Ikiwa Rais ndiye anatoa pesa zake kwa maendeleo ya nchi, Serikali inapeleka wapi kodi zetu?

Kauli ya hovyo ni kua mama halali usiku na mchana kutupambani utasema aliutaka urais ili akalale
 
Tumesikia kila mdomo wa Waziri na viongozi waandamizi wanaposimama kuhutubia ama kuzungumza wanamshukuru Rais kwa kutoa hela ambazo zimwtekeleza miradi ya maendeleo na miundombinu.

Hivyo wanatuaminisha kuwa fedha zote za miradi na maendeleo zinatolewa na rais. Na anayetoa hela hufanya hivyo kwa hiyari halazimishwi. Ndo maana hata akina pascal Mayala wanatuasa kuwa tuwe na shukrani kwa hisani anazotufanyia rais ambapo tafsiri inayojengeka ni kuwa Rais hawajibiki kwa yeyote na lolote bali ni utashi wake kufanya kila analofanya na hakuna wa kumhoji na ni kumkosea heshima kuhoji wajibu wake wa kikatiba.

Sasa, tunajjuliza sisi wadadisi na wakaidi wa mfumo usiozingatia katiba na sheria.

  1. Nini hutokea kwa mtu anayegombea urais akashinda na ghafla anakuwa tajjri mkubwa anayeweza kufadhili miradi ya serikali bila masharti magumu?
  2. Tunapolipa kodi zetu na fedha za wafadhili zinapoingia serikalini huwa zinapelekwa wapi? Kwa sababu hatujawahi kusikia serikali imetoa hela za miradi. Rais anajitolea mnoo hadi tunamhurumia
  3. Wizara ya fedha kwa nini isifutwe ama isiwekwe chini ya ofisi ya Rais kwa sababu inakusanya fedha na haiwezi kuziratibu zinaliwa hovyo hadi rais anaingilia kati kutoa fedha zake kufanikisha miradi ya maendeleo
  4. Ushahidi wa ripoti ya CAG unaonesha wazi kabisa kuwa ofisi ya Rais haijawahi kupata hati chafu.
  5. Lakini hakuna wizara wala idara ya serikali iliyokwepa tuhuma za matumizi mabaya ya kodi zetu, hivyo inawezekana kodi zetu zinaliwa na serikali hadi kufikia Rais kutoa fedha zake
  6. Wabunge wana kazi gani kama siyo ulaji wa fedha za umma? Nasema hivyo kwa sababu wakifika Bungeni hugeuka kuwa wabunge wa chama na siyo wa wananchi tena. Tumeona viongozi waandamizi wa vyama wakikutana na wabunge na kuwapa maelekezo hususan Bunge la Katiba lazima chama kikuu kiwape maelekezo wabunge na hakuna mahala ambapo wwnanchi wamewahi kusikilizwa na wabunge. Mifano ni mingi sana...

All in all, kama rais anatoa fedha zake kwa maendelo ya nchi, serikali inangoja nini kujiuzulu kwa kushindwa kufanya hivyo kwa jamii? Na kodi zetu zinaenda wapi?

CC: Retired Depal MshanaJR
Asante na endelea na maswali magumu.
 
Hoja kama hizi machawa huwa wanazitazama kwa jicho la pembeni, kwamba mama katoa pesa😂
 
Pesa za serikali zinapelekwa kwenye mfuko wa Rais ambae ndie custodian wa pesa zote then anazitoa kwenye miradi mbalimbali.

Punguza ujinga ndugu na kujitoa ufahamu,hata vitani kamanda ndio husifiwa ila uliwahi muona mstari wa mbele wa vita?
Pesa za serikali zinapelekwa kwenye mfuko wa raisi? Hili naomba maelezo yake ya kina, kumbe kuna mfuko wa raisi?
 
Tumesikia kila mdomo wa Waziri na viongozi waandamizi wanaposimama kuhutubia ama kuzungumza wanamshukuru Rais kwa kutoa hela ambazo zimwtekeleza miradi ya maendeleo na miundombinu.

