Kwa jicho la mbali lisu hakuonesha au kueleza njia watakauotumia kuzuia uchaguzi , mfano angesema mojakwa Moja wafuasi wake wasiende kupiga kura wakae nyumbani,
Kwasababu hakusema watatumia njia gani Mimi Kwa mtazamo wangu naona serikali iko sahihi kutafasili kuwa kile kilichotokea ndincho kilicho maanishwa ,
Na huo ni ukweli mchungu Kwa WANACHADEMA.
Wewe ungelikuwa mwanasheria basi wateja wako wangekuwa wanaangukia pua kila mara...
Mimi tu layman wa sheria naweza kukuambia kwamba kwa sababu Lissu hakutaja mbinu yeyote ni namna gani watakinukisha, watafanya uasi, watazuia uchaguzi basi huwezi muhusianisha na namna hiyo iliyojaribiwa na waandamanaji...
Hukumu ya mahakama huwa inatolewa kwa ushahidi usio na shaka, tena shaka iliyothibitishwa...
Katika matamshi ya Lissu hakutaja kama wataandamana, kama watachoma mali za umma, kama wanataka kuipindua serikali n.k...
Kwa akili ya kawaida tu, kama Lissu angelikuwa amepanga hayo yote, ilikuwepo wapi TISS au intelijensia ya jeshi kuzima jaribio hilo hata kabla ya MO29?
Majibu yanaweza kuwa mawili
1. Hakukuwa na mikakati yeyote ovu hivyo mamlaka za ushushushu zilipuuzia na kujiandaa kwa nguvu ya kawaida...
2. Mamlaka zetu za kiusalama zililala usingizi, na hili linaweza kuwa na mashiko kidogo maana viongozi wakuu wa serikali walikiri katika hotuba zao mbalimbali kwamba nchi iliingiliwa na mamluki toka nchi za jirani...
Sasa katika hoja zote hizi mbili, hadi sasa kutokana na mwenendo wa kesi ya TL, unaona kuna kilichotajwa?