kama ambavyo sisi sote hatujakamilika,hata polisi wasiotenda haki wanaodhulmu watu ni wa hovyohovyo Kama Hamza tu,nadhani angesema hivyo angekuwa amebalance
 
ccm mmeanza kumalizana wenyewe, hamza mwanaccm amewamaliza ccmpolice na wao wakammaliza, hivi ccm mnanini lakini?

Muulize mgombea wenu wa urais 2015 atakuambia ccm wana nini😂😂😂
 
Back
Top Bottom