Ikitokea dada yangu na kaka yangu wamesalitiwa na wenza wao nitamuonea huruma zaidi kaka yangu kuliko dada

Mila na desturi tu.

Hata wanaume tuna mizigo yetu tumebebeshwa. Mwanaume anaamini anastahili kabisa kuteseka kwa ajili ya mwanamke kisa "majukumu".
Hiki kitu wanawake wa kisasa wengi hawakijui. Wamekalilishwa usawa wa kijinsia kwa mtazamo kwamba mwanaume na mwanamke wapo uniform kwenye kila kitu. Bahati mbaya sana ukifika wakati wa wao kuvaa viatu vya mwanaume wanaamisha magoli.

Kiukweli binadamu hatupo sawa. Kuna situation ambazo zinamkandamiza mwanamke lakini hazimuathiri mwanaume mfano promiscuos life, vile vile kuna situations ambazo zinamkandamiza mwanaume lakini hazimuathiri mwanamke mfano umasikini. Mwanamke masikini anaweza kupendwa, kujaliwa na kuthaminiwa. Lakini mwanaume masikini akuna anaemuhitaji kwa lolote kwenye maisha yake
 
Prida hajahalalisha usaliti, kafanya ulinganisho wa athari za usaliti pale unapofanywa na mume na unapofanywa na mke. Either way usaliti sio kitu kizuri lakini hatuwezi ku-pretend kwamba athari zake ni sawa ukifanywa na jinsia yoyote.

Kuna kimoja kimoja ambacho wanawake mmegoma kukiachia nacho ni "provision demand" kwenye mahusiano. Unapokubali provision kutoka kwa mwanaume lazima ukubali kwamba unauza uhuru wako. Nafikiri unajua anaelipia ndie mmiliki, ndie mwenye sauti na ndie mwenye haki ya kufanya anachotaka. Mkitaka uhuru anzeni kwanza kuikataa hiyo provision demand kwenye mahusiano.
Ni umasikini tu ndio unawafanya mna-reduce provision kwenye pesa pekee. Wanawake wana provide vingi tu, sana sana sana.

However hata ukiprovide kama elon musk ukisaliti you will be held accountable.
 
Hiki kitu wanawake wa kisasa wengi hawakijui. Wamekalilishwa usawa wa kijinsia kwa mtazamo kwamba mwanaume na mwanamke wapo uniform kwenye kila kitu. Bahati mbaya sana ukifika wakati wa wao kuvaa viatu vya mwanaume wanaamisha magoli.

Kiukweli binadamu hatupo sawa. Kuna situation ambazo zinamkandamiza mwanamke lakini hazimuathiri mwanaume mfano promiscuos life, vile vile kuna situations ambazo zinamkandamiza mwanaume lakini hazimuathiri mwanamke mfano umasikini. Mwanamke masikini anaweza kupendwa, kujaliwa na kuthaminiwa. Lakini mwanaume masikini akuna anaemuhitaji kwa lolote kwenye maisha yake
Ndo maana viongozi wakubwa wanatakiwa wawe wameoa/olewa.

Ndoa ina siasa sana, inahitaji compromise nyingi, ukiishi humo unakuwa mwanasiasa bora kabisa😅
 
Hakuna mtu anapenda kushare mbo*/kum* ni vile tu hamna namna mnakubali kushare, usaliti unauma sababu hakuna mtu willingly anapenda kushare.
Naelewa. Wanaume wanaonyamazia usaliti watakuwepo pia kwa sababu mbalimbali.

Tamaduni zetu hazijali kuhusu ubinafsi(individualism) zinajali zaidi kuhusu kundi(collectivism). Mpaka tutakapojali ubinafsi wa mtu huu utata utazidi kuwepo.
 
Ni umasikini tu ndio unawafanya mna-reduce provision kwenye pesa pekee. Wanawake wana provide vingi tu, sana sana sana.

However hata ukiprovide kama elon musk ukisaliti you will be held accountable.
Sio umasikini, ni asili ya kimaumbile. Hata mwanamke mwenye hela pia kuna namna anafurahia uanamke wake akiwa na mwanaume anayempa provision na protection. Kwenye dunia ya sasa provision, security and protection ni pesa. Hapa hakuna haja ya kuleta siasa.

