IGP Sirro, huyo ni mtoto wa nani?

Vipi kuhusu huyu wa chanika? Ambaye ni mtoto wa inspector general na bado anapulizia watu bangi usoni? Baba yake ndiye alimfundisha hivyo?
 
Huyo ni Mtoto wa Sirro anasumbua watu sana mtaani kwa ubabe wake na anavuta bangi hadharani. Muda Mwingi anashinda Chanika kwenye Bar ya Baba yake.
Mrekodini matukio yake kisha mturushie humu ili na Sisi wa mikoani tuweze kumfahamu.

Hivi wale waliowashambulia watu Kule Z'bar au wale waliotaka kumuondoa Mh Lissu Duniani Kwa Sirro waliokuwa Sawa sio? Au wao hawakuwa na wazazi wala ndugu sio?? Kumbe Polisi ndio wenye kujua kuzaa sio? Kumbe ndio wenye wazazi na ndugu sio? Kuna mtu alikuwa analindwa na mabunduki kuliko yeye Sirro lkn Mauti hayakumuogopa.

Sirro ajue Mungu muweza wa yote yuko na anamsikia anamuona na anashuhudia utendaji wake wa kazi. Ameshawajaza raia hasira vyakutosha sasa ameanza ku beep Mungu ktk Uumbaji wake.

Hawa wote wanaodhulumiwa kwakuwa hawana wa kuwatetea, Mungu muumbaji wao alishasema kupitia vitabu vya dini" wale wote wenye Mamlaka wasipowatetea wanaoonewa basi ardhi itawalilia". Kila Jambo linalotendeka Lina kusudi Kwa Mungu hata hili la Mwamba Hamza.
 
" Watanzania kuweni makini msije mkazaa mtoto wa hovyo hovyo kama Hamza aliyetuletea majanga Watanzania, wazazi wa Hamza mnajisikiaje kuzaa mtoto kama huyo? Na nyie ndugu zake mnajisikiaje kuwa na ndugu kama Hamza?".

Nasi tunajisikia vibaya sana wazazi wake Siro kuzaa mtu kama yeye na siyo yeye Polisi wote wanaofanana na yeye wenye kuleta uonevu na kuleta umaskini kwa jamii kwa vitendo vyao viouvu.Tunashangaa sana wazazi wao waliwazaa vipi?

Imekuwaje wazazi wao wakazaa aina ya viongozi mbugila mbugila , akili tope wenye kauli chafu za kuudhi na kuumiza watu ni aina gani ya wazazi waliwazaa hao jamaa?

Kwa mantiki hiyo tunawalaumu sana wazazi wa viongozi jinsi walivyokuza akili mbovu ..ingewezekana wangewatupa vyooni mapema sana wajifie huko kuliko kuleta watu wenye lugha chaafu halafu ni watu wazima.
 
Hamza angekuwa na mama yake nae ana bunduki pale Salenda angestahili dharau hizi lakini maskini hata yeye atakuwa amejua kupitia vyombo vya habari kama Sisi. Sirro angekuwa umewahi kubeba mimba hata wiki moja usingeharisha huo utumbo wake.
 
Nasikia Kuna mtoto akiwa na genge lake aliwahi kudhulumu wazungu dhahabu ya mabilioni ya fweza akakimbilia airport kwenda mwanza Cha ajabu hakuna data zozote zilizoonekana airport zote mbili alikotoka na alikotua eti data hizo zilifichwa kimagumashi je Toto hilo ni lanani?
 
Hata mimi jamaa nilikuwa namkubali sana speech zake kipindi kile anawapa mawaidha wakina mambosasa.
Inawezekana amevurugwa na formality ya uongozi kubadilika na hajui hatima yake.

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Yaani Huyo kamanda utadhani Hamza na Yeyr hawako chama kimoja. Kila kauli inaonesha anamkana.
 
Watu wengi hamjuwi kilichopo moyoni mwa IGP ila nataka niwahakikishie ndani yake ameshasoma alama za nyakati na anatamani aruhusiwe kustaafu maana alisha staafu sema wakamkatalia sasa moyo wake anatamani kustaafu na ndio maana anaongea sentence tata atumbuliwe basi. Ila ndio wana kaa kimya. Hata ingekuwa wewe ungetamani kustaafu maana muda wake ktk utumishi wa umma umefika then watafute mwingine. Nadhani hayo ndio siri moyoni mwake.
 
Jeshi loote la polisi hawana mtu mbadala wake? Basi kuna shida mahali
 
Mimi ninachokiona ni Kutaka kumbebesha Mzigo Hamza. Tunajua hamza ana makosa makuba kuwaua wale Polisi wetu. Lakini bado ukweli haujulikani wale polisi walikuwa wamemfanya nini. ni Kama kamanda anataka kuonesha upande mmoja tu kuwa Hamza ana makosa pekee yake.

Hii kesi ya Hamza na naifananisha na kezi ya Abdalla zombe
 
Sasa alikuaje mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM?!!

Au CCM ni kokoro by John Komba rip.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…