IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

Hayo maneno si kitu kabisa unapolinganisha na kosa kubwa alofanya Msomali la kuua watu wasio na hatia!

Uhai wa binadamu unathamani kubwa sana isiyo mithiri.

Uhai wa mwanadamu ukishapotea hauwezi kupatikana popote Duniani hata kwa kuuzwa !

Acheni chuki jamani !
Kama hayo makosa madogo ya dhulma uonevu mauji yanayofanywa na polisi yataendelea kuwepo basi pengine tutaraji haya makosa makubwa kama ya Hamza kuzidi kutokea. Na mimi sioni kosa kubwa kwa Hamza kwa sababu hakudeal na raia katika ugomvi wake yeye na polisi.

Mwambie Sirro kwani yeye na jeshi lake wamewafanyaje raia hadi wanafikia kuzaa watoto wanaouwa polisi?
 
IGP Sirro jana umetoa kauli nzito na ngumu mno kutolewa na kiongozi wa aina yako na mtu mwenye umri mkubwa kama wewe na mtu anayeheshimika kwa cheo chake kama wewe.

Angalia sana ulimi wako jinsi unenavyo, muombe sana Mungu akupe hekima ili kabla ya kutamka neno lolote hekima ikutangulie.

Jana ulitamka maneno haya nami nakunukuu.

"Watanzania kuweni makini msije mkazaa mtoto wa hovyo hovyo kama Hamza aliyetuletea majanga Watanzania, wazazi wa Hamza mnajisikiaje kuzaa mtoto kama huyo? Na nyie ndugu zake mnajisikiaje kuwa na ndugu kama Hamza?". Mwisho wa kunukuu.

IGP Sirro, hakuna mzazi anayepanga azae mtoto wa aina gani, Binadamu tunazaa mwili hatuzai Roho.

Kuna kijana anasumbua sana mitaani, anajitapa kwamba hakuna wa kumfanya lolote kwa sababu Baba yake ana cheo kikubwa mno serikarini, kijana huyo huvuta unga na kwenda hadi kwenye Hotel ya Baba yake iliyoko Chanika ambako hufanya vituko vya ajabu, ukiwemo kupiga watu.

Je, unajua huyo mtoto ni wa nani? Tafadhali sana, wazazi wa Hamza hawakujua kama wanazaa mtoto wa aina gani, hata wazazi wako wewe Sirro hawakujua kama ipo siku utakuja kuwa IGP.

JITOKEZE UIOMBE MSAMAHA FAMILIA YA HAMZA ILI ULINDE HESHIMA YAKO.
Wee muache tuu, si anaona kuwa IGP hapa Tz ameshapatia maisha.... Kuna kizazi chake kinakuja na kitabeba jina la ukoo... Asidhanie kuna mtu anapenda kupata mtoto ambaye baadae atakuja kuwa msumbufu duniani. Ni hakika kauli yake kwa asilimia Mia, ni ya kuudhi bila kujali wewe ni mtanzania au si mtanzania. Ili mradi tuu ni binadamu ukiisikia kauli yake unasikia ukakasi kwa ndani.
 
Hayo maneno si kitu kabisa unapolinganisha na kosa kubwa alofanya Msomali la kuua watu wasio na hatia!

Uhai wa binadamu unathamani kubwa sana isiyo mithiri.

Uhai wa mwanadamu ukishapotea hauwezi kupatikana popote Duniani hata kwa kuuzwa !

Acheni chuki jamani !
Mkuu wliouawa ni polisi sio watu naomba urekebishe
 
Nani alisema kuwa Lenana ilijengwa Siro alipoingia mjini? Huwezi kujenga kabla hujaingia mjini.
Huo Ni uongo mwenye Lenana namfahamu.Hamna tofauti na yule jamaa maarufu wa mitandaoni aliyesema Hill water Ni ya yule Mbunge Kessy wa CCM,akiambiwa sio mwenye nayo anakomaa kusema unajua Nani Yuko nyuma ya huyo mmiliki hahah.Hillary alisikitika Sana.

Simkubali Sirro na mambo yake lkn kwny uongo nitakataa.
 
Kwani walioko shamba hawaruhusiwi kujenga? wewe unacheza na kazi ya upolisi, kazi ya upolisi unaweza tajirika wakati wowote haijalishi unacheo au hauna, ogopa mtu anayedeal na waalifu.
Hizo story mkawapigie wasiojua lkn sio Mimi mzee.
 
Hadi page ya nane hakuna picha wala jina la huyo mtoto wa siro!
Wabongo tunakwama sana, hawa ni wauaji, madhulumati bado watu mnaojua kiasi kuwahusu mnafichaficha kama vile ni mali halali itakayowafaidisha.
Wananchi tusipoichukua hii vita, tukiviachia vyama vya siasa pekee tutakuwa tumebugi sana.
 
Back
Top Bottom