IGP Wambura awaonya vikali wanaotaka kuandamana, asema huo ni uhaini akitaka "Wakome" na Wasitishe matamshi yao ya Kichochezi...

IGP Wambura awaonya vikali wanaotaka kuandamana, asema huo ni uhaini akitaka "Wakome" na Wasitishe matamshi yao ya Kichochezi...

Kuiangusha serikali kamwe siyo uhaini, asitake ku generalise mambo hapa.
Namna inayoweza kutumika kuiangusha serikali nje ya utaratibu wa kikatiba, hiyo ndiyo inaweza ikawa uhaini.
Kuiangusha serikali kabla ya muda wake ni jambo ambalo limewekewa utaratibu ndani ya Katiba. Kama Katiba imeuona umuhimu wa kuwepo na utaratibu wa aina hiyo wa kuiangusha serikali kabla ya muda wake, maana yake ni dhahiri ilitoa nguvu hiyo ili kuihami nchi pale serikali itakapoonekana kufanya sivyo na kuhatarisha maslahi ya nchi n.k, hapa serikali imenasa.
Zaidi, wenzake wala walikua hawa maanishi ingawa kuna kitu walikilenga na amemeza ndoano utamu sana, maana ameshawapa point.

Faida ninayoiona kwenye press yake hii ni kwamba wamezidi kuliongezea uzito swala hili na kulipa mile age na kuifanya nchi izidi kuchangamka, maana hao anao waambia wakome lazima watamjibu tu na wana maneno ya kukera kuliko hili la kuwaambia 'wakome'.
Akae kwa kutulia, majibu yake yanakuja.
 
#HABARI Jeshi la Polisi Tanzania, limetoa onyo kali watu wanaotangaza mpango wa kuiangusha serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais @samia_suluhu_hassan akibainisha kuwa huu ni uhaini na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura ameeleza kuwa taarifa hiyo imekuwa ikisambaa tanga jana Agosti 10, 2023 kwenye mitandao ya kijamii ikihusu kundi la watu ambao wameeleza kwamba wanaandaa maandamano ya nchi nzima ili kuiangusha serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya sita kabla ya mwaka 2025 huku hoja inayotajwa ikihusu masuala ya bandari.

IGP ametaka wananchi kuzipuuza taarifa hizo.

Maandamano
Sources Via East Africa
hivi leo ni jumapili au jumanne?
 
nyie jitieni kichwa ngumu tu mtachakaaa mtapigwa halafu mkishapata maulemavu hakuan hata kiongozi mmoja anakuja kukuangalia hata kukuetea hela ya kula wakati unasota hospitali kwagarama zako mwenyewe mjitambue kila mtu anatafuta ugali wake hakuna cha mbowe wala lissu anayetaka kupata madaraka agawane na nyie mnaojifanya kuandamana mtakoma
 
Mkuu IGP sir.
Najua unapitiamo humu kuokota mawili matatu.

Hoja ya Bandari ninakubaliana nawe ijibiwe kwa hoja. Lakini kuna tatizo.

Tatizo ninaloliona ni kuwa wanaohoji uhalali wa mkataba wa Bandari wanajibiwa na meno ya polisi. Wanashughulikiwa na kuswekwa rumande bila kesi za maana.

Nashauri
Polisi ijikite kuimarisha ulinzi na usalama wetu sisi raia wakiwemo viongozi

Polisi muache kutumikia siasa kama ilivyo sasa

Polisi muanze kutufundisha sisi raia somo la.uzalendo kwa vitendo

Mimi sijaichoka amani
Mimi sijaichoka Tanzania
Viongozi wameonesha kuichoka amani na nchi yetu kwa jumla
 
viongozi wa upinzani ndiyo wameichoka amani wewe kiongozi mzima na akili zako utawaambiaje watu wakaandamane badala ya kutoamhoja kusubiri ujibiwe mikutanoi si mnafanya? maandamano ya nini kila mtu ajuwe la kuambiwa changanya na zako yatakayo kukuta ni wewe na familia yako ndiyo itateseka wenzio wanakunywa mvinyo wewe huna mguu
 
Kiongozi anayesigina haki, taratibu, sheria na katiba ndiye hupelekea hayo yote kutokea
 
Back
Top Bottom