Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 35,566
- 104,386
Wakuu.
Ikitokea, haujaridhishwa na mwenendo wa Bei ya mafuta, na unataka gari ambalo 99% misele Yako ni mjini bila kwenda nje ya mkoa wako, na unakaa Nyumba ambayo unaweza kupark gari na kuchaji, basi moja kati ya EV hizi zitakufaa;
1. Nissan Leaf (2018 - 2024)
Ni vizuri kuanza na gari affordable, na brand inayotambulika na kila mmoja. Mfano Nissan.
Hii gari Ina generation tatu, ninayoiongelea hapa ni 2nd gen ya 2018 hadi 2024.
Kwanza ni affordable, unapata kwa CIF hadi ya $4,000 na ushuru nafuu, unapata hadi kwa Mil 10.
Range yake kwa battery la kawaida (40 kWh) ni Kilometa 250 hivi, kwahiyo Kwa unit 40 hivi unatembea Kilometa 250.
NB: Unit 40 ni kama Tsh 15,000 tu.
Unaweza kuchagua generation ya kwanza, ambayo ni nafuu zaidi, unaweza kuipata used hadi kwa $2,500 ila Ina range ndogo hadi ya Kilometa 150 ikiwa mpya, used itashuka hadi 120.
Pia kwenye Nissan Kuna alternative Nissan Ariya (zenyewe zinaanzia mwaka 2023+) nayo ni SUV muonekano Bora zaidi na range kubwa zaidi (Kilometa 350 na zaidi kwa battery kubwa zaidi). Ila Bei zake inaweza anzia $17,000 kuendelea kabla ya ushuru.
2. Tesla Model 3 (2022- )
Ukitaka kuumiza watu vichwa, basi icheki na Tesla Model 3. Hapa Kuna option ya miaka mingi, ila at least angalia ya 2022 kwasababu Tesla walianza kutumia LFP (Lithium Iron Phosphate) battery na pia walianza kutumia AMD Ryzen processor, ambazo ni bora kuliko Intel za zamani.
Tesla zina range kubwa zaidi ya Leaf, unaweza kufika hadi Kilometa 300+
Changamoto kuu ni brand mpya kwa nchi za Africa, pia baadhi ya features kama ramani, satellite navigation, live traffic, remote start, SIM card nk havitafanya kazi Africa. Ila Bado utaendeshwa vizuri tu.
Model 3 za 2022 ukitulia unazipata kwa $12,000 au pungufu, na ushuru wake ni nafuu sana, haivuki Mil 12.
Pia unaweza kucheki Model Y ambayo ni kubwa zaidi au Model X ambayo ni SUV, Ile yenye milango ya kishua. Ila hizi Bei sio nafuu.
3. Toyota bZ4X (2022 -)
Kama unapenda watu wadhani unaendesha Rav 4, kumbe EV, basi ishi na bZ4X kutoka Toyota.
Hii ni SUV nzuri, reliable (of course it's Toyota), range kubwa kuanzia Kilometa 400, na kwasababu wanatumia platform ya TNGA (Toyota New Global Platform) basi inaingiliana baadhi ya spare na Magari mengi tu ya kawaida mfano Prius, Aqua, CH-R, Corolla nk (ya 2020+)
Subaru wanayo hii gari, wanajiita Subaru Solterra ila rebadged, kila kitu sawa kabisa.
Kwa used unazipata kuanzia $17,000 ukiwa mvumilivu unaweza kupata pungufu.
4. Hyundai Ioniq 5 (2022 -)
Moja ya best selling EV Duniani kutoka Hyundai, ni hii Ioniq 5.
Ina muonekano mzuri, kwa wapenzi wa gari jamii ya kina Golf au Polo, pia Ina range nzuri kuanzia Kilometa 350 na zaidi.
Bei yake ni competitive, unapata hadi $12,000 na uzuri platform yake inashare na Magari mengi tu ya Hyundai na baadhi ya Kia. Kwahiyo issue ya spare sio kubwa sana.
Changamoto kuu nimeona ni kupata RHD, mengi nimekutana nayo ni LHD, kwasababu mengi yapo stock ya Korea.
5. Chinese EV
Ukitaka options za China, nashauri utembelee Ofisi zao mfano BYD Nyerere Rd Dar es Salaam. Wao wana hadi kuarrange test drive Kama upo serious na kununua.
Mwenye mawazo tofauti au kuongezea karibu.