Ikitokea dada yangu na kaka yangu wamesalitiwa na wenza wao nitamuonea huruma zaidi kaka yangu kuliko dada

Ikitokea dada yangu na kaka yangu wamesalitiwa na wenza wao nitamuonea huruma zaidi kaka yangu kuliko dada

Anachoongea kina mantiki na ndio uhalisia wa maisha halisi.Ni basi tu mnataka kubadilisha mifumo sio kitu rahisi na pia ina gharama zake na moja ya gharama ni wanawake wengi kuwa Singles.
 
Eti watasema uko dickmatized, kumbe umeamua kukubali nature mrembo.

Ila me napinga ku normalize usaliti sis, kwa mahaba ya kiwango chako usaliti usivumilie ata kidogo you deserve the best as much as you give it 🌹🌹
ASante.
Sija normalize mkuu.
NImesema tu kuwa mfano mim mume wangu ananihudumia mimi pamoja na mwanangu ambae sio damu yake nikimsaliti maumivu yake yanakua makqli zaidi.
 
Mwambie kabisa mimi ni shindikana kama mdau mmoja alivyosema pale juu 😁😁
Sidhani kama kuna haja yakumwambia unaonekana tu au basi ngojea nimwambie😃 ephen_
Ephen mdogo wangu sitaki kukuona unaongozana na Khantwe
😃😃😃.

Atakuharibu🏃‍♂️‍➡️😃
 
Dogo netiweki inasumbua huko kwenu? Mbona unanikwoti mara tatu post moja?
Inasumbua balaa.
Au sijui ni hiki kiswaswadu kimeshindwa kuhimili vichambo vyenyu😃
 
Kwa uzoefu wangu siwezi kumuunga mkono au kumpinga ila nina uhakika anasema kweli.

Wananawake mnatofautiana kimtazamo. Kuna watamaduni sana na wasasa sana.

Kuna KE atavumilia kukaa nyumbani bila shughuli, ila hatovumilia kusalitiwa.

Kuna KE atavumilia kusalitiwa, ila hatovumilia kusimangwa.

Kuna KE atavumilia kupigwa, ila hatovumilia kusalitiwa nk. nk.

Kuna KE wameridhika tu na mfumo uliopo. Labda hawajaelimika sana, wameshika sana dini, malezi nk.
Na ninahisi familia nyingi zipo hivi. Wanaishi kama wapangaji tu, wameshaachana kitambo ila hawajatawanyika. Au wananafikiana.
Wala mi sikatai hali halisi hivyo ndivyo watu huishi huko mitaani, kesi zote tunazozisikia kila siku ni sababu ndio maisha ya watu.

Ila yes usaliti ni tatizo, kujustify that’s another story inaonekana mtu thamani yake ni ndogo sana kama anaweza akasalitiwa halafu akaona ni kawaida.

Kesi ni tofauti kwa mitara ya waislamu sina tatizo nao , lakini pia sio supporter.

Probably we share dicks/pussies, but we can’t love sharing. How can one justify this?
 
Nakuona kama mwanamke aliyechanganyikiwa.
Upo radhi kukaa kwenye uozo ili tu uonekane upo kwenye ndoa.
Kaongea ukweli. Athari za kuchepuka mume na kuchepuka mke ni tofauyi. Mume akichepuka bado ndoa inaweza kuendelea kuwepo lakini mke akichepuka ndoa inakufa hapo hapo. Sababu kuu ni uwekezaji ambao mwanaume anaufanya. Akisalitiwa maumivu ni makubwa zaidi, hata akichepuka bado uwekezaji wake utapooza maumivu ya mwanamke. Ndio maana hata wanawake mkisalitiwa na mwanaume asiye na hela wala hawahudumii mtamwita msaliti, lakini mkisalitiwa na mwenye hela na anawapa huduma zote mtamsambulia mchepuko na kumwita mwizi wa waume za watu
 
Prida kuna muda unakwama pabaya, unatupa vibe ya pick me fulani hivi. (Mwanamke anayeshusha vigezo ili iwe rahisi kuchaguliwa) Aina ya wanawake ambao mnawaweka wanaume juu mnawakandamiza wanawake wenzenu chini.

Maumivu ya usaliti kwa watu wenye commitment ni yale yale kwa KE au ME,

Out here, wanawake wengi ni kama mmechanganyikiwa kwa kusalitiwa kila siku na kusamehe/kupotezea.

Usaliti una destroy a soul.

Usaliti una sababisha insecurities, ndio maana wengi mnachukia wanawake wenzenu sababu the moment mkisalitiwa mnaanza kujiuliza huyu ana nini, mimi sina nini.

Usaliti unaleta magonjwa ya ngono ndani ya ndoa, hakuna exception kwamba mmoja ataleta magonjwa mwingine hataleta.

There’s no better!
Prida hajahalalisha usaliti, kafanya ulinganisho wa athari za usaliti pale unapofanywa na mume na unapofanywa na mke. Either way usaliti sio kitu kizuri lakini hatuwezi ku-pretend kwamba athari zake ni sawa ukifanywa na jinsia yoyote.

Kuna kimoja kimoja ambacho wanawake mmegoma kukiachia nacho ni "provision demand" kwenye mahusiano. Unapokubali provision kutoka kwa mwanaume lazima ukubali kwamba unauza uhuru wako. Nafikiri unajua anaelipia ndie mmiliki, ndie mwenye sauti na ndie mwenye haki ya kufanya anachotaka. Mkitaka uhuru anzeni kwanza kuikataa hiyo provision demand kwenye mahusiano.
 
Back
Top Bottom