Kuhusu kuwajibika linapokuja suala la kuchepuka kila mwanaume anahukumiwa kulinganana na uwezo wake kiuchumi. Mwanaume asiekua na hela ataitwa msaliti. Mwanaume mwenye hela haitwi msaliti, badala yake mchepuko wake ndio utaitwa mwizi wa waume za watu.

Ule msemo wenu wanawake wa "bora ulie ukiwa kwenye benzi, kuliko kulia ukiwa kwenye baiskeli" unajua maana yake. Maana yake ni kuhalalisha usaliti na maumivu mengine yote ambayo mwanamke anafanyiwa na mwanaume mwenye hela kwenye ndoa/mahusiano.
 
Ni kama haupo proud na gender yako shida ni nini dear?
Sijaona mahali kaonyesha hajivunii uanamke wake. Ni mtazamo tu. Tena watu wa namna hii ambao hawaishi kwa kuiga mitazamo ya wengi au "trends" wanakuwaga na very high self esteem.
 
Wala mi sikatai hali halisi hivyo ndivyo watu huishi huko mitaani, kesi zote tunazozisikia kila siku ni sababu ndio maisha ya watu.

Ila yes usaliti ni tatizo, kujustify that’s another story inaonekana mtu thamani yake ni ndogo sana kama anaweza akasalitiwa halafu akaona ni kawaida.

Kesi ni tofauti kwa mitara ya waislamu sina tatizo nao , lakini pia sio supporter.

Probably we share dicks/pussies, but we can’t love sharing. How can one justify this?
Hajahalalisha usaliti japo mliomuelewa hivyo pia siwalaumu kwa namna alivyoandika. Nimemuelewa kwamba hukumu kwa msaliti inapaswa kuzingatia specific facts of the case. Adhabu kama itatolewa nayo izingatie character nzima ya mhalifu. Siyo kila mtu anayekutwa na hatia ya mauaji apewe death penalty au life in prison. Na uhalisia on the ground ndo upo hivyo mara nyingi kwa mambo mengi.
Hakuna anayependa au anapaswa kusalitiwa. Ila pia kusema msaliti hasamehewi ni kauli mbiu kama kauli mbiu nyingine tu. Unaweza kusema sitasamehe na ukaja kusamehe. Na unaweza kusema utasamehe ukajikuta unashindwa kusamehe ikikutokea.
 
Somehow somewhere mnadhani hatujamuelewa Prida, mna-understatement uwezo wetu wa kusoma kwa ufahamu, wengine kwenye comprehension tulikuwa tunapata maksi zote kama ni tano tuna chukua zote.

Ili umuelewe Prida vizuri ni lazima uelewe mitazamo yake, falsafa yake na usuli wa mabandiko yake. This is just the tip of the iceberg. Angalia comments za tuliompinga, hatujampinga with a random opinions, tumempinga kwa opinions zenye pattern za kufanana…. wala hamjajiuliza kwanini?

😅

Wapi huko hukumu ya msaliti inapaswa izingatie specific facts za usaliti? Usaliti ni usaliti kuhusu nani atafanya nini na msaliti wake that’s another story, kuuremba usaliti kwa jina la provision ndio kitu tumekataa. Hata kama hali halisi ipo hivyo, uhalisia unakataa.
 
Sio umasikini, ni asili ya kimaumbile. Hata mwanamke mwenye hela pia kuna namna anafurahia uanamke wake akiwa na mwanaume anayempa provision na protection. Kwenye dunia ya sasa provision, security and protection ni pesa. Hapa hakuna haja ya kuleta siasa.

Kuhusu kuwajibika linapokuja suala la kuchepuka kila mwanaume anahukumiwa kulinganana na uwezo wake kiuchumi. Mwanaume asiekua na hela ataitwa msaliti. Mwanaume mwenye hela haitwi msaliti, badala yake mchepuko wake ndio utaitwa mwizi wa waume za watu.

Ule msemo wenu wanawake wa "bora ulie ukiwa kwenye benzi, kuliko kulia ukiwa kwenye baiskeli" unajua maana yake. Maana yake ni kuhalalisha usaliti na maumivu mengine yote ambayo mwanamke anafanyiwa na mwanaume mwenye hela kwenye ndoa/mahusiano.
Jamii imebadilika sana, Kuna maamuzi hayafanyiki collectively kama mnavyotaka kuonesha. Na hapa ndipo tatizo linapoanziaga, kuwachukua binadamu wote kuwalundika kwenye kapu moja.

