Sasa kama tuna cha kujivunia; shida yote ya nini ya kujinasibisha na watu ambao hata asili yao hatuijui!!!
Kujinasabisha na wengine ni upuuzi ila kwamba hatuna cha kujivunia kwa maoni yangu ni upuuzi Zaidi.Nina lundo la maelezo ya maeneo tuliyofanya vizuri kuliko binadamu mwingine yeyote toka kale hata sasa.
Kipindi hicho mnachojadiliana kuhusu filauni uhuni ulikuwa mkubwa huko wengine wanakoona kuna waungwana.Arabuni,Babeli,Rumi na Israeli ya wakati huo kimbilio salama la walionewa lilikuwa Misri.Misri ipo Afrika.
Maandishi ya kwanza ya binadamu yalianzia Misri.Watalii waliomua kwenda wanapotaka kwa gharama zao kushuhudia wanayosimuliwa walikuwa waafrika,rejea ziara ya malkia wa Kushi kumtembelea mfalme wa Israel aliyeitwa Suleiman mwana wa Daudi.
Njaa ilipoikabili Israel kimbilio lao lilikuwa Misri.Misri ni Afrika.
Rejea simulizi za Walter Rodney" How Europe underdeveloped Africa",usiishie tu kusoma habari zake fuatilia sababu/kiini cha kifo chake utajua kiwango cha uwezo wa akili zetu.Huko mbali fuatilia Patrice Lumumba na nmna alivyomalizwa kikatili utajua uwezo wetu wa akili ukoje.Shida ni mamluki na kundi dogo wanaotamani kuwa watumwa milele.
Afrika hatujapungukiwa uwezo wa akili wala raslimali,tumebweteka kwa utajiri uliokithiri( najua unafuata ubishi na matusi mengi),nitatoa kielelezo.Mwajiriwa anayelipwa Tsh.1000,000/=( take home) na mfugaji wa kimasai au kisukuma mwenye ng'ombe 50 anaozurula nao mchna na usiku,jua lake na mvua yake ukikutana nao njiani utamwona nani tajiri aliyefanikiwa? wengi watamwona mopkea 1,000,000/= Kila mwezi tajiri kwa kungalia anavyokula, anavyo vaa, simu aliyo nayo, kagari kamkopo nk.Mfugaji mwenye mgolole ataonekana omba omba. Sitisha ajira mwezi mmoja tu,utajua nani tajiri kati yao.
Ndiyo tofauti yetu na hao ambao miongoni mwao wanatamani kujinasabisha nao.Wana mbwe mbwe hawana kitu Zaidi yetu ila shida zimepanua matumizi ya akili zao.Nitabaki Mwafrika na kujivunia uafrika.
Kwa mada iliyo mezani awe Filauni au Farao maadam alikuwa mtawala wa Misri na kama ngozi yake nyeusi kama yangu huyo ni sehemu yangu,makosa yake ni makosa yetu kinachonitenganisha naye ni maungamo yangu kwenye makosa aliyoyatenda.Damu ya thamani kubwa ilinitenganisha na kila uovu.
Baraka za Ibrahimu zitaambatana name kwa kuwa nilishiriki kuwatunza watumishi wa MUNGU waliofukuzwa na kukataliwa na wakwake.
Ninajua kuwa historia ya kweli Misri ni ya waafrika halisi weusi kama tulivyo.