Yaani shetani yuleyule wa miaka yote anaendelea kuwakamata viongozi wetu na kuwatumia kuharibu na kuumiza wananchi na nchi...
Angalieni, huyu mama (Rais Samia Suluhu Hassan) naye keshamvaa shetani huyo huyo na keshaingizwa mkenge na yeye mwenyewe kwa mkono wake kusaini mkataba hatari na angamizi na kampuni ya waarabu iitwayo DP World...
USHAURI:
Wandugu, haya mambo hayako kama tunavyoyaona Kwa macho ya damu na mwili huu tulionao. It's beyond that..
Hii kitu haiwezi kukoma unless nguvu kuu inayozidi ile iliyowashika viongozi na watawala wetu itachukua nafasi yake..
Ni Rahisi tu. Zingatieni haya👇👇
1. Kila mwana wa nchi hii mwenye mapenzi na nchi yake, na anayeamini kuwa yupo Mungu aliye hai aliyetupa nchi hii kuwa urithi wetu na vizazi vyetu, basi aombe kwa lugha yake ili kuruhusu mkono wa Mungu wetu aliye hai uwe juu ya nguvu hii ya uharibifu inayowatawala na kuwaongoza viongozi wetu kufanya maamuzi hatari na angamizi kwa nchi yetu..
2. Kila mwana wa nchi hii anayeamini katika nguvu na mamlaka iliyo kuu zaidi (yaani Mungu - Yehova katika Yesu Kristo) akiombee
KITI CHA U - RAIS wa nchi yetu. Katika kiti cha u - Rais wa nchi yetu ndipo ambapo chanzo (source) ya maamuzi yote ya nchi na taifa hili la Tanzania yawe mabaya au mazuri yanapotoka...
Na kwa jinsi ilivyo sasa, ni wazi kuwa nguvu ya MKUU WA MAPEPO na WACHAWI ndiye inayekimiliki na kukitawala kiti hicho. Yeyote anayekikalia hata awe msafi namna gani, hata awe na makusudi na malengo mazuri kiasi gani juu ya nchi yetu wakati anaingia, lakini mara akikaliapo kiti hicho kama nguvu hana iliyo kuu kuliko inayokitawala kiti hicho, Rais huyo lazima ata - compromise na matakwa na miongozo ya ubaya ya yule mwenye nguvu
mchawi mkuu - shetani anayekimiliki kiti hicho...
Wakati mwingine nguvu hii ya kishetani na kichawi, huchagua yenyewe mtu wa kuja kukikalia kiti hicho kuanzia ktk hatua za michakato ya uchaguzi...
Nguvu hii ndiyo inayodhibiti mifumo ya kisiasa na kiutawala ya nchi yetu ili ibaki kama ilivyo na ubovu wake pasipo kuruhusu mwanya wa mtu anayemjua Mungu na anayejua siri ya utendaji kazi wa nguvu za kipepo na kichawi zinavyofanya kazi ktk tawala za nchi kuchukua uongozi wa nchi..
Mashetani, wachawi na MAPEPO yanajua mtu wa namna hii akichukua nafasi ya kukikalia
kiti cha maamuzi katika nchi a.k.a Kiti Cha U - Rais, basi ndo itakuwa mwisho wa nguvu na utawala wao na ndiyo itakuwa ndo mwisho wa mifumo yao ya uovu kuendelea kutawala nchi...
KWA HIYO;
✍️Tatizo siyo watu. Tatizo sio Mkapa wala Kikwete wala Magufuli na wala tatizo sio Rais Samia Suluhu Hassan kwa sasa. Tatizo ni nguvu iliyo nyuma yao kusukuma maamuzi yao ambayo huleta athari hasi katika nchi..
✍️Kwa kuwa akili na ufahamu wao halisi unakuwa umedhibitiwa na nguvu za kipepo na kichawi, obvious wao huwa hawaoni ubaya wa maamuzi yao. Wao huona wamefanya kwa wanachokiita "uzalendo wa nchi yao", lakini ukweli ukiwa kinyume chake. Huja kugundua kuwa wamefanya maamuzi ya hovyo baadaye wakiwa hawapo kwenye position zao..
✍️Kwa hiyo, tukitaka kumshinda adui huyu asiyeonekana kwa macho ya mwili na tukitaka kuikoa nchi yetu, basi hatupaswi kufanya vita kwa jinsi mwili na damu. Badala yake vita viwe vya kiroho kama ilivyoandikwa;
2 Kor 10:3-6 SUV
"......Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome😉 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia..."
✍️Pia silaha zetu za kutumia katika vita hii si hizi tunazohimizwa na kina Mwabukusi na kina Dr Wilbroad Slaa (physical congratulation) kama vile kuandamana, migomo nk . Bali silaha zetu za kumwangamiza kabisa na kumtiisha adui huyu zimeanishwa very clearly na Mungu mwenyewe katika Neno lake..
Wefeso 6:11-14, 16-18 SUV
".......Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;...."
Walio upande wangu na kuijua elimu hii wamenielewa vizuri sana..
Namtakia kila mtu kila la kheri ktk kuchukua hatua..