Ingekuwa rahisi hivyo wanaume wenye hela wasingekaa waachwe kwenye ndoa since hela ni kila kitu, ila kuna miamba wanawake wenzetu wamethubutu wameweza, that’s accountability ninayoizungumzia. Nasema hivi; usaliti upo, unafanyika kila siku left right and center, ikitokea msaliti akakamatwa msalitiwa atadeal naye anavyoona inafaa.

Mada ya prida ina lenga kudogosha kosa la usaliti kiumeni, kulikuza kikeni na kuwapa wanaume free card ya kuliendeleza, since lina madhara machache kwa wanaume…. Haihitaji degree ya sheria kuelewa mnachofanya hapa.
 
Labda kama kuna tafsiri nyingine ya “high self esteem” imetoka.
Tafsiri ileile ya self esteem ya vitabuni. And, yes, you can have a high self esteem based on misguided beliefs. Anaweza asiwe sahihi ktk baadhi ya mitazamo yake but she sounds comfortable with her beliefs. Being comfortable with your beliefs is generally a strong sign of a healthy self-esteem. Hatafuti kukubalika, anajua msimamo wake siyo popular hapa jukwaani kwa wanawake wenzie wengi, lakini anauelezea kwa lugha isiyo ya kulazimisha kuaminiwa.
 
Jamii imebadilika sana, Kuna maamuzi hayafanyiki collectively kama mnavyotaka kuonesha. Na hapa ndipo tatizo linapoanziaga, kuwachukua binadamu wote kuwalundika kwenye kapu moja.

Ingekuwa rahisi hivyo wanaume wenye hela wasingekaa waachwe kwenye ndoa since hela ni kila kitu, ila kuna miamba wanawake wenzetu wamethubutu wameweza, that’s accountability ninayoizungumzia. Nasema hivi; usaliti upo, unafanyika kila siku left right and center, ikitokea msaliti akakamatwa msalitiwa atadeal naye anavyoona inafaa.

Mada ya prida ina lenga kudogosha kosa la usaliti kiumeni, kulikuza kikeni na kuwapa wanaume free card ya kuliendeleza, since lina madhara machache kwa wanaume…. Haihitaji degree ya sheria kuelewa mnachofanya hapa.
Kama kumbukumbu zangu zipo sawasawa alishawahi andika hapa kwamba yupo comfortable na maisha ya yeye na son wake tu (single mother). Hivi leo anasema ana mwenza and she's proud of her new lifestyle (being a wife). Quite a jump. Anaonekana kama ni mtu ambaye she's open to change when confronted with new life realities/facts. That's a strong sign of maturity. Don't you think so? Huyu siyo wa kumtafsiri, kumhukumu au kumkosoa kwa historia ya maandiko yake tu peke yake. Utahitaji other facts kupinga misimamo yake. And, again, I don't necessarily agree with her on everything she writes. Ila yupo sahihi kiasi fulani. Viapo vingi kwenye maisha havitekelezeki kiuhalisia.
 
Somehow somewhere mnadhani hatujamuelewa Prida, mna-understatement uwezo wetu wa kusoma kwa ufahamu, wengine kwenye comprehension tulikuwa tunapata maksi zote kama ni tano tuna chukua zote.

Ili umuelewe Prida vizuri ni lazima uelewe mitazamo yake, falsafa yake na usuli wa mabandiko yake. This is just the tip of the iceberg. Angalia comments za tuliompinga, hatujampinga with a random opinions, tumempinga kwa opinions zenye pattern za kufanana…. wala hamjajiuliza kwanini?

