Ikitokea Manchester City akashinda leo navuta milion 50

Ikitokea Manchester City akashinda leo navuta milion 50

Kila la heri boss, kubeti ni mchezo wa kubahatisha, bahati ikiwa upande wako unashukuru MUNGU.
 
Wakuu Leo ndio Leo kwangu ikitokea Manchester city kamfunga arsenal navuta milion 50 nakua new milionea in town maombi yenu aisee Wana JamiiForums wenzangu treni langu linaisha Leo lilikua mechi 20 mechi ya Mancity na Arsenal ndio ya mwisho.
Pole
 
Kabisa mkuu yaani usitangaze kabisa ni bora watu waone matokeo tayari. Halafu sometimes unayemwambia anaweza kuwa hajui kama ana negative forces towards you na wengine makusudi kabisa anakufanyia roho mbaya.
Mkuu Mimi Kuna ticket nilitangaza na nilishinda milion 12 kawaida tu hata haihusiani na hizo imani
 
Kabisa mkuu yaani usitangaze kabisa ni bora watu waone matokeo tayari. Halafu sometimes unayemwambia anaweza kuwa hajui kama ana negative forces towards you na wengine makusudi kabisa anakufanyia roho mbaya.
Ukweli kabisa...husdah ni mbaya sana! Watu kila siku wanapunwa halafu wewe unakuja kuwatangazia kuwa unaenda kula pesa ndefu..Lazima wakuhusudu tu na utashangaa mambo yanavyokwenda kinyume naa vile ulivyokuwa ukitarajia
 
Duh kweli mpira hautabiriki, dakika za nyongeza Man city wanasawazisha hapa na dakika mbili baadae wanapata chuma cha tatu. Dakika za jioooooni Man City inamfurahisha mleta uzi. Man city 3 Arsenal 2. Mechi imeisha, mleta uzi kachukue milioni 50 yako. Hongera sana haikuwa rahisi aisee.
Mkuuu cash out dakika ya 90 haipo
Maumivu makali sana yalinitokea hadi nikawaga
 
Imekustua nini? Ukawa una refresh mara mbili mbili kuona pengine ni kweli. Nilikuwa natania tu japo ilikuwa kidogo nipatie ngoma imeisha 2-2 pole kwa mleta uzi. Angeweka double chance angekuwa anafurahia hapo.
Nilkuwa nimeandika comment yang awali,nilipoona hii comment yako ikabid niifute yang kwanza afu nifatilie matokeo
 
Back
Top Bottom