IGP Sirro: Tunakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu baada ya kupokea fedha nyingi takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje

IGP Sirro: Tunakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu baada ya kupokea fedha nyingi takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje

IGP Sirro amesema jeshi la polisi linakichunguza kituo cha Kutetea Haki za Binadamu kinachoongozwa na Ole Nguruma baada ya kituo hicho kupokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka nje.

Sirro amesema kwa mwaka huu pekee kuanzia mwezi January kituo hicho kimepokea takribani Tsh bilioni 6 kutoka nje hivyo Jeshi linataka kujiridhisha uhalali wa fedha hizo zisijekutumika kwa nia ovu ikiwemo ugaidi na utakatishaji.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia!

Maendeleo hayana vyama!
"Kwa Sasa wenye fedha zao,epukeni mabank Kama ukoma"
 
IGP Sirro amesema jeshi la polisi linakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu kinachoongozwa na Ole Nguruma baada ya kituo hicho kupokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka nje.

Sirro amesema kwa mwaka huu pekee kuanzia mwezi January kituo hicho kimepokea takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje hivyo Jeshi linataka kujiridhisha uhalali wa fedha hizo zisijekutumika kwa nia ovu ikiwemo ugaidi na utakatishaji.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia!

Maendeleo hayana vyama!
Swali kifikirishi je unaweza kujenga nyumba ya bilioni 5 kama inawezekana basi hizo pesa siyo nyingi
 
Ina maana siku hizi donors kutuma hela kwa wadau hairuusiwi tena kwan mboga mboga mnaogopa nini
Wewe unafikiri Donors wanatoatoa tu pesa!! Kama ni halali si waseme ni za nini?? Siyo kuja kuanza kufadhiri magaidi hapa nchini si umeona kuna watz watatu wamefikishwa mahakamani jana kwa tuhuma za ugaidi!!
 
Dah hii ni Tanzania.Kaka yangu Ole Ngurumwa hata wakizuia Pesa.lazima tutawanyoosha tu kwenye sanduku la kura ije jua ije mvua.
Mbona wakati Kituo hiki kinapata pesa hio ilitangazwa katika vyombo vya habari? Haikufanyika kwa kificho na ilielezwa makusudi ya pesa hizo. Hao donors walitangaza fursa ya ruzuku hio, Kituo kikapeleka proposal kikapata. Shida iko wapi? Au wanataka zikajenge reli? Kama hazitaki basi wazirudishe zilikotoka!
 
Wanaogopa zitatumika kumsaidia kijana mtukutu kufanya kampeni kuna muda nawaza nimezaliwa Tz bahati mbaya au makusudi ila najikuta naichukia tu nchi yangu kwa ujinga mwingi badala ku focus na mambo ya msingi na yenye mantiki siasa tu mda wote
Nchi zingine wanakaribisha fedha kama hizo kama uwekezaji,mradi tu taratibu wezeshi ziingie kihalali na kukaguliwa zinafanya nini zikishaingia.Hapa kwetu muda siyo mrefu ukiwa na fedha Benki zinaweza kuchukuliwa na mamlaka kwa visingizio visivyo na mashiko. Tunapopambana na adui umaskini huku tunakataa raslimali ikiwemo misaada ya Diaspora au uraia wa nchi mbil(Duo-Citizenship),yote hiyo ni kuwafungia wasomi na watu wajanja ili wasije kuwafumbua Watanzania macho kuhusu Dunia inavyoendeshwa kisayansi huku tukihakikisha wananchi wanabaki gizani.Ujinga ni mtaji wa CCM na Umaskini wetu ni silaha ya kujilinda na Ujinga ndiyo Jela ya Watanzania.
Hii Nchi ni Yetu sote,Kituo cha Haki za Binadamu kinahitaji fedha za Uendeshaji,Serikali inayojitambua ingekipatia fedha ila hapa kwetu ni kinyume chake.Wakipata fedha toka kwa Wasamaria wema pia inakuwa nongwa?Kazi ya Kutetea Haki za Binadamu haisadii Serikali ya CCM?Nani hasa anayevunja Haki za Binadamu?Serikali haiwezi kuweka namna ya kufanya ukaguzi wa mapato/matumizi ya NGO's zinazofanya kazi nchini?Sheria zilizoanzisha hizo NGO inasemaje?Taratibu,Sheria na Kanuni zilizoanzisha hizi taasisi zinaruhusu Disputes zake kuwekwa Public kwa jinsi hiyo hata kabla ya Uchunguzi?Hapo wanataka kusema wameshatoa hint kwa wachunguzi/wapelelezi kuwa ni aina gani ya matokeo ya uchunguzi yanatarajiwa na watawala.Hawawezi kuja na hoja zitakazoonyesha kuwa IGP alikurupuka kuutangazia umma jambo ambalo hajalifanyia utaifiti wa kutosha.
Sifahamu aina hii ya Uongozi inayotumika na huyu Kamanda na Watawala wetu inaitwaje?Democratic,Autocratic,Buerocratic,Laizer's Fare or Dictatorship type of Admistration?
 
