Ladha ya mijadala ni kutanua wigo wa kujadili ili kuogezeana maarifa, sasa inapokuja mtu anadadisi au anaongezea kitu ambacho hakimpendezi mwingine kwa kuwa yeye hataki iwe vile ilishakuwa ndiyo shida huanzia hapo.
Mfano, binafsi sikumbishia mleta mada, nikaenda mbele zaidi kuwa siyo China tu, hata Afrika ya sasa inajengeka kuliko maeneo mengi ya Ulaya na Marekani, ila kabla ya ku diss miondo mbinu ya wale, wengine tujiulize, je, SERA na Sheria zinasemaje?
Pia tuelewe, kuna wale walishajenga na hata sasa haiwapi shida kwanini waanze kujenga tena badala ya kufanya mengine?
Kingine kuna nchi zenyewe zinataka kusambaza watu katika maeneo mengi zaidi ya nchi zao kwa kuwa yapo empty, wakati nchi nyingine watu wake wanafurika mijini, hapo lazima ujenge maghorofa marefu kwa ajili ya makaazi na ofisi. Kuna factors nyingi tu. Pia kuna cultural issue.
Unaweza ukaleta hoja kama hii, lakini mwingine akaikataa kwa sababu inakwamishabkile alichokusudia. Hapo tunakuwa tunaufinya mjadala.