Ikitokea ukapewa fursa ya kukutana na wewe mwenyewe wa miaka 10 nyuma. Je, utajishauri nini?

Ikitokea ukapewa fursa ya kukutana na wewe mwenyewe wa miaka 10 nyuma. Je, utajishauri nini?

greater than

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
1,653
Reaction score
3,060
Habari za Jumatatu wanajamii.Pia hongereni kwa pirika za kutafuta pesa za mahitaji yako.

Ninajua mpaka kufika katika umri ulionao kuna makosa kadhaa ushafanya na pengine ukawa unajutia.

Hapa nina swali fikirishi
Eti, kama ikatokea ukapewa fursa ya kurudi miaka 10 au 15 nyuma na kukutana na wewe mwenyewe wa miaka hiyo kumi nyuma na ujipe ushauri. Je, utajishauri nini?

Kwangu binafsi, ningejishauri
  • Kuangaika kupata fursa na kujitutumia katika kuzitekeleza hata kama zitafeli.
  • Kuondoa uoga kabisa katika kuanza maisha.
  • Fursa haziishii Dar,nitoke na kwenda mikoani na hata ikitokea nje ya Tanzania.
  • Kuwa karibu na watu wenye kuwaza maendeleo.
 
Ningejiambia kijana punguza umalaya.

Miaka ingezidi hiyo 10, ikawa 15 hivi, ningejiambia Ugenious wako hauendani na utoro wako, ingia darasani utafanya vizuri maradufu.

Matokeo yako ni mazuri ila unapaswa kuingia darasani na sio kwa kubagua vipindi.

Kisha nisingekubali kusoma A level baada ya O level ningeenda chuo moja kwa moja.
 
Habari za Jumatatu wanajamii.Pia hongereni kwa pirika za kutafuta pesa za mahitaji yako.

Ninajua mpaka kufika katika umri ulionao kuna makosa kadhaa ushafanya na pengine ukawa unajutia.

Hapa nina swali fikirishi...
Eti,kama ikatokea ukapewa fursa ya kurudi miaka 10 au 15 nyuma na kukutana na wewe mwenyewe wa miaka hiyo kumi nyuma na ujipe ushauri, Je,utajishauri nini....?

Kwangu binafsi ,ningejishauri...
  • Kuangaika kupata fursa na kujitutumia katika kuzitekeleza hata kama zitafeli.
  • Kuondoa uoga kabisa katika kuanza maisha.
  • Fursa haziishii Dar,nitoke na kwenda mikoani na hata ikitokea nje ya Tanzania.
  • Kuwa karibu na watu wenye kuwaza maendeleo.
Nitaingia ccm mapema sana na kuwa chawa mwandamizi Ili nipande vyeo
 
Kwenye maisha kuna vitu vinaitwa 'disruption points'

Disruption points ni matukio hasi kwenye maisha, ambayo yanakubadilisha kimtazamo, na kukupa uzoefu fulani mfano; kufiwa, kuumwa sana, kuachika, kuachishwa masomo au kazi nk

Unaweza ukatamani kurudi nyuma ubadilishe hayo matukio lakini utakuwa umejinyima upeo flani ambao ungeupata kwa kupitia mambo hayo.

Mfano labda ukajishauri uache utoro mashuleni, huwezi jua kama ule utoro ndo umekusaidia kujijengea tabia ya kujiamini na ku 'take risks'

Kila unachopitia kwenye maisha yako kinakujenga kwa namna fulani, ukijaribu kubadilisha mambo huwezi jua unabadilisha tabia zako kwa kiasi gani.
 
Back
Top Bottom