IGP Sirro: Jeshi la Polisi kukagua yanayofundishwa kwenye nyumba za Ibada

Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa lintakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameeleza hayo wakati akizungumzia ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.
“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au yanawabomoa vijana.
Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.
Yaani hata hili Dogo nalo alienda kujifunza Rwanda. Nilidhani angekuja na karipio la kupiga marufuku makanisa ya mitaani.
 
Tenda haki you will be safe! Kama mtu Ana sababu za kutosha moyoni kwake kujifunza kitu haitaji Mwalimu au mahali.
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Source: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti!
Wakienda hao wakaguzi, wanapigiwa kareti za tumbo, wajiharishie mji mzima, Hadi wakifika kwa wake wakose Cha kuelezea. Nawakaribisha Mtambani
 
Hivi kujua karate ndio ugaidi ? Hii nchi hata maombi hayatasaidia chochote , tuachane nayo tu
Kwa kweli maana kuna baadhi ya watanzania hawatumii akili ndo maana hua wanakua brainwashed easily na kubeba chuki dhidi ya wengine halafu wanajifanya wapenda amani na wao ni watu wema,very funny
 
CUF walikuwa wanajifunza judo kwenye nyumba za mitume!
 
Tenda haki you will be safe! Kama mtu Ana sababu za kutosha moyoni kwake kujifunza kitu haitaji Mwalimu au mahali.
Haswaaaaa,wanatengeneza mabomu halafu yakiripuka wanatafuta chanzo ni nini wakati walitengeneza wenyewe,facts over opinions and hate as I always say
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.
Mnafiki mkubwa IGP Sirro.
Kaambiwa amkamate Gwajima kwa kumpinga sera za Mama Samia kuhusu Covid19 hakutekeleza amri.
Sasa unafiki huo aanze kwa kutembelea kanisa la Gwajima.
 
CUF walikuwa wanajifunza judo kwenye nyumba za mitume!
Hebu tuonyeshe hizo nyumba za mtume huku Tanzania ziki wapi? Second kwani kujifunza judo ni kosa?? Nchi ngapi wanajifunza umewahi kusikia ni kosa,pole sana,you are sick
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.
IGP sasa anafukuza watalii kwa kuitangaza Tanzania kuwa kuna ugaidi
 
Hebu tuonyeshe hizo nyumba za mtume huku Tanzania ziko wapi? Second kwani kujifunza judo ni kosa?? Nchi ngapi wanajifunza umewahi kusikia ni kosa,pole sana,you are sick
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.

Hivyo kujifunza kareti ni kujifunza ugaidi??!!
 
Tunajua nyumba za ibada wanazozilenga. Lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu anajifunzia ugaidi msikitini, sio Tanzania labda nchi nyingine huko.

Badala ya kutafuta sababu za msingi na vyanzo halisi vya ugaidi wao wanaanza kutafuta chuki na uhasama na dini fulani. Upumbavu nao ni kipaji.
Pesa hakuna wamebuni miradi ya kuwabambikia kesi watu kwa visingizio vya ugaidi ambao haupo Tanzania ni aina fulani ya uonevu wa kuwatisha wananchi wawaogope Polisiccm ili CCM iendelee kukaa madarakani milele na milele
 
Back
Top Bottom