DPW ndiye mwenye mzigo wote uliopo DRC na Rwanda. Na ndiye mwenye kuutoa huko akauleta bandarini na kuupeleka sokoni.
Logistic supply chain yote ameikamata huyu mwarabu. Rais Tshisekedi alikuja nchini na siku hiyo hiyo akaenda kuikagua bandari.
JPM ziara yake ya kwanza kabisa alikwenda Rwanda akaonana na Kagame akapewa ngombe kadhaa walionona, wajuaji tukasema madikteta wawili wanatafutana kisiasa kumbe ni kuweka sawa suala zima la kuuleta hiyo mzigo kutoka Rwanda.
Baada ya ziara ile ikajengwa reli ya SGR na JPM akapinga kuiona ikienda DRC akapambana mpaka imekwenda Kigali, ili kuuchukua mzigo na kuiwahi hii tenda ya DPW.
Haya yote yanafanyika kimkakati tangu 2015, hivyo Samia anaendeleza kile ambacho JPM iwapo angekuwa hai leo hii angekuwa anakifanya.
Na tumeamua tu kuwa wabaguzi. JPM angekuwa amepewa siku za kuishi mpaka muda huu angeshamaliza hii shughuli na hakuna yoyote ambaye angehoji wala kuleta fyokofyoko.
Tumemuona mwanamama wa kizanzibari tena mpenda demokrasia ndio kila mtu sasa hivi anafungua mdomo wake eti kupinga uwekezaji.