DOKEZO IGP tuokoe na wizi ulioibuka Arusha unatisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Serikali iongeze watu katika ajira za Polisi. Polisi waliopo hawatoshi nchi hii, waongezwe kadhaa kwa kila kata na walipwe vizuri

Pia serikali ijitahidi kutengeneza mazingira ya ajira kwa vijana

Fikiria kama hizi bodaboda na Bajaji zisingekuwepo, je hawa Madogo wanaofeli form four kila mwaka wangefanya nini?
 
Nahisi pia machinga wamegeukia wizi
 
Kuzaa bila mpangilio na malezi ya hovyo ndo vinaleta wizi,

Unakuta kijana wa miaka 14 hasomi kashatoka nyumbani unategemea afanye kazi gani?

Tuzaeni watoto tunaoweza kuwalea.
 
Hamna kitu hao ni porojo tu !! Na ivyo vijambazi vyao ni stimu za bangi tu mirungi hata miili havina vimekauka kwa kuvaa mashati oversize.
Naskia hawa ni tofauti na panya. Wanachofanya wanakuvizia huna hili wala lile na hakuna watu karibu wanakuchoma na sijui spoku au bisibisi wanaiba wanakimbia na boda.

Arusha watu ni wakorofi, bila kuviziana wanakuua wale. Kuna siku Nipo huko maeneo ya sakina kuna mama alichomwa na spoku akamshika mmoja, pamoja na spoku zote ila uyo mmoja hakumuachia mpaka watu wakafika, wawili wakakimbia na boda yao. Aisee yule aishukuru defender ya polisi, alipoiona tu alipata nguvu aliikimbilia akaingia huko ndani na kelele za niokoe za kutosha.
 
Hawa wezi wa tatu mzuka ni hatari mnooo . Wao kazi Yao ni kuvizia watu
 
Arusha ipi unayokaa wewe ? Matukio haya ya ujambazi yamekifthiri kila mahali . Watu wamepoteza ndugu zao pamoja na wengine kujeruhiwa alafu unakuja kuongea mashudu humu ndani . Kama hujapata athari ya haya yanayoendelea ni bora ukakaa kimya mzee
Njiro,. Sijasikia..

Nilisikiaga moja mwaka jana, hapo Tanesco 3 mzuka waliibia wanafunzi sijui.
 
Happy police wakae pembeni njemba zitoke japo monduli kimya kimya zije kunja hao machali wanao zingua A.R hatutaki uhalifu Ni place ya peace and love
 
Arusha yakianzaga haya mambo huwa ni balaa. Huo mji una majambazi professional. Miaka ya karibuni kulipoa ila kama wameanza tena inabidi jeshi la polisi lichukue hatua za makusudi. Matajiri wengi wa Arusha huwa wanaishi kwa wasiwasi.
 
Uzunguni wanavizia watu wa jogging, Kuna jamaa wa CRDB zimepita Kama wiki tatu au mwezi hivi walimnyang'anya simu na headphones.

Sio kwa ubaya lakini Warangi ndio vinara. Wanazaa sana na malezi mabovu + umaskini

Malaya wengi makao mapya wanashirikiana na vibaka kuwaibia wateja hasa wakuja na kuondoka.
 
Arusha yakianzaga haya mambo huwa ni balaa. Huo mji una majambazi professional. Miaka ya karibuni kulipoa ila kama wameanza tena inabidi jeshi la polisi lichukue hatua za makusudi. Matajiri wengi wa Arusha huwa wanaishi kwa wasiwasi.
Wamerudi kweli , kiota Chao ni night spots za makao mapya. Ukiwa na Hela Arusha ni Bora kwenda kuspend time sehemu Kama Gran Melia, Sawa Sawa village, Aces Lounge nk
 
Mara ngapi tunasema ndugu zetu wamevamiwa na panyaroad angalia comments za wenzio wa huko kwenu uone dharau zao za kishamba.
Kuna tofauti kati ya Panya road na hawa wezi wa Arusha. Panya road ni watoto ambao wanaishi mitaani na wanafahamika kabisa ila kwa upumbavu wa watu wa Dar wanafichiana siri. Utakuta kitoto cha miaka 13 kinasumbua mtaa mzima halafu watu wazima wa mtaani kwao wanamtazama tu. Hao wa Arusha wengi wao kuwafahamu ni hadi upelelezi.
 
Tanzania ufala mwingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…