IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

Hakuna mwanadamu apangaye nani azaliwe duniani isipokuwa Mola pekee.

Suala la mtu kuwa wa namna fulani ni choice zake mwenyewe kutokana na jinsi anavyoyachukulia maisha na matukio yake.

Huwezi kuwasononesha ndugu na wazazi wa Hamza kwa jambo lile.Wao inawahusu nini?

Yeye polisi badala ya kufanya uchunguzi kwa weledi wake akatuletea sababu yenye mashiko kulikuwa na nini kati ya vijana wale wa kitanzania hadi wakapigana risasi,anaanza kuleta shombo za ajabu ajabu.

Sina kawaida ya kuwasema viongozi lakini huyu mzee ameniboa sana.Wamtoe pale,hafai kuongoza jeshi letu tena.

Hivi mzee Sirro na wale wanaozaa taahira nao unataka tuwalaumu wazazi wao kwa kuzaa vilema wasiochangia chochote kwenye nguvu kazi ya taifa?

tutafika kweli tukiwa na falsafa za aina hii?unaelewa upana wa kauli yako mzee wangu?!inasikitisha sana!
Mpaka hapo tusitegemee majibu chanya hata kama kutakuwa na uchunguzi. Kilangila.
 
Mtoa uzi, shikamoo....!!!!. Inawezekana nakuzidi umri,lkn nimekupa salamu hii km ishara ya kuheshimu busara zako zilizoonekana ktk uzi huu, Kweli pale hatuna IGP, nashangaa Kwanini amekuwa na mihemko kiasi kile, nadhani angejikita kujua Kwanini mtu ambaye Chama tawala kilimwani hata kuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Ilala,Dola yenyewe ilimwamini ndio maana alimiliki silaha kisheria,Haya hata ktk kuua,aliua Askari tu,na si raia, Kwanini??.Sirro km mtu mzima ilipaswa atafakari hayo na si kuwalaumu Wazazi wake Hamza na kuwapaka matope.
Hata wewe umetoa hoja kali sana. Kama HAMZA alikuwa mtu wa hovyo, ilikuwaje akapewa silaha? Ni kazi ya nani kumchunguza mtu anayepeka maombi ya kumiliki silaha? Kilangila.
 
Hayo maneno si kitu kabisa unapolinganisha na kosa kubwa alofanya Msomali la kuua watu wasio na hatia!

Uhai wa binadamu unathamani kubwa sana isiyo mithiri.

Uhai wa mwanadamu ukishapotea hauwezi kupatikana popote Duniani hata kwa kuuzwa !

Acheni chuki jamani !
Tuanzie hapa, uliwahi kudhulumiwa Sh. 400,000,000/=? Kilangila.
 
Siro ukimwangalia mwonekano wake kimwili utadhani ni mtu wa kuheshimika sana!

Hapana, kuna wakati hata matamshi yake yalionekana kuwa ya mtu mwenye busara.

Haieleweki ni kitu gani hasa kimembadilisha akili kiasi hiki alivyokuwa sasa?

Unajua, inasemekana damu za binaadam zikimwagwa kwa uonevu tu, hazimwachi mtu anayesababisha zimwagike, ni lazima atadhurika tu kwa njia moja au nyingine.

Siro ni mhanga wa umwagaji wa damu za waTanzania ambao hawakustahili kuuliwa au kuumizwa.

Maisha yake ya uhai wake uliosalia yatakuwa ya matatizo tupu.
Hakuna jambo baya kama kumwaga damu isiyo na hatia.
 
Ana stress kiasi,kesi Mahakama kuu,kifo Cha Hamza,uu staafu wake
Mambo ni mengi jamani........,
mlioko nje ya system ham oni ila walio ndani wanatamani kikombe kiwapite mbali lakini wapi
Hata ukiwa ndani mkuu, huna lazima ya kukinywa "kikombe" bila kutumia akili. Huwezi kujitoa ufahamu kwa vile tu upo ndani ya 'system'.
 
Kwahiyo unahalalisha hizo kauli za Sirro? kwanini usione kuwa Sirro pia nae kakosea?

Mwambie basi atuambie Mkewe Sirro alizaa vp wanae ili watanzania wajifunze jinsi ya kuzaa vizuri ili wapate watoto wakamilifu kama yeye?
Mkuu 'UHURU JR', ahsante sana kwa mstari wako huo wa pili ulioandika hapo juu; umejaa hekima nzito.
 
IMG_20210829_163012_555.jpg
 
Mrekodini matukio yake kisha mturushie humu ili na Sisi wa mikoani tuweze kumfahamu.

Hivi wale waliowashambulia watu Kule Z'bar au wale waliotaka kumuondoa Mh Lissu Duniani Kwa Sirro waliokuwa Sawa sio? Au wao hawakuwa na wazazi wala ndugu sio?? Kumbe Polisi ndio wenye kujua kuzaa sio? Kumbe ndio wenye wazazi na ndugu sio? Kuna mtu alikuwa analindwa na mabunduki kuliko yeye Sirro lkn Mauti hayakumuogopa.

Sirro ajue Mungu muweza wa yote yuko na anamsikia anamuona na anashuhudia utendaji wake wa kazi. Ameshawajaza raia hasira vyakutosha sasa ameanza ku beep Mungu ktk Uumbaji wake.

Hawa wote wanaodhulumiwa kwakuwa hawana wa kuwatetea, Mungu muumbaji wao alishasema kupitia vitabu vya dini" wale wote wenye Mamlaka wasipowatetea wanaoonewa basi ardhi itawalilia". Kila Jambo linalotendeka Lina kusudi Kwa Mungu hata hili la Mwamba Hamza.
Waliotaka kumuuwa Lisu kwa siro Ni watu Safi na ni watakatifu na hawapaswi hata kuchunguzwa. ZEEE shetani sana hili
 
IGP Sirro jana umetoa kauli nzito na ngumu mno kutolewa na kiongozi wa aina yako na mtu mwenye umri mkubwa kama wewe na mtu anayeheshimika kwa cheo chake kama wewe.

Angalia sana ulimi wako jinsi unenavyo, muombe sana Mungu akupe hekima ili kabla ya kutamka neno lolote hekima ikutangulie.

Jana ulitamka maneno haya nami nakunukuu.

"Watanzania kuweni makini msije mkazaa mtoto wa hovyo hovyo kama Hamza aliyetuletea majanga Watanzania, wazazi wa Hamza mnajisikiaje kuzaa mtoto kama huyo? Na nyie ndugu zake mnajisikiaje kuwa na ndugu kama Hamza?". Mwisho wa kunukuu.

IGP Sirro, hakuna mzazi anayepanga azae mtoto wa aina gani, Binadamu tunazaa mwili hatuzai Roho.

Kuna kijana anasumbua sana mitaani, anajitapa kwamba hakuna wa kumfanya lolote kwa sababu Baba yake ana cheo kikubwa mno serikarini, kijana huyo huvuta unga na kwenda hadi kwenye Hotel ya Baba yake iliyoko Chanika ambako hufanya vituko vya ajabu, ukiwemo kupiga watu.

Je, unajua huyo mtoto ni wa nani? Tafadhali sana, wazazi wa Hamza hawakujua kama wanazaa mtoto wa aina gani, hata wazazi wako wewe Sirro hawakujua kama ipo siku utakuja kuwa IGP.

JITOKEZE UIOMBE MSAMAHA FAMILIA YA HAMZA ILI ULINDE HESHIMA YAKO.
Hiyo Kauli aliyoongea siro siyo ya busara hata kidogo.
 
Back
Top Bottom