IGP Sirro: Tunakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu baada ya kupokea fedha nyingi takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje

Kutetea haki za binadamu B6 zote hizo ni za nini kama sio hujuma.
Akili za kimaskini shida sana! Kwa hiyo unaona bilioni 6 ni hela nyiiiingiiiiiii?????

Kweli CCM wameharibu taifa!!!!
Nikwambie tu ndugu, hizo ni hela ndogo saaana hasa kwa ofisi.

Akili yako ya kimaskini na kukosa exposure isikufanye uone hiyo hela ni nyingi sana.
 
Unajifanya unajuaaaa kumbe hamna kituu, kama b6 ingekuwa ndogo serikali isinge funga account zao.
Tena haswa pale hela inaiingia kutoka nje bila maelekezo yoyote punguza mahaba tanzania kwanza chadema baadae.
 
Unajifanya unajuaaaa, kama b6 ingekuwa ndogo serikali isinge funga account zao.
Kwa iyo we jambo lolote linalofanywa na serikali we unaona wako sahihi! Kwa iyo kuzuia matibabu ya Lissu walikuwa sahihi??! Kuzuia vyombo vya habari kutangaza Habari za Lissu wako sahihi????

Embu kama huna exposure omba uambiwe ili ujue!!!

Serikali ya kipindi hiki mambo mengi wanayofanya ni kwa nia ovu hasa kuongopa wao kupata changamoto full stop.

Nenda kwenye NGO kubwa tena zinazofanya kazi nchi nzima watakwambia bil 6 sio hela. Wao hiyo ni hela ya kawaida sana maana kuna miradi hadi ya bil 10 mpaka 50. Sembuse bil 6????
 
Aeleze Sheria inasemaje kuhusu hizi NGO mwisho wao kutumia au kupokea ni shilingi ngapi
 

Hofo ya lisuu yote hio
 
Fedha za miradi hutolewa kutokana na mahitaji halisi. Hii hutokana na kile kilichopo ndani ya 'techical & financial proposals" na kukubalika kutokana na matakwa ya "funders". Kusema TZS 4Bn ni kiasi kikubwa na kuzitilia ni sababu nyepesi sana na kukosa elimu sahihi juu ya uendeshaji wa miradi
 
Kwahiyo anataka watu wakionewa kituo kisiweze kuwatetea kwa kukosa pesa. Kama ukiukaji wa haki za binadamu unaongezeka alitegemea gharama za kuwatetea zisiongezeke pia wapunguze unyanyasaji wa raia na matumizi ya hicho kituo yatapumgua automatically.
Tujiulize sheria inasemaje? Bongo ukikubali kusajiliwa, ukubali kukumbana na sheria zinazokuongoza. Sheria inakutaka ku "declare source of income" unachokwepa nini? Umekuwa "Kuku Project?" unajifanya unafugisha kuku kumbe upatu. Akaunti ikivimba utafuatwa tu
"explain why the NGOs had failed to heed government call to submit its contractual agreements with foreign donors as required by the law."
 
Siasa za kwenye mitandao ya kijamii raha sana.
We endelea kudharau mitandao ya kijamii, ipo siku utafurahi. Dunia imeshabadilika usipokubali kwenda nayo utaachwa. Kama haujui Social media na vijana ni damudamu ma hao ndio anguko lenu kama hamjawekeza huko.
 
Hivi taasisi kama hivyo bil 6 ni fedha nyingi? Mmepitia proposal zao kujua hivyo bil 6 waliomba kwa mchanganuo gani? Onesmo ni mtetezi wa haki za Binadmu kweli,polisi acheni kutumika na wanasiasa.
 
Hiyo hela hata msanii Diamond unaweza kuta anayo kweny kibubu chake iweje kwa NGo kubwa ile.
 
johnthebaptist,

Hamna lolote CCM na serikali yake wanatapatapa kuelekea kibra, kazi kwenu mlijifanya wajuaji haya sasa mnakaangwa na wenye dunia mmeshaingia kwenye kumi na nane.
Hakuna fedha isiyokuwa na shughuli ya kufanya,tatizo hapa kutatokea utaifishaji kwa visingizio vya kibabe.Kituo cha Hali za Binadamu wanapewa bajeti na Bunge?Kama jibu ni hapana,na taasisi hiyo ipo kisheria,IGP amewahi kujiuliza kwamba huwa kituo hicho kinaendeshwaje?
 
Kikawaida walipaswa kutumiwa shilingi ngapi?

Laki tano, milioni moja , kumi au vipi?

Na hizo pesa huwa wanazitumia wapi mbona hatuoni kazi yao,
Wana miradi gani, wanatetea akina nani kuku mikoani?
Au kazi yao ni kutetea wanasiasa peke yao?
Hatujawahi kusikia wanatetea watu kukosa maji, au watu wanaopewa kesi si halali, huku magerezani bali wao wanazitumia hizo pesa wapi?
Na hilo shilika mlezi wao ni nani ni mabeberu au lina jiendesha kutokana na nini?
 
Naona una hofu hadi unakaribia kuchanganyikiwa. Kama hujui miradi yao umezuiliwa kwenye ofisini kwao kuangalia miradi yao??? Umeshindwa hata kufungua website yao tu????
 
Nchi ya hovyo sana
 
Wewe unataka serikali ifanye kama anayotoka lisu na watu wake wakati wao hawataki kufata utaratibu wa serikali. unajua kuna vitu vingine nibora angevifanya raia wa kawaida ambaye hajui tratibu zinakuwaje lakini sio kwa wakina lissu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…