Another hopeless from the hopeless police.

TZS 5 billion - only $2m, imekuwa tatizo. Ni uwendawazimu tu. Mtakatishaji gani wa fedha anayetumia mifumo wazi ya kibenki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IGP Sirro amesema jeshi la polisi linakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu kinachoongozwa na Ole Nguruma baada ya kituo hicho kupokea kiasi kikubwa cha fedha kutoka nje.

Sirro amesema kwa mwaka huu pekee kuanzia mwezi January kituo hicho kimepokea takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje hivyo Jeshi linataka kujiridhisha uhalali wa fedha hizo zisijekutumika kwa nia ovu ikiwemo ugaidi na utakatishaji.

Chanzo: BBC Dira ya Dunia!

Maendeleo hayana vyama!
Safi sana.



MAGUFULI4LIFE.
 
Diplomatic language ni shida Tanzania.

Kulikuwa na namna nyingi za kutolea maelezo kwanini serikali imeamua kuchunguza.

Mfano IGP angeweza sema historical income and expenditure ya taasisi inaonyesha funding ya mwaka huu ni kubwa sana kushinda previous years kwa ivyo serikali inataka kujua kwanini wakati hakuna ushahidi wa kuongezeka kwa huduma zao unaoenda sambasamba na ukubwa wa funding iliyoingia ndani ya mwaka.

Kwa sababu iyo serikali inachunguza kama kuna fraud activities ambapo taasisi ime overstate it’s budget ili kujipatia hela zaidi kwa makusudi ya watu wachache wajinufaishe, au kuna money laundering, au kuchunguza source ya hizo hela kama zinatoka kwa regular funders wa kila siku.

Yote hayo ni kwenye kazi ya jeshi la polisi (serious fraud unit) kuhakikisha matumizi ya hizo hela zinaenda kutumika kulingana na budget iliyopangwa na taasisi, katiba yao na sio mambo mengine kinyume na shughuli za usajili wao au sheria za Tanzania

Sababu alizotoa Sirro sio za ki IGP ni za level ya mtu kama Musiba petty and the explanation given is not in per with top civil servants language anatakiwa ajue kutumia diplomatic language.

YOTE HAYO ANGEYATOLEA MAELEZO LEO YANGEHARIBU UCHUNGUZI AMBAO BADO UNAENDELEA.WEWE KAA NA DIPLOMA YAKO ACHA UCHUNGUZI UENDELEE.
 
Ina maana siku hizi donors kutuma hela kwa wadau hairuusiwi tena kwan mboga mboga mnaogopa nini
Sheria ya utakatishaji wa pesa inalazimisha uchunguzi ufanyike kabla kuruhusu kutumika hizo pesa. Uchunguzi kama huo ni kawaida ila haitangazwi.
 
Uonevu usio na maana
Hawaichukui wanataka wajue matumizi yake ...alichokosea ni kutangaza public ila nchi zote taasisi isiyo ya kiserikali ikipokea fedha za mashaka wanafatilia hata wasipotangaza
 
Back
Top Bottom