Ijue Historia ya Firauni na uongo aliozushiwa

Wewe huyo Pharaoh ushawahi kumuona hadi useme babu yako?!
Evidence za mummies za mafarao ndo zinathibitisha hilo mzee, Kuna mummies kibao pale Giza tembea uone, we unaweza kunionyesha mummies ya hao unaowataja, ili twende tukapate proof maabara?
 
Tuna kazi ya kuamsha ndugu zetu hawa wamelala fofofo bila shaka!
Na bila ya ukombozi wa kiutamaduni na kujitambua, maendeleo ya kiuchumi na kijamii Africa tusahau kabisa. Lazima tujikomboe, mapigano ya kifikra lazima yaimarishwe. Mi sijui hata hawa wa utamaduni wana majukumu yapi, eti utalii.

Chinese, Indians wote wamejitambua ndo kisa cha kusonga kwao. Utumwa wa ubongoni ni mbaya zaidi kuliko mwingine wote. Wazungu wanautumia kututawala kiuchumi, kiteknolojia,kisiasa na kijamii.

Sukuma legal system ni bora sana kwa Afrika na inakisi sana uafrika wetu kuliko common law legal system, hata sijui tunashindwaje. Afrika tunauushi utumwa saana.
 
Kaka nimesoma andiko lako vizuri mno.Na nimeona mapungufu yafuatayo.

1.Hujaonyesha ushahidi wa kutosha ya kuwa ni kweli firauni hakufa katika gharika lililotokea wakati wa Musa alayhi salaam.Kwa kuwasingizia wale wenye kuamini hivyo ya kuwa wanadai tu na si wa kweli au hawana uhakika juu ya hilo.Kanuni za ujibuji wa hoja ni kuwa wewe mwenye kukanusha jambo hutangulizwa sababu unaonekana una elimu ya ziada juu ya jambo husika.Cha kusikitisha umeshindwa kulithibitisha hilo.

2. Jambo la pili ni kuhusu umri.Imekuja katika historia ya kuwa watu wa kale walikuwa wanaishi mpaka zaidi ya miaka 900,huo nimetoa mfano wa kukuzindua juu ya uhakiki wa habari za kihistoria. Kila zama zilikuwa na tabia kadiri ambavyo Mola aliye juu amepanga.Kwanza huwezi kunithibitishia ya kuwa Firauni alikufa akiwa na miaka 80.
Je unaweza kunithibitishia ya kuwa kwa umri umati za zamani mtu mwenye miaka 80 ni mzee ?

3.Unaonekana ya kuwa,kutokana na uelewa wenye imanai za dini huwa wanafata vitu kibubuswa yaani kichwa mchunga,kama una amini hivyo unakosea sana.Mathalani uma huu sisi huwa tunauita umma wa Muhammad,ni kuwa wastani wa kuishi ni miaka 70.Jua ya kuwa na umati zilizopita zilikuwa zina makadirio yao ya kuishi.Hapa nimekupa faida tu.

4.Pia kuwa na shahada,shahada ya uzamili au shahada ya uzamivu,si kipimo cha mtu kuwa na upeo wa juu kabisa wa kuhoji mambo au kung'amua mambo.Mawazo haya si sahihi.Mola wetu muadilifu sana,wapo watu hata hawajaenda huko kwenye usekula lakini wanang'amua mambo kwa upeo wa juu zaidi.
 
Hapana, ninyi nyote mko na msimamo mmoja ila njia tu nitofauti. Hajasema sisi ni akina Farao, bali Farao alikuwa mweusi na alifanya yaliyo makuu. Hapa anawaamsha weusi wajionao hawawezi kwakuwa tu ni weusi.
 
Inawezekana alikuwa mtu mwema ila hizi dini zinatudanganya! asili haibadiliki Waisrael hadi leo tabia zao ni mbovu mbovu! lazima hata mababu zao nao walikuwa hivihivi!
Kwanini huwa hamsemi vitu mkiwa na uhakika navyo.Huku mkatanguliza "mimi nadhani.." mara "Inawezekana..." mara "Nafikiri...".Matamko haya huonyesha dalili ya kukata tamaa katika kuutafuta ukweli wa jambo fulani hasa jambo hili la kielimu.Kama kitu hukijui bora kunyamaza kuliko kudhani dhani....
 
Mi nimsaidie kujibu hoja moja tu juu ya umri, kwanza mafarao si watu wakale wa kuishi miaka hiyo 900, kiimani Musa aliishi miaka kama 3500 tu iliyopita. Mke wa Ibrahimu, miaka mingi kabla ya akina Musa, alipata ujauzito wa Isiaka uzeeni, ni miaka yake ya 80s. Sijui nimelijibu.
 
Nimesikia hadithi nyingi kutoka kwa wazee mbalimbali, lakini sijapata kuisikia inayozungumzia maisha ya Misri ya kale. Natambua kuwa Waafrika hatuna fasihi andishi bali fasihi simulizi tunayo. Kukosa masimulizi ya Maisha ya Misri japo inayofanana kuna maanisha historia hiyo siyo ya kwetu, imebuniwa tu.
 
Aisee umeongea jambo kuu mno.
 
Wewe utakuwa mwarabu koko.
 
Kitabu cha dini unayoiamini kilitokea wapi? na kama hukuona kilikotokea, ni una uhakika ama unadhani? Nini maana ya Mungu kukupa Macho?
 
Historia ya Misri ni fasihi andishi, imeandikwa Kwenye mapyramid na matempo kule Giza, Mabavu hao wa kale waliangalia mbali sana na ndiyo maana waliandika, na kuchora michoro ili wenye vichwa vigumu waone picha, hivyo picha na maandishi mengi, vimetawala kwenye pyramid na temple vya misri. Ile si fasihi simulizi!
 
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji115] mbavu zangu zafwaaaa
 
Naam umenena mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…