IGP Sirro: Ukiwa na mtoto mhalifu halafu usitoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama wewe ni tatizo kwa Watanzania

IGP Sirro: Ukiwa na mtoto mhalifu halafu usitoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama wewe ni tatizo kwa Watanzania

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
"Huwa nawaambia siku zote, usicheze na mtu wa hovyo hovyo, usimwamini kila mtu. Walipomuona huyu mtu wa hovyo hovyo Hamza anawasogelea, walijua ni Mtanzania wa kawaida, kumbe alikuwa na pistol na akafanya alichofanya."- IGP Simon Sirro katika ibada ya kuaga miili ya askari wanne

=========

IGP Sirro

Watanzania wenzengu, Kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya Jeshi la Polisi niwape pole sana wafiwa nawapa pole sana waombolezaji hili tukio ni kweli ni kubwa lakini ndio kazi yetu sisi askari, lakini tukio kama hili linapotokea sisi Askari tuna kitu cha kujifunza, wananchi wana kitu cha kujifunza lakini pia wafiwa wana kitu cha kujifunza.

Watanzania wenzangu ukishakuwa na mtoto mhalifu, ukishakuwa na mtoto mwizi. ukishakuwa na mtoto gaidi, ukishakuwa na mtoto mwenye tabia mbayambaya, usiposhirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, maana yake kuna namna mbili Moja kubwa anaweza akaleta madhara kwa watanzia lakini pia anaweza akapoteza uhai wake yeye mwenyewe.

Sasa huyu Hamza aliyofanya kama ndugu zake wangewajibika vizuri leo tusingekuwa hapa sasa. Lakini watanzania wenzangu waele siku zote askari polisi na vyombo vingine vya usalama vipo kwa ajili ya kulinda Watanzania na ndio maana tumeapa kufa kwetu kwa risasi tumeapa kwa Amiri jeshi Mkuu hatuoni tabu juu ya hilo lakini watanzania wajue kuwa na sisis tuna familia zetu.

Kwa hiyo kuna kitu cha kujifunza kwamba ukishakuwa kwenye familia yako kuna mhalifu ujue wewe ni tatizo kwa Watanzania tulitegemea Watanzania wazae mtoto aje kuwa Waziri aje kuwa IGP aje kuwa Mwalimu, lakini ukizaa mtoto akawa mwizi akawa kaluwanja ni tatizo kwa Watanzania.

Lakini kwa wafiwa kuna kitu cha kujifunza, Askari wetu hawa hawakuwa gaidi, hawakuwa wezi, hawakuwa majambazi wamekufa wakiwa wanatetea watanzania hivyo kifo chao ni kwa heshima ya Watanzania wamekufa wakiwa wanalinda Watanzania kwa hiyo tusapate huzuni sana tuwaombee, tusipate huzuni sana kwa sababu walikuwa wanalinda Watanzania.

Lakini kwa Poliai ofsa na sisi viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama kuna kitu cha kujifunza kwa askari wetu hawa kufa kwa risasi kwa kupigwa na risasi kichwani. Siku zote huwa wanawaambia usicheze na mtu wa ovyo ovyo, usimwamini kila mtu hii yote ni kwa sababu ya imani, walipomuona huyu mtu wa ovyo ovyo Hamza anakuja walijua ni Mtanzania wa kawaida anakuja lakini kumbe alikuwa na pisto na akafanya alichofanya.

Lakini tumejifunza ukizubaa usilaumu jeshi, ukizubaa usilaumu serikali, askari mna mafunzo ya kutosha ni Hightime, tuna challange, tuna changamoto si kila mtu ni rafiki lakini niseme kwamba kama jeshi tumepoteza vijana wadogo sana sis ambao tunakaribia kustaafu tunaamini hawa ndio wangeendesha jeshi lakini kwa sababu ni sehemu ya maisha yetu askari ninaamini wale mnaobaki mnajifunza sasa si kila mtu anapenda Askari polisi, si kila mtu anapenda vyombo vya dola.

