IGP Sirro: Jeshi la Polisi kukagua yanayofundishwa kwenye nyumba za Ibada

Mbona kuna sehemu za kufundisha karate hata baadhi ya shule ni kama somo tu. Hapo kuna watu wamelengwa tayari.
Mfano Centennial Christian Seminary pale mbele ya Kongowe mkoa wa Pwani.

Watoto wale wanapiga ngumi kama mizimu aisee!
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.
===
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameeleza hayo wakati akizungumzia ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.

“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au yanawabomoa vijana.

Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.
Uzalendo unafundishwa kwenye nyumba za ibada? Taasisi yake unafundisha aje uzalendo, Kwa kuweka taswira na mazingira ya rushwa, kubambikia makosa yasiyokuwapo, kupendelea CCM?
Anza kwako ndugu!
 
Rwanda ni Nchi ya kidikteta hakuna uhuru wa kuabudu, ni Aibu kubwa kwa Tanzania kujifunza mbinu haramu za kishetani toka Rwanda
Sinema ya Royal wameiga Rwanda na huu uharamia nao wamechukua Rwanda !
 
Kama sio kutaka kuudhi jamii flani,
Hili jambo wala ilikua haina haja ya kulitangaza ni kufanya tu kimya kimya,
Lakini imesemwa"hawatawadhuru isipokuwa maudhi tu"
 
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa lintakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameeleza hayo wakati akizungumzia ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.

“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au yanawabomoa vijana.

Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.
Good approach!
 
IGP Sirro amesema jeshi lake litaanza kukagua yale yanayofundishwa kwenye nyumba za ibada.

Chanzo: Swahili times

My take; Baadhi ya nyumba za ibada huzalisha magaidi kwa kufundisha kareti.
===
Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa litakuwa likipita katika nyumba za ibada kukagua mafunzo wanayofundishwa watoto katika madrasa na shule za Jumapili (Sunday schools) kufahamu aina ya mafundisho yanayotolewa.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro ameeleza hayo wakati akizungumzia ziara yake ya siku nne nchini Rwanda na kusema wamejifunza hilo kutoka huko, hivyo ni vyema wapite kwenye maneno hayo kujua malengo ya mafunzo yanayotolewa.

“Tumeona wenzetu hizi shule za dini, kwa mfano haya Madrasa, kwa mfano hizo Sunday schools kuna kikosi maalum kuona mafunzo yanayofundishwa. Je! Mafunzo yale yanatolewa kwa ajili ya uzalendo, au ni mafunzo yanayotolewa kwa ajili ya kuharibu nchi,” amesema Sirro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sirro ameeleza utaratibu huo ni mzuri na kwamba watawashirikisha viongozi wa dini na timu ya kupambana na makosa ya kigaidi kuona namna ya kupitia mafunzo yanayofundishwa kwenye shule za dini na shule za elimu dunia, hadi ngazi ya vyuo vikuu, kuona kama mafunzo yanawajenga au yanawabomoa vijana.

Aidha, ameitaka jamii kutoa taarifa endapo itabaini kuna mtu ana tabia au mwenendo kinyume na jamii husika, na kwamba sio lazima mhusika afungwe, bali wanaweza kumsaidia kuwa mtu mwema na akaendelea na shughuli zake.
This should have been done secretly. Why putting it public?
 
Hapa wanalenga madrasa, hiyo ya sunday school ni zuga tu...
 
Unaona huyu mwehu kada wa CCM amesahau Tanzania haina dini wala kabila na kila mtu ana haki ya kuamini anachoamini, kinachofundishwa huko misikitini au makanisani hakiwahusu na hamna haki ya kuwapangia wafundishe nini au waamini nini, kama kuna issue wasubirini waje huku nje wavunje sheria ndio mpambane nao, hizi hadithi za ugaidi kutoka kwa hawa maboya kina Siro na wenzake naona zimezidi na hakuna ushahidi, huyu boya anajua kuteka watu tuu, wizi wa kura na kubambikia watu kesi, simpendi kabisa huyu mpuuzi anaharibu nchi tuu
 
Mambo kama Haya yatupasa kuunga mkono juhudi za Viongozi wetu katika kusimamia maswala ya kiusalama.
Ukianza kuruhusu serikali kuingilia mambo ya watu wanachofundishwa au kuamini makanisani, misikitini au nyumba zao za ibada ndio mwanzo wa total dictatorship,nchi haina dini na kila mtu ana haki kuamini anachoamini sheria za nchi ziheshimiwe tusiingiliane na viongozi nao ni watu tuu, kama kuna sheria ya nchi imevunjwa protocol zifuatwe
 
Tenda haki you will be safe! Kama mtu Ana sababu za kutosha moyoni kwake kujifunza kitu haitaji Mwalimu au mahali.
Kweli, wao wenyewe walisema Hamza alijifunzia ugaidi mitandaoni leo wanataka kukagua madrasa.
 
IGP SIMON SIRRO AJA NA MAPYA: JESHI LA POLISI SASA KUCHUNGUZA MAFUNDISHO (DOGMA) MAKANISANI NA MISIKITINI!

Mkaguzi wa Mtaala ni lazima aujue mtaala au awe na elimu kuhusu mitaala! Mitaala ya Shule ya Jumapili (Sunday School Curriculum) hutungwa na wasomi na wataalamu wa Theologia (Theology), Masomo ya Biblia (Biblical Studies), Falsafa (Philosophy) na Elimu ya Dini (Religious Studies/Education). Jeshi la Polisi nchini Tanzania linataka kujipa kazi ya kukagua Mitaala ya Sunday School Makanisani. Tunawakaribisha Askari Polisi kujiunga katika Vyuo vya Theologia na kwenye Seminari Kuu ili kusomea masomo hayo. Liandae watu wenye sifa kwa ajili ya kusomea Shahada za Theologia na Falsafa. Baada ya hapo wakasome ubingwa (Shahada za Juu) katika masomo hayo wakibobea katika Mitaala!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

B2DA996A-99A8-47F3-A204-8EBD694FF753.jpeg
 
Back
Top Bottom