IGP Sirro: Jeshi la Polisi kukagua yanayofundishwa kwenye nyumba za Ibada

IGP Sirro: Jeshi la Polisi kukagua yanayofundishwa kwenye nyumba za Ibada

IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.
===
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameeleza hayo wakati akizungumzia ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.

“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au yanawabomoa vijana.

Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.
Hiyo sio kazi ya jeshi la Polisi mosi, pili hakuna uhusiano wa mfano wa Rwanda na Tanganyika, Tatu angewashirikisha BAKWATA kwa upande wa waislam ambao nadhani ndio wahanga wa kuu wa hili, hizo Sunday schools zimetajwa kubalance stori tu, lakini pia wafanye utafiti wa mitaa badala ya kukurupuka, mfano Wakatoliki hawako radical kama walokole (mf juzi Gwajima yuko live kanisani kwake anatetea msimamo wake wa kuiprovoke, kuibehua na kuitweza serikali na viongozi wake, eti Adai ni ufunuo kutoka kwa Mbwana Mungu wake), huko kwa Waislam pia kuna makundi na makundi, mfano kuna ikhwaan muslimuna na khawarij ambao wao kwao jihad ni ibada ya kwanza nyingine zafuatia, tofauti na wale Masalafiy ambao wao wanahamsisha twaa kwa viongozi hata kama ni Makafiri.

Kwa hivyo sirro awe makini japo naamini kazi itamshinda, ama hatofikia target (kwakuwa sio realistic, na principles zinataka uhalisia unapo project), au Atapata taabu kisha atakwaza watu na atakwazika yeye na mwisho tutamshangaa sote.
 
Ndio hivyo. Kazi inafanywa kimya kimya kupitia special agents. Hilo ni eneo nyeti la kazi. Kuna masheikh/maimam na wachungaji na waumin ambao ni maajent wa CID/TISS. Walitakiwa wawe wanafanya kazi hiyo tangu tunapata uhuru.

Hii kutangaza hadharani ni kutafuta sifa za kisiasa. Ni aibu. Kama vile ma-informer wa TISS wanavyojitangaza mitaani siku hizi.
Mtaa gan
 
Siamini kama idara ya usalama haijui kinachofundishwa kwenye madrasa na hizo sunday schools (jumuiya za mitaani kila j'mosi). Ila kama mnasema kuna wanaolengwa haya, ngoja tuone!!
TISS




WW KWELI HUJUI NGOJA MWISHONI NITAELEZEA. JAMBO
 
Mnaoshabikia kuna mambo hamjajua

Kuna shule kubwa tu

U ya advance

Nchi nzima idara zote za usalama na vyombo vilishindwa ku imulika. Mpaka ikawa too much

Nahapo wakuu wa nchi hii walienda na kutoa matamko na kutisha watasambaza wanafunzi nchi nzima

Miaka zaidi ya 10 tiss ilikuwa imelala nguvu zinahitajika

Ndo mara ya kwanza kuona watu wanasema waziwazi ndio wakuu wa usalama wa taifa mkoa na wilaya
 
#WATAHANGAIKA_SANA

يُرِيدُونَ لِيُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَاللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

Surat (ASS'AF - 8)
"Wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao. Na Mwenyezi Mungu atakamilisha nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia."
___

Hata Firauni naye alipeleka Askari wake wakague Nyumba kwa Nyumba ili kuhakikisha Kama Kuna mtoto yoyote wa Kiume amezaliwa, basi auawe. Matokeo yake, yule aliyemuona ADUI yake, ndiye aliyemlea katika kasri lake na ndiye aliyekuwa sababu ya maangamizi yake.
___

"Wanapanga mipango, ALLAH naye anapanga mipango (yake), na ALLAH ni mbora wa mipango
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti...
My observations;
Tunaanza kuabudu na mitutu na pingu kwenye nyumba za Ibada? Na Je IGP na watu wake wameiva kwenye Quran na Biblia?
 
Target hasa ni madrassa, hii sunday schools ni red herring. Wanajaribu kutaka kutuonesha kuwa matendo ya Hamza ni zao la elimu ya dini.
 
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa
Amekosa kazi za kufanya
 
Hana kazi huyo, wamebaki kubambikia watu vyesi vya ugaidi ipo siku magaidi watatinga hapa ndio atawajua vizuri naona anawasikia tu.
 
Target hasa ni madrassa, hii sunday schools ni red herring. Wanajaribu kutaka kutuonesha kuwa matendo ya Hamza ni zao la elimu ya dini.
Basi tungekuwa na magaidi sana imagine kuna madrasa ngapi?
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.
...
Ni mjinga tu anaamini kareti ni ugaidi, zipo shule nyingi sana na vikundi vya mitaani hufundisha kareti na hazina magaidi, na kama ni hivyo nchi za China, Japani na nyinginezo za mashariki ya mbali zinvekuwa ndiyo kitovu cha ugaidi duniani, pia hakuna gaidi anatumia kareti labda akimfumania hawara ya mke wake.
 
Makosa makubwa sana yalifanywa na serikali kuwashirikisha viongozi wa dini kwenye siasa ovu.

Sasa viongozi wa dini wakiazimia kupinga na kuungana na wapinzani kuiondoa wanaowaingilia shughuli zao itakuwaje?
 
Kwani huko si wanafundisha Biblia na Kuruani? Naamini Biblia anaijua, si ajifunze Kuruani ili ajue somo la msikitini bila kwenda kwenye misikiti?!
 
Back
Top Bottom