Wakati mwingine tunaambiwa tunatumia nguvu kubwa sana sio au hatutendi haki sio? Lakini yanapotekea hapa hatusikii mtu anasema habari ya haki ya polisi maana yake nini msiwe na Double Standard. Kazi hii ni ngumu sana mtu akiiona hivi anajua ni kitu rahisirahisi tu lakini kudeal na mhalifu sio jambo dogo!.

Sisi tuwaombee sana waliotangulia na sisi tuko nyuma yao tunafata. Na ninyi mliofiwa si kwamba mmefiwa peke yenu na sisi ni ssehemu ya tatizo pia kwa sababu vijana wetu wametangulia na kijana wetu wa SGA najua kazi yetu ni moja ndio maana huwa nasema sisis ambao tuvaa buti kazi yetu ni moja. Mhalifu anapotuoona hajui huyu ni wa kampuni binafsi anajua kazi yetu ni moja ni ya kulinda maani, na ndio maana huwa nasema acheni kubaguana sijui huyu ni wa kampuni ya ulinzi hapana kazi yetu ni moja kwa hiyo tuheshimiane.

Lakini wafiwa niseme tutajitahidi kwamba vijana wetu hawa wanapata haki zao, kama wana familia zao tutajitahidi kulingana ya kanuni zetu kuhakikisha wanapata haki zao niwashukuru sana asanteni sana.
 
"Huwa nawaambia siku zote, usicheze na mtu wa hovyo hovyo, usimwamini kila mtu. Walipomuona huyu mtu wa hovyo hovyo Hamza anawasogelea, walijua ni Mtanzania wa kawaida, kumbe alikuwa na pistol na akafanya alichofanya."- IGP Simon Sirro katika ibada ya kuaga miili ya askari wanne https://t.co/wboL2HHZVt
Ameshahukumu kabla ya ripoti ya uchunguzi
 
8860003675.jpg
 
Kwa muonekano wa yule gaidi askari walifanya makosa kumuamini
Well trained askali and equiped asingeweza pigwa risasi, askali wetu wako na mazoea mabaya. Wengi ffu ni form four pass mark, unamupeleka Police hata reasoning ya mazingira ya kazi kama alishindwa shule uko, sawa atamaliza kozi atapangiwa kituo Cha kazi yanarudi yale yale ya form four division four.
 
Alijua yupo kikosini kumbe kuna raia
 
Ifike mahali Viongozi wetu wajue askari Wana ndugu na wanafamilia pia, IGP anapotamka mbele ya familia za wafiwa kwamba askari waliofariki walikuwa wazembe kuruhusu watu wa hovyo kuwasogelea nikuweka kovu miyoyoni mwa wazazi wa vijana hao.

Mtu mwenye silaha haitaji kukusogelea kukuua na hakuna Askari mwenye macho yakuscan silaha.

Lakini pia huyu mtu wa hovyo alikuwa anakula meza moja na viongozi wa nchi hii na hakina sehemu intelligence ya IGP na nchi imewahi kuwataadharisha wakae mbali naye, ameshiriki kampeni za Urais last year kwa mujibu wa clips zinazosambaa...huyu mtu wa hovyo utamjuaje kwa macho?

Nadhani Mzee Siro aina ya jeshi unalowaza lilishapitwa na wakati, wape moyo askari na wekeza kutengeneza jeshi lililojisimika kwa wananchi ili wananchi wakusaidie kupata taarifa. Hakuna jeshi linalojenga uadui na wananchi likafanikiwa, wananchi ndio jamii na Wana macho kila kona. Usiwaite jamii watu wa hovyo Wala usione Kama askari waliouwawa walikuwa wazembe
 
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro wakati akitoa salamu za jeshi la polisi kwenye msiba wa polisi waliouawa na jamaa aliyejulikana kwa jina la Hamza , ametoa wito kwa jamii kuwa makini na watoto wao kwani kama ikitokea ukawa na mtoto gaidi na anayefanya mambo ya hovyo hovyo kama aliyokuwa anafanya Hamza andika maumivu kwani vyombo vya usalama vikimpata hatabaki salama.

 
Back
Top Bottom