IGP Sirro: Tunakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu baada ya kupokea fedha nyingi takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje

IGP Sirro: Tunakichunguza Kituo cha Kutetea Haki za Binadamu baada ya kupokea fedha nyingi takriban Tsh. bilioni 6 kutoka nje

Haki za binadamu siyo kipaumbele cha serikali za Kiafrika.
Africa hamnaga haki, haki ni siku ukifa - Geneza lako pale unasikia - Katangulia mbele ya HAKI.

Ukiwa duniani hasa Africa - Haki yako ipo kaburini.
 
Chadema hizi pesa walitakiwa waziingize hata mwaka jana au wangeangalia Taasisi nyingine kuliko kumtumia huyu Ole Ngurumwa ambaye anajulikana yuko upande gani.
Kuliko saiz hizi pesa kuziingiza zote mwaka huu.!
Tukisema intel yenu iko very weak mnapiga kelele sasa mko under watchdog sijui kama mtavusha ata mia, Muda ni mwalimu tunawasubiri mpitishe bakuli
 
Ina maana siku hizi donors kutuma hela kwa wadau hairuusiwi tena kwan mboga mboga mnaogopa nini
Mkuu njia za magaidi ni nyingi. Unaweza kuta hizo ni hela za kuvuruga amani. Tena wakomae nao kabisa.
 
Nchi zingine wanakaribisha fedha kama hizo kama uwekezaji,mradi tu taratibu wezeshi ziingie kihalali na kukaguliwa zinafanya nini zikishaingia.Hapa kwetu muda siyo mrefu ukiwa na fedha Benki zinaweza kuchukuliwa na mamlaka kwa visingizio visivyo na mashiko. Tunapopambana na adui umaskini huku tunakataa raslimali ikiwemo misaada ya Diaspora au uraia wa nchi mbil(Duo-Citizenship),yote hiyo ni kuwafungia wasomi na watu wajanja ili wasije kuwafumbua Watanzania macho kuhusu Dunia inavyoendeshwa kisayansi huku tukihakikisha wananchi wanabaki gizani.Ujinga ni mtaji wa CCM na Umaskini wetu ni silaha ya kujilinda na Ujinga ndiyo Jela ya Watanzania.
Hii Nchi ni Yetu sote,Kituo cha Haki za Binadamu kinahitaji fedha za Uendeshaji,Serikali inayojitambua ingekipatia fedha ila hapa kwetu ni kinyume chake.Wakipata fedha toka kwa Wasamaria wema pia inakuwa nongwa?Kazi ya Kutetea Haki za Binadamu haisadii Serikali ya CCM?Nani hasa anayevunja Haki za Binadamu?Serikali haiwezi kuweka namna ya kufanya ukaguzi wa mapato/matumizi ya NGO's zinazofanya kazi nchini?Sheria zilizoanzisha hizo NGO inasemaje?Taratibu,Sheria na Kanuni zilizoanzisha hizi taasisi zinaruhusu Disputes zake kuwekwa Public kwa jinsi hiyo hata kabla ya Uchunguzi?Hapo wanataka kusema wameshatoa hint kwa wachunguzi/wapelelezi kuwa ni aina gani ya matokeo ya uchunguzi yanatarajiwa na watawala.Hawawezi kuja na hoja zitakazoonyesha kuwa IGP alikurupuka kuutangazia umma jambo ambalo hajalifanyia utaifiti wa kutosha.
Sifahamu aina hii ya Uongozi inayotumika na huyu Kamanda na Watawala wetu inaitwaje?Democratic,Autocratic,Buerocratic,Laizer's Fare or Dictatorship type of Admistration?
Hio IGP ku announce Public ni Wake up call kuwa Ivi NGO vyote viwe aware visije kutumika Kuvusha mpunga kiholela haswa kipindi hichi kuelekea uchaguzi hizo inshu zipo sana na hazikuwa kuwa announced publicly
 
Ukimaliza huo uchunguzi utakuta hizo fedha zote hazipo. Dawa kuzifungia kwanza ukimaliza uchunguzi kama ni halali unaziachia. Kama zina walakini unazihold mpaka waseme Meeee kama mbuzi
Mnahold kwa vigezo vya kuwashukia kutakatisha fedha?Je,kituo hicho kilisajiliwa baada ya kuzingatia sheria,vyanzo vyao vya mapato viliwekwa wazi?Taasisi hii ina umri gani sasa?Fedha walizopokea ni mara yao ya kwanza?
 