😅

Wapi huko hukumu ya msaliti inapaswa izingatie specific facts za usaliti? Usaliti ni usaliti kuhusu nani atafanya nini na msaliti wake that’s another story, kuuremba usaliti kwa jina la provision ndio kitu tumekataa. Hata kama hali halisi ipo hivyo, uhalisia unakataa.
Wanaume wengine wanadhani tunamponda Prida, wakati ukweli ni kwamba tunapinga hoja yake sio yeye binafsi

Sisi hatumpondi wala kumbeza Tunachopinga ni mtazamo wa kumfanya mwanamke ajione kama chaguo la mwisho kana kwamba ili apendwe au akubalike na mwanaume, lazima ajishushe na kuvumilia kila kitu

Na Prida mada zake nyingi ni za kumshusha hadhi mwanamke huku akimpa thamani mwanaume pekee

Kuna tofauti kubwa sana kati ya utii na kujidhalilisha
Kuna tofauti kati ya kumheshimu mwanaume na kupoteza thamani yako mbele yake

Sisi tunawaheshimu wanaume, tunawatii pale inapostahili na tunajua nafasi yao
Lakini utii wetu hauondoi heshima yetu na upendo wetu haupaswi kuwa sababu ya kujishusha thamani

Ooh dada na kaka angu wa ki cheatiwa nitamuonea huruma kaka yangu hivi huyu yupo sawa kweli kwanini kaka na sio wote?

Nasena hivi prida Mwanamke anaweza kuwa mtiifu bila kuwa mnyonge

Anaweza kumheshimu mwanaume bila kujidhalilisha

Na anaweza kumpenda mwanaume bila kujiona kuwa chaguo la mwisho

Heshima kwa mwanaume haimaanishi mwanamke ajivue heshima na thamani yake mwenyewe

Wanawake tuzinduke usingizini tujifunze kutofautisha mambo
 
Mkuu kumshutumu mtu kwamba hajivunii jinsia yake ya kike ni personal attack. Hakuna hoja hapo. Kusema mwanaume ana mchango mkubwa ktk maisha ya mwanamke ni mtazamo tu. Na mara nyingi - ktk baadhi ya maeneo ya kimaisha, siyo ktk kilakitu, siyo mara zote, na siyo kwa kila jamii - kuna ukweli. Mimi nikikuambia wewe una strengths nyingi kuliko mimi ktk jambo fulani la kimaisha haina maana kwamba mimi sifai chochote. Unaweza kuwa mtazamo wangu potofu au ukawa ndio ukweli wenyewe. Kwani binadamu hatutofautiani strengths and weaknesses?
 
Jamii imebadilika sana, Kuna maamuzi hayafanyiki collectively kama mnavyotaka kuonesha. Na hapa ndipo tatizo linapoanziaga, kuwachukua binadamu wote kuwalundika kwenye kapu moja.

Ingekuwa rahisi hivyo wanaume wenye hela wasingekaa waachwe kwenye ndoa since hela ni kila kitu, ila kuna miamba wanawake wenzetu wamethubutu wameweza, that’s accountability ninayoizungumzia. Nasema hivi; usaliti upo, unafanyika kila siku left right and center, ikitokea msaliti akakamatwa msalitiwa atadeal naye anavyoona inafaa.

Mada ya prida ina lenga kudogosha kosa la usaliti kiumeni, kulikuza kikeni na kuwapa wanaume free card ya kuliendeleza, since lina madhara machache kwa wanaume…. Haihitaji degree ya sheria kuelewa mnachofanya hapa.
Prida hajahalalisha usaliti. Usaliti sio mzuri ukifanywa na yoyote lakini ukweli ni kwamba athari zake ni tofauti unapofanywa na mume na unapofanywa na mke. Chanzo cha utofauti huo ni uwekezaji ambao mwanaume anabebeshwa kuanzia mwanzo wa mahusiano. Mifano ipo wazi sijui ni umeamua tu kuwa mbishi au lah.
 
Mkuu kumshutumu mtu kwamba hajivunii jinsia yake ya kike ni personal attack. Hakuna hoja hapo. Kusema mwanaume ana mchango mkubwa ktk maisha ya mwanamke ni mtazamo tu. Na mara nyingi - ktk baadhi ya maeneo ya kimaisha, siyo ktk kilakitu, siyo mara zote, na siyo kwa kila jamii - kuna ukweli. Mimi nikikuambia wewe una strengths nyingi kuliko mimi ktk jambo fulani la kimaisha haina maana kwamba mimi sifai chochote. Unaweza kuwa mtazamo wangu potofu au ukawa ndio ukweli wenyewe. Kwani binadamu hatutofautiani strengths and weaknesses?
Nani kam attack na hivi unajua kutofautisha kati ya shutuma nakuuliza ?

Naomba mimi na wewe tuishie hapa 🙌
Tusichoshane
 
Back
Top Bottom