Iipofika topic ya Kinjekitile tulimcheka sana na kumuona mshamba lakini hatukujua hata sisi tulikuwa tushapakwa dawa na kuambia risasi zitageuka maji

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Manipulation:
Ni jinsi gani unaweza kumshawishi mwanadamu mwenzako?, its simple, mfanye akuamini zaidi ya nafsi yake, mfanye aamini ya kufikirika yana special connection na wewe.

Confusion:
Tulimshangaa sana ngwale lakini kuna upande mwingine ulituambia alifanya ushujaa ili ashawishi vijana, lakini pia upande mwingine ulituambia alifanya vijana wakabwateka kupigana bila ya tactics na plan.

One finger facing me, Three Facing you:
All in all kwa maana dawa haikufanya kazi, basi tukaja na conclusion ya kuuona kuwa mwamba alifanya utapeli, lakini tukasahau kuwa hata sisi tunaishi katika utapeli na la kushangaza tunaouona una ukuu zaidi ya ule wa ngwale.

We are the victims:
Unaambiwa uvae mabomu uende ukajiue na kuua watu fulani then Mungu atakupokea. Unapangiwa viwango vya sadaka kutoa ili kukuhamasisha kupata muujiza mkubwa. Unaambiwa utoe michango huko kwenye jumuia ili ujiapatie njia rahisi ya kubarikiwa kwenye harusi na kubarikiwa siku ya kuondoka.

Sasa sisi na vijana wa kinjekitile tuna utofauti gani?
 
Hii inaonyesha kuwa mwanaadamu anaimani ndani yake, hata hao wanaojifanya hawaamini chochote, lakini kiuhalisia yapo wanayoyaamini ambayo hayana ufafanuzi wa moja kwa moja.

Sasa kuwa na imani fulani sio tatizo, tatizo ni kuwa na imani lisilokuwa la kweli( imani potofu).
Ila imani ni kitu kipo ndani yetu.
 
Hii inaonyesha kuwa mwanaadamu anaimani ndani yake, hata hao wanaojifanya hawaamini chochote, lakini kiuhalisia yapo wanayoyaamini ambayo hayana ufafanuzi wa moja kwa moja.

Sasa kuwa na imani fulani sio tatizo, tatizo ni kuwa na imani lisilokuwa la kweli( imqni potofu).
Ila imani ni kitu kipo ndani yetu.
Hakika, na imani ndani yetu naamini ndio genuine tatizo imani zetu za ndani zimekuwa kutapelishwa na imani binafsi za wengi .

Kinachobakia ni kunungunika, kubaguana , kujichukia , lakini kumbe tunaahangaika na imani za watu
 
Hii inaonyesha kuwa mwanaadamu anaimani ndani yake, hata hao wanaojifanya hawaamini chochote, lakini kiuhalisia yapo wanayoyaamini ambayo hayana ufafanuzi wa moja kwa moja.

Sasa kuwa na imani fulani sio tatizo, tatizo ni kuwa na imani lisilokuwa la kweli( imqni potofu).
Ila imani ni kitu kipo ndani yetu.
Imani potofu ni ipi na imani sahihi ni ipi?
 
Usahihi wa imani au upotofu wake unategemeana na ukweli au uongo wa kile anachokiamini mtu.

Na hii ni kutokana na maana yenyewe ya imani, maana imani ipo nje ya yale mambo ambayo tunaweza kuyadiriki kwa milango yetu ya fahamu au akili zetu.

Hivyo imani inaweza ikawa sahihi kwangu na kuwa potofu kwa mtu mwingine.
 
Unathibitisha vipi ukwel wake ama upotofu wake wakati imani ili iwe imani haihitaji uthibitisho ?
 
Imani inahitaji ushahidi ambao utakuwa ndio kama uthibitisho wa jambo lenyewe.

Ushahidi wenye nguvu ambao humfanya anayeamini kuwa na uhakika na anachokiamini kana kwamba ameshawahi kukishuhudia.

Ni kama uhakika anaokuwa nao yule ambaye ameona moshi unafuka sehemu kwa mbaali, japo hajauona moto, ila anauhakika kuwa hapo lazima kutakuwa kuna moto kwa sababu anajua kuwa panapofuka moshi ni lazima patakuwa na moto.

Lakini anaweza mwingine akampinga na kudai kuwa huo moshi hautokani na moto, bali utakuwa umetokea tu wenyewe.

Lakini tayari umeshaona jinsi mtu wa kwanza aliyojenga hoja yake na namna inavyokubaliana na akili.

Basi hivi ndivyo imani sahihi inavyotofautiana na imani batili.
 
Yap nimekupata kwa mfano wako uwepo wa Mungu unapatana vipi na akili?
 
Jitazame wewe kama mwanaadamu uliyezaliwa na wazazi wako ukiwa kiumbe dhaifu ambaye hujiwezi kwa lolote.

Katika hali hiyo utakuwa unakubaliana na mambo mawili
1. Wewe hukujiumba mwenyewe na wala sio wewe uliyeuumba huu ulimwengu.

2.Haingii akilini kuwa wewe (na jinsi ulivyo)uwe umetokea tu, yaani hukutokana na yeyote.

Kila mwanaadamu anapita kwenye mzani huu.

Hakuna mwanaadamu anazaliwa tu na kusema kuwa kuna Mungu, wala sio hizo hoja 2 zinazomfanya mtu aconclude kuwa kuna Mungu.

Bali waliokuja na kusema kuwa wao ni wajumbe kutoka kwa Mungu( wanapokea ufunuo), ambao ni wanaadamu kama sisi, ndio wamekuja na habari kuwa kuna aliyetuumba sisi wanaadamu na ndiye aliyeumba huu ulimwengu na vilivyomo.

Sasa kwa kutumia akili kupima hoja walizokujanazo na ushahidi walionao ndio utakubali au kukataa kuwa kuna Mungu au hakuna
 
Kwa mantiki hiyo pia haiingii akilini Pia Mungu katokea tu.
 
Back
Top Bottom