Mnahold kwa vigezo vya kuwashukia kutakatisha fedha?Je,kituo hicho kilisajiliwa baada ya kuzingatia sheria,vyanzo vyao vya mapato viliwekwa wazi?Taasisi hii ina umri gani sasa?Fedha walizopokea ni mara yao ya kwanza?
Hayo Maswali yako yote nadhani ndo polisi wanataka kuyajua
 
Lisu ni gaidi
Una ushahidi wa hiyo tuhuma?Unaweza kuisaidia nchi endapo utawasilisha ushahidi wa hilo.Unapokaa kimya au kuleta taarifa JF badala ya vyombo vya kusimamia sheria unastahili kushtakiwa kwa kuficha ushahidi kwa kukusudia,wewe utakuwa msaliti.Yakitokea mashamulizi ya kigaidi nafsi yako itakuwa huru?
 
Kwa nini unataka IGP atoe maelezo kwa namna unayotaka wewe wakati kosa lililotendwa na taasisi ni la kisheria? Sheria ya udhibiti wa fedha za wafadhiri kwa NGO's/vyama vya siasa, imetungwa na bunge na kazi ya polisi ni kusimamia utekelezaji wa sheria.
Inabidi ukaisikilize interview yenyewe aliyofanya BBC ili uelewe perspective yangu.

Sioni tatizo la polisi kufanya walichofanya. Tatizo Sirro alikuwa too specific on one area without evidence.

Kuna wakati aliulizwa mbona taasisi yenyewe shughuli zake zipo wazi za kutetea haki za binadamu akaanza kujiuma uma na majibu ya kujibalaguza uwezi jua sijui usiamini watu etc with things which don’t up.

Unapokuwa unafanya investigation hasa za hela mambo kama hayo yanataka generic approach of concerns kulingana na sheria to justify why police investigation is lawful.

Sio kung’ang’ania sehemu moja tu ‘ugaidi’ kama ilivyokuwa kwa IGP matokeo yake alikuwa ana struggle kujibu maswali.
 
Hawa Polisi wakikwambia 10 usishike hata moja. Ndiyo hawa hawa wanabambikia kesi FAKE Watanzania wengi wasio na hatia hivyo hata huu ushahidi wao pia unaweza kuwa ni FAKE. Kumbukeni kesi chungu nzima FAKE walizobambikiwa Watanzania mbali mbali ikiwemo yule Kabendera na kusababisha kifo cha mama yake mzazi.

johnthebaptist,
Na ndio haohao tuliowapongeza baada ya kuonyesha weled wakat wa kumsindikiza lisu akitafuta wadhamin
 
Hivi taasisi kama hivyo bil 6 ni fedha nyingi? Mmepitia proposal zao kujua hivyo bil 6 waliomba kwa mchanganuo gani? Onesmo ni mtetezi wa haki za Binadmu kweli,polisi acheni kutumika na wanasiasa.
kwanza wakuu ingekua vizuri mwenye kujua atujuze kwamaba hasa kipindi kama hichi tunapoelekea uchaguzi ni yapi huwa ni majukum ya taasisi kama izi ingetusaidia kupata mwanga
 
Ina maana siku hizi donors kutuma hela kwa wadau hairuusiwi tena kwan mboga mboga mnaogopa nini
Labda hao wanaotetewa wamelalamika fedha zao kutowafikia?
Ndio maana Jeshi la Polisi na vyombo vingine wanataka kujilidhisha kuhusu miamala ya hizo 6Bil.
 
Baada ya hizi pesa kupigwa pin, naona chadema wehairisha ziara zao za kutafuta udhamini mkoa wa songea.
Naunganisha tu dots
mkuu sikia chadema mpaka sasa wakitaka bil 20 ndani ya siku tano kwa kuchangiwa na wananchi wanapata mkuu, ni swala la wao kutangaza tu basi , so hawawezi kukosa pesa na hata hivyo wamejipanga mda mrefu na sio ajabu yanayotokea leo waliyajua hata miaka miwili kabla,
 
mkuu sikia chadema mpaka sasa wakitaka bil 20 ndani ya siku tano kwa kuchangiwa na wananchi wanapata mkuu, ni swala la wao kutangaza tu basi , so hawawezi kukosa pesa na hata hivyo wamejipanga mda mrefu na sio ajabu yanayotokea leo waliyajua hata miaka miwili kabla,
Sawa kabisa mkuu. Yeye anadhani wana-CHADEMA na viongozi wao ni vilaza. They know Precise Planning (PP).
 
Back
Top Bottom