Ikijulikana mahakama ilidanganya kuhusu CDF itaaminika tena?

Ikijulikana mahakama ilidanganya kuhusu CDF itaaminika tena?

Hajawaita wamtetee, amewaita wadhibitishe uhani wake kutokana na nafasi zao kikatiba. Ama unadhani ni utetezi wa hivyo unavyodhani?
Wale ni mashahidi wa utetezi atawaongoza kumtetea wanaotakiwa kuthibitisha uhaini wake ni mashahidi wa jamhuri na washapita hivyo wakienda kinyume na hilo wakamgeuka ndio itambidi yeye awafanyie cross examination
 
hao wote DCI, IGP na CDF hawaji mahakamani kumtetea lisu na wote tunalijua hili, lakini technically wanakuja kumtetea Lissu

yaani ni kwamba Lissu atawaongoza huku amewatight kwahiyo watakubali kiaina
 
Wale ni mashahidi wa utetezi atawaongoza kumtetea wanaotakiwa kuthibitisha uhaini wake ni mashahidi wa jamhuri na washapita hivyo wakienda kinyume na hilo wakamgeuka ndio itambidi yeye awafanyie cross examination
Akishaweka kwenye kona unategemea hao mawakili wa jamuhuri wawahoji kuhusu miamala yao ya bank kama Heche?
 
Mahakama itaaminika kwa kusema ukweli, sio kushurutishwa kuiamini.
Siku Mahakama ikisema ukweli mtaiamini?
Kilichoko ni kama alivyosema Lissu kwamba majaji ni CCM so ht wafanyeje hamtoiamini hiyo mahakama
 
Siku Mahakama ikisema ukweli mtaiamini?
Kilichoko ni kama alivyosema Lissu kwamba majaji ni CCM so ht wafanyeje hamtoiamini hiyo mahakama
Ukweli ni ukweli, wathibitishe kwa nyaraka kuwa hao watu walikuwa nje ya nchi. Hatuamini sanamu sisi, bali kwa udhibitisho.
 
Siku Mahakama ikisema ukweli mtaiamini?
Kilichoko ni kama alivyosema Lissu kwamba majaji ni CCM so ht wafanyeje hamtoiamini hiyo mahakama
Hivi wewe unaweza kuiamini mahakama inayo sikiliza kesi mwaka mzima ya uhaini wa mtu Mmoja?. Yani kwamba mtu Mmoja anaweza kupindua serikali.
 
Hivi wewe unaweza kuiamini mahakama inayo sikiliza kesi mwaka mzima ya uhaini wa mtu Mmoja?. Yani kwamba mtu Mmoja anaweza kupindua serikali.
Kilichopo ni kwamba Mahakama zetu haziaminiki. Na sio eti ikionekana jana walisema uongo ndo haitoaminika. That's why nikauliza na ikionekana walisema kweli ndo mtaiamini hiyo Mahakama?
 
Jana Mahakama ilisema CDF yupo nje lakini kuna tetesi yupo.

Najiuliza, mahakama ni sehemu ya kutoa haki ukiidanganya mahakama unaweza kufungwa, inapotokea mahakama yenyewe ndiyo imedanganya itakuwaje.
Sio kazi mahakama kumleta shahidi mahakamani. Hiyo ni kazi ya Lissu na genge lake.
 
Kwani MAHAKAMA inaaminika na nani??? nyie jamani msifikirie sisi mazuzu tunajua sana haya mambo fikiria mtu kama Katuge akipewa U judge ataachaje kupokea maelekezo??!! ndio mana tunasema katiba ibadilishwe Judge apatikane kwa uwezo sio kuzushia watu na kuwaumiza!! Kama pia hafuati taratibu aondolewe!!!

Leo hii tunajua kabisa kesi hii ni ya uonevu kabisa na tunajua kabisa hukumu ni kumfunga Lissu au Kumpa Hukumu yeyote mbaya zaidi tunajua na ndio itakua hivyo.....Hao wanaoitwa Ma Judge au Mahakimu wanalaumiwa sana nchi nzima hii!!! unadhani Ndunguru yule atakataa maelekezo???
 
Na wasipothibitisha je!?
Kwa wale matomaso kuwa hizo ni mahakama za simu moja watadhibitisha. Kuna watu huwa wanahadaa wananchi kuwa hakuna aliye juu ya sheria, watajionea mambo ya zilongwa mbali, zitendwa mbali.
 
Back
Top Bottom