Hivyo wanatuaminisha kuwa fedha zote za miradi na maendeleo zinatolewa na rais. Na anayetoa hela hufanya hivyo kwa hiyari halazimishwi. Ndo maana hata akina pascal Mayala wanatuasa kuwa tuwe na shukrani kwa hisani anazotufanyia rais ambapo tafsiri inayojengeka ni kuwa Rais hawajibiki kwa yeyote na lolote bali ni utashi wake kufanya kila analofanya na hakuna wa kumhoji na ni kumkosea heshima kuhoji wajibu wake wa kikatiba.

Sasa, tunajjuliza sisi wadadisi na wakaidi wa mfumo usiozingatia katiba na sheria.

  1. Nini hutokea kwa mtu anayegombea urais akashinda na ghafla anakuwa tajjri mkubwa anayeweza kufadhili miradi ya serikali bila masharti magumu?
  2. Tunapolipa kodi zetu na fedha za wafadhili zinapoingia serikalini huwa zinapelekwa wapi? Kwa sababu hatujawahi kusikia serikali imetoa hela za miradi. Rais anajitolea mnoo hadi tunamhurumia
  3. Wizara ya fedha kwa nini isifutwe ama isiwekwe chini ya ofisi ya Rais kwa sababu inakusanya fedha na haiwezi kuziratibu zinaliwa hovyo hadi rais anaingilia kati kutoa fedha zake kufanikisha miradi ya maendeleo
  4. Ushahidi wa ripoti ya CAG unaonesha wazi kabisa kuwa ofisi ya Rais haijawahi kupata hati chafu.
  5. Lakini hakuna wizara wala idara ya serikali iliyokwepa tuhuma za matumizi mabaya ya kodi zetu, hivyo inawezekana kodi zetu zinaliwa na serikali hadi kufikia Rais kutoa fedha zake
  6. Wabunge wana kazi gani kama siyo ulaji wa fedha za umma? Nasema hivyo kwa sababu wakifika Bungeni hugeuka kuwa wabunge wa chama na siyo wa wananchi tena. Tumeona viongozi waandamizi wa vyama wakikutana na wabunge na kuwapa maelekezo hususan Bunge la Katiba lazima chama kikuu kiwape maelekezo wabunge na hakuna mahala ambapo wwnanchi wamewahi kusikilizwa na wabunge. Mifano ni mingi sana...

All in all, kama rais anatoa fedha zake kwa maendelo ya nchi, serikali inangoja nini kujiuzulu kwa kushindwa kufanya hivyo kwa jamii? Na kodi zetu zinaenda wapi?

CC: Retired Depal MshanaJR
Swali murua sana
 
Ni siasa tu za kujipendekeza kwa mkuu. Mara unasikia mama katoa fedha, rais kaleta fedha, ina maana ana mfuko wake wa kutoa fedha kwa maendeleo ya taifa? Mpaka mwenyekiti wa kijiji anaimba wimbo wa mama katoa fedha katujengea dispensari, kaleta fedha katujengea madarasa ya shule! Hapa sentensi sahihi inatakiwa kutamkwa hivi: serikali imetoa fedha, fedha ni za serikali na si za kiongozi. Hata kama kiongozia ana fedha za kugawa kwa maendeleo ya nchi zitaundiwa mfuko. Zikitoka itasemwa zimetoto kwenye mfuko wa taasisi husika kama mfuko wa mwalimu nyerere, mkapa fellow, taasisi ya moyo ya jk, bill and melinda gate foundation na nyinginezo. Labda mama ana taasisi ya kitaifa kutoa fedha za maendeleo ya nchi.
 
Kwa hakika kuanzia wanachi wa Tanzania [emoji1241], na viongozi wameharibiwa sana na CCM.

Yani najaribu ku imagine! Pale marekani mbunge asimame aseme tunamshukuru Biden kwa kutoa pesa kwaajili ya miundo mbinu au namna yoyote ile, aiseee haiwezi tokea

Rais hana pesa za kufadhili miradi bali ni ujinga mkubwa sana kwa viongozi wetu wenye, PhD za kupewa udom( serious kidding [emoji38]). Lakini pia kutokujitambua kwa wanachi wenyewe ambao ndio walipa kodi.
 
Back
Top Bottom