IGP Sirro: Kipindi cha kampeni nilimtafuta Tundu Lissu aje kuhojiwa lakini hakuja

..IGP amekosea kutoa kauli za kumkashifu Tundu Lissu.

..kusema Lissu anatumia hilo tukio la kushambuliwa kujipatia kipato na kulelewa na wazungu sio sahihi.
Ni uongo?
 
Waziri wa mambo ya ndani, wakati huo Mwigulu Nchemba, alisema kwamba gari yenye namba ambazo Tundu Lissu alidai inamfuatilia ilionekana Arusha.

..Na waziri wa mambo ya ndani akadai kwamba wamewahoji wahusika na wamejiridhisha kwamba gari hiyo haikuwahi kufika D'Salaam.

..IGP Sirro anadai Lissu hakuwahi kutoa taarifa kituo cha polisi kuhusu kufuatiliwa. Vilevile IGP anadai polisi hawana taarifa zozote kuhusu Lissu kufuatiliwa na " watu wasiojulikana. "

..Sasa katika mazingira kama hayo tumuamini nani? Je, Waziri wa mambo ya ndani alidanganya? Je, IGP anadanganya?
Mwambieni Lisu na dereva wake waende polisi kuhojiwa
 
Siro naye ni mjinga wa kutupwa kama wajinga wajinga wenzake.
 
Kuna utofauti mkubwa kati ya kesi ya mauaji na kesi ya kujeruhiwa
Acheni kupotosha. Polisi walitakiwa kufungua jalada la uchunguzi mapema tu. Kuna wale waliokuwepo nyumba za jirani ambao walishuhudia na hata kusikia milio ya risasi. Hao ndio wa kwanza kuhojiwa. Hakuna aliyehojiwa.
Kuna ishu ya kamera za cctv. Tunaambiwa ziliondolewa. Hatujaelezwa chochote. Kuna walinzi wa eneo hilo ambao pia waliondolewa. Na kama hawakuondolewa, basi hao ni mashuhuda muhimu. Kama waliondolewa mapema, basi tukio zima lilipangwa na mamlaka ya juu.

Kuna kamati maalum iliyoundwa na Bunge, chini ya Adadi Rajabu. Tunaambiwa siku iliyopangiwa kuwasilisha ripoti Bungeni, ghafla taratibu zikabadilishwa na ripoti hiyo haikufika Bungeni. Kwa nini? Jibu ni wazi. Kuna mamlaka yenye nguvu ambayo haitaki uchunguzi ufanyike.

Ukimsikiliza vizuri Kamanda Sirro, haongei kama afisa wa polisi, kama ambavyo mtu kama Ernest Mangu angeongea. Haongei kitaalamu, anababaisha. Ana ushahidi gani kwamba Tundu Lissu kaenda Ubelgiji kutafuta unafuu wa maisha? Matibabu je?

Sirro anaongea kama kikaragosi cha watawala. Anawasaidia watawala
 
Wangemuuliza wamefiki wapi na ya Ben, Azory, viroba kuelea, ofisi za Immma, Mo, Roma na wengine
 
Kwa nini uhoji jirani wakati mwenye tukio yupo?
Nani mwenye taarifa sahihi kati ya jirani na Lisu?
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amesema kwenye kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 alimpigia simu Lissu ili aje kituo cha polisi amhoji na atoe maelezo ya nini kilitokea hasa aliposhambuliwa kwa risasi jijini Dodoma lakini hakwenda kituo cha polisi hadi leo.

Sirro amesema Tundu Lissu anatumia hilo shambulio kama njia ya kujipatia kipato na kuweza kulelewa na wazungu Ulaya.

Pia, soma: Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji

View attachment 1849358
Kijogoo D,Naona nguvu zipo za kutosha,nivyema ukazitumia vyema,zikipotea hazirudi.Ni mawazo tu.
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro amesema kwenye kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 alimpigia simu Lissu ili aje kituo cha polisi amhoji na atoe maelezo ya nini kilitokea hasa aliposhambuliwa kwa risasi jijini Dodoma lakini hakwenda kituo cha polisi hadi leo.

Sirro amesema Tundu Lissu anatumia hilo shambulio kama njia ya kujipatia kipato na kuweza kulelewa na wazungu Ulaya.

Pia, soma: Tundu Lissu: IGP Sirro ni Jeshi la Polisi, hawajawahi kunipigia simu wala kunihoji

View attachment 1849358
Kwani Lissu bado yupo jamani, mbona hatumsikii?
 
Back
Top Bottom