The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Swali Kwa swali!
Kwa uono wako,
Lissu akichaguliwa Kuwa Rais Leo,vatafuta manunuzi ya V8 nchini ikiwa ameridhia wananchi wamnunulie V8 mpya Kwa kuchangishana?
Nijibu Kwa HOJA.
Hoja yako ni ya kipuuzi na haina mantiki...
Kwani hizo V8 ziko kwa ajili wanyama au watu...?
Kwani huko serikalini nani kukuambia kuwa gari V8 wakati wowote na kwa yeyote hazitakiwi kabisa...?
Kinachopigiwa kelele serikalini wala siyo uwepo wa magari aina ya LandCruiser V8...
Kinacholalamikiwa ni vipaumbele ktk matumizi ya fedha za umma...!!
Mfano huwezi kuwa na shida ya maji mahali fulani na kukawa na hitaji la mradi wa milioni 500 Ili unufaishe wananchi 200,000 halafu ukachukua hizo milioni 500 ukanunua gari la Mkurugenzi fulani mmoja tu...
Huu ndio udwanzi tunaoupigia kelele...!!
Lakini kama pesa ya mradi wa maji ipo, za ujenzi wa barabara zipo, za kununua vitabu vya wanafunzi mashuleni zipo, za kukamilisha miradi ya ujenzi wa reli ya SGR zipo na za kununua magari V8 zipo, then, kwanini gari zisinunuliwe na kupewa viongozi Ili wazitumie kufanya kazi zao...?
Back to Tundu Lissu..
Kwa hiyo ndo kusema kuwa, hoja yako is quite irrelevant....
Kwa sababu wananchi ndio wameamua wamchangie pesa Ili anunue gari moja tu imara na lenye nguvu ili limsaidie kwenye shughuli zake za kuizungukia nchi kwa shughuli za kisiasa kutoa elimu ya uraia...
Binafsi, nadhani, hata ingewepo gari ya Billion 1 na fedha ikawepo, apewe gari hiyo kwa sababu matumizi yake ni justifiable...