IGP Sirro: Ukiwa na mtoto mhalifu halafu usitoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama wewe ni tatizo kwa Watanzania

IGP Sirro: Ukiwa na mtoto mhalifu halafu usitoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama wewe ni tatizo kwa Watanzania

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro wakati akitoa salamu za jeshi la polisi kwenye msiba wa polisi waliouawa na jamaa aliyejulikana kwa jina la Hamza , ametoa wito kwa jamii kuwa makini na watoto wao kwani kama ikitokea ukawa na mtoto gaidi na anayefanya mambo ya hovyo hovyo kama aliyokuwa anafanya Hamza andika maumivu kwani vyombo vya usalama vikimpata hatabaki salama.


Dah! One day Tukutane mbinguni kwenye haki ya kweli, huku haki haipo
 
Hatoshi.

Keshamuhukumu ni Gaidi, halafu watanzania mtegemee taarifa ya kina na ya kitaalamu ya uchunguzi wa hili tukio kutoka kwa Jeshi la Polisi Tanzania.

Poleni.
Nafikiri wabongo wengi mnamihemko sana. Mnapenda kushangilia vitu ambavyo havina maana kabisa na ni hatari vikiendelezwa.

Issue ni hivi. Assume ni kweli kuwa Hamza alinyanganywa dhahabu yake. Je, ndio uanze kuchukua hatua mkononi ya kuwaua kila askari na hata ambao hawana hatia?

Je, nchi ikiruhusu ujinga huo wa Hamza alioufanya tutaishi salama,?Nchi hii IPO kisheria zaidi. Kama MTU amekukosea kwanini uanze kuchukua hatua kali za kuua?

Hii ni kama kwenye soka. Unachokozwa unareact unatolewa nje. Hamza anaingia kwenye ugaidi kwa style yake ya kushambulia watu kwenye nchi ya kisheria. Kama tukiruhusu ujinga huo mnao ushadadia utamalaki. Hata nyie au ndugu zenu hawawezi kuwa salama.

Aidha kwanini pia alikuwa anapeleka kuuza madini kwa njia za panya.? Angefungua kesi ,angefuatilia ,kama ni kweli ametendewa mnachoongea.Basi wrote wanaohusika wangechukuliwa hatua.
 
Mbona kama Vile ametangaza vita?

ni mwendo wa kuliana timing saivi au?

au mwandishi ndio kaiwasilisha vibaya?
IMG_20210827_205957.jpg
 
Mbona kama kapanic inaonesha wazi ni kweli marehemu Hamza alikuwa na matatizo yake na polisi hakuwa na issue za ugaidi, na kibaya kawadhalilisha kweli polisi yani mtu kasimama tu katikati ya barabara ila polisi walikuwa wanapiga risasi pembeni sasa angekuwa gaidi kweli na angetaka kuwadhuru raia hali ingekuaje pale?
 
Kauli hii, endapo itadababisha polisi kuingiza gia ya mauaji "Killing Spree", ICC inamhusu huyu kamanda.

Sina hakika alichomaanisha huyu kamanda wetu, lakini inaweza kuwa ni kuwatia hamasa askari waue raia bila kufuata taratibu za kisheria zinazotambulika.

Tuombe heri, labda Sirro, siku zijazo atalazimika kukemea mauaji yatlnayotarajiwa kuendeshwa kwa maagizo yake. Tuombe Uzima.
 
Nimefatilia taarifa ya UTV walienda hadi kwenye migodi yake miwili ya chunya ,pia Hamza ile picha inayomuonyesha kwenye jiwe la chama cha mapinduzi ni ofisi aliyoijenga yeye mwenyewe na alizindua 20-12-2020.

Hamza alikuwa Uvccm kindakindaki.
 
Kauli ya hatari sana kutoka kwa sirro ,kwahiyo raia wasio nadhifu pindi wakiwa karibu na polisi wadhibitiwe? Vipi wenye nia ovu wakiwa smart)nadhifu) aka sio wa hovyo hovyo?
 
Kauli hiyo kwa sisi wataalamu wa kiintelijensia maana yake ni kuwa hao Maaskari wakufa kizembe.
 
Mbona kama kapanic inaonesha wazi ni kweli marehemu Hamza alikuwa na matatizo yake na polisi hakuwa na issue za ugaidi, na kibaya kawadhalilisha kweli polisi yani mtu kasimama tu katikati ya barabara ila polisi walikuwa wanapiga risasi pembeni sasa angekuwa gaidi kweli na angetaka kuwadhuru raia hali ingekuaje pale?
Nenda ukasimame na wewe wapige pembeni
 
Back
